Mshirikishe mwenzako
Image copyrightGetty
Image captionPierre-Emerick Aubemeyang
Kilabu ya Ujerumani Borussia Dortmund imemaliza uvumi kwamba mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubemeyang huenda akaihama kilabu hiyo katika dirisha la uhamisho mwezi huu.
Dortmund imesema kuwa itawashikilia wachezaji wake wote hadi mwisho wa msimu akiwemo nyota wake Aubemayang ambaye alishinda taji la mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2015.
Arsenal inadaiwa kuwa miongoni mwa timu zinazomwinda mshambuliaji huyo .