ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
Tunasimama na Wafanyakazi Tanzania, Kikotoo cha mafao kinawaumiza wafanyakazi.
Chama cha ACT Wazalendo kinaungana na wafanyakazi wote Duniani katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi. Siku hii ni muhimu sana katika kuwaleta pamoja wafanyakazi katika kutafakari hali yao, maslahi na stahiki zao. Wafanyakazi ndio wajenzi wa nchi kwa kukuza uchumi, kuimarisha huduma na uzalishaji wa mahitaji ya msingi.
Tunatambua kuwa hapa nchini Tanzania hali ya wafanyakazi si nzuri. Kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipunjwa maslahi yao kutokana na Sera, Sheria na Kanuni kandamizi zisizojali maslahi yao.
Chama chetu kimekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki na maslahi ya wafanyakazi. Tunataka wakati wote masuala ya wafanyakazi yawekewe taratibu, kanuni, sheria na miongozo yenye maslahi kwao. Vile vile, tunapigania kuhakikisha kuwa maslahi yao yasiamuliwe na utashi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika mwendelezo wa madai ya wafanyakazi tunaitaka Serikali kuchukua hatua zifuatazo;
i. Kumaliza mgogoro wa Kikotoo cha pensheni za wastaafu kwa kurejesha kanuni za zamani za kukokotoa mafao zilizotumika kabla ya mwaka 2017. Tunataka wastaafu walipwe 50.5% ya pensheni kama kiinua mgongo kwa kikotoo cha 1/540 na kwa maslahi yao yote.
ii. Kulipa madeni yote ya wafanyakazi yanayohusisha, malimbikizo ya mishahara, likizo, kujikimu, uhamisho na posho za kisheria.
iii. Serikali na sekta binafsi zipeleke michango yote ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii (NSSSF, PSSSF na WCF) kiasi cha Shillingi billion 856 ambayo kwa muda mrefu haijawasilishwa ili mifuko hiyo iweze kuwahudumia wafanyakazi.
Mwisho, Serikali iache kuingilia vyama vya Wafanyakazi nchini. Tunavisihi vyama vya wafanyakazi viendelee kupigania maslahi ya wafanyakazi, aidha tunawatia ari wafanyakazi waendelee kufanya kazi kwa bidii na wasichoke kupambania haki na maslahi yao kila wanapopata nafasi, wasichoke, ACT Wazalendo tupo nyuma yenu wakati wote.
Imetolewa na,
Ndg. Dorothy Manka Jonas Semu
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo.
Mei 01, 2024