Dondoo ya leo

Dondoo ya leo

jabirj864

Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
9
Reaction score
13
KUNA MWALIMU MMOJA ALIINGIA DARASANI AKAANDIKA UBAONI KAMA IFUATAVYO:

(1) 9+1=70
(2) 9+2=11
(3) 9+3=12
(4) 9+4=13
(5) 9+5=14
(6) 9+6=15
(7) 9+7=16
(8) 9+8=17
(9) 9+9=18
(10) 9+10=19

Alipomaliza kuandika tu, akaona wanafunzi wote walikua wanacheka, kwasababu alikua amekosea swali la kwanza.

Akawatazama wanafunzi, kisha akawaambia yafuatayo:
"Nimejikosesha lile swali la kwanza makusudi, kwasababu nilihitaji mjifunze kitu kimoja muhimu sana.Mnapaswa kujua namna ambavyo dunia inaweza kuwachukulia. Unaona hapo, nimeandika kwa usahihi maswali tisa (9), lakini hakuna kati yenu aliyenipongeza kwa hilo; wote mmecheka na kunilaumu kwasababu ya kosa moja tu nililofanya."

HIVYO, HILO NI SOMO KWENU:

"Dunia haijali mazuri unayofanya hata ukiyafanya mara milioni, lakini fanya baya moja uone jinsi watakavyo kulaumu"

"Hata hivyo usikate tamaa, MARA ZOTE SIMAMA IMARA NA USHINDE VIKWAZO VYOTE"

Huu ndio ujumbe wangu kwenu siku ya leo.
Siku njema kwenu
 
Back
Top Bottom