Mbaga Lazaro
Senior Member
- Aug 9, 2020
- 132
- 108
Siku chache baada ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe Augustine lyatonga Mrema mke wake aliyefunga naye ndoa siku za karibuni amefunguka mbele ya wanahabari mambo mbalimbali ilkiwa pamoja na anayodai ni usia alioachiwa na marehemu mume wake pamoja na matumaini yake baada ya kifo cha mumewe.Ikumbukwe kwamba baada ya kifo cha mumewe maoni mengi yametolewa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu maisha yake baada ya kifo cha mumewe hasa ukizingatia kwamba ndoa Yao haikufanikiwa kudumu kwa muda mrefu (kutokana na kifo cha mumewe) ukizingatia swala la kurithi Mali.Wapo wanaodai hastahili kupata mgao kwa kua kwa muda waliofanikiwa kuishi pamoja si rahisi kwamba walichuma Mali pamoja kumstahilisha urithi,wapo wanaosema hawakufanikiwapata mtoto pamoja hivyo kumpunguzia vigezo vya urithi.Wapo wanaodai alijiegesha kiujanja ujanja ili apate Mali japo mwanamama huyu alishawahi kusikika akisema anamiradi yake(ya Maua ) maeneo ya Moshi hivyo kilichompeleka kwa mzee Ni upendo na si Mali .Ikumbukwe kwamba siku za karibuni imejitokeza minong'ono na hata kufikia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwamba huko ndani Hali si shwari.Ati wasema magari yanatolewa Hadi baadhi ya vifaa [emoji87]Amesema pamoja na changamoto alizopitia na anazopitia anaimani mtetezi wake yu hai na ama hakika mungu yu hai atampigania.
Nukuu
[emoji116]
"yapo yanayosemwa kwa kuyashuhudia kwa macho, ninaamini baba hajafunga macho, kama alivyoniahidi, kuwa hata akifa hatafumba macho, na ninaamini katika maneno yake."
"Sitakuwa na hofu wala sitakuwa na huzuni kwani naamini nimeachwa katika mikono salama. Bado nitaendelea kuishi kwa unyenyekevu, kama niliyekuwa mke wa Mrema, nitaendelea kuwaheshimu na kuwapenda wale ambao niliachwa kwao kama mke wa ndugu yao," amesema
"Nitaendelea kuwa mnyenyekevu kwa Serikali ya Tanzania na Watanzania wote na wote waliokuwa na mapenzi mema na familia ya Mrema" ameeleza
Amesema yapo mengi yanayozungumzwa kuhusu hatma yake akibainisha kuwa yapo baadhi yana ukweli na mengine ni upotoshaji.
"Yapo mengi yanayozungumzwa kwenye vyombo vya habari juu ya hatma ya maisha ya Doreen, yapo ambayo ni ya kweli na hayahitaji uchunguzi wa kiintelijensia na kimaabara."
"Lakini yapo ya upotoshaji kwa sababu ya dhamira mbalimbali nisisitize tu kwa kuwa changamoto zozote zilizotokea na zinazotokea naendelea kuzihifadhi lakini ninaamini mtetezi wangu yu hai” amesema na kusisitiza
“Niendelee kuwahakikishia Watanzania nitamuenzi mume wangu mpenzi na kuishi vile alivyoniasa na kunihusia, muondoe shaka juu yangu ila tumaini langu na imani yangu ni kwa Mungu aliye hai atampigania.
Nafikiri Dada huyu anapitia wakati mgumu kwa namna moja au nyingine anastahili kufarijiwa na watu wa karibu na watu wa unasihi pia wakimtembelea ni vizuri .Anaweza akawa anawaza kweli hilo la Mali kwamba je nitapata Mali Kama mke halali au la.Je aachane na yote akaolewe na na mwingine(ukizingatia bado kijana)
Lakini Pia wajuvi wa mambo ukizingatia wapo wadau wa Sheria humu na wafukunyuzi vp baada ya kufunga
ndoa Alikuwa mke halali wa ndoa Ila ukizingatia muda mfupi alioishi na mume wake stahiki zake Kama mke zinakuwa katika utaratibu upi Kama elimu kwa walio wengi kwani tumeshuhudia matatizo makubwa anapoondoka mtu na ukute ameacha mali . Just elimu kwa uma