hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,544
Salaam.
Nianze kwa kuwapongeza watu wote waliojiandikisha kupiga kura, tangu zoezi la kujiandikisha lilipoanza ingawa kulikuwa na changamoto nyingi karibu maeneo yote ya uandikishwaji.
Sasa uandikishwaji umekamilika na katika kuhakiki ndipo changamoto nyingine ilipo/inapozuka! Watu kujiandikisha na kupewa kitambulisho halali cha mpiga kura lakini kukosa majina yao katika orodha ya watu wakiohiandikisha. Nimejaribu kuuliza na kufuatilia maeneo tofauti tofauti ambapo maeneo mengine wanasema, "hata kama jina halipo utaruhusiwa tu kupiga kura" na maeneo mengine wanasema, ".. ni lazima kujihakikisha kwanza hata kama una kadi tayari kwani hutapiga kura"
Ni wazi kwamba majina haya yanatolewa katika maeneo maalumu tu. Pili, ni wazi kuwa si wote huwapo maeneo hayo(mf. watu waliojiandikisha lakini kusafiri n.k).Ninachojiuliza
1. Kwanini kuingia gharama za 'maigizo' haya ya kuhakiki wapiga kura kama watu watapiga kura regardless of majina kutokuwepo?
2. Ni hatua gani sahihi zinazopaswa kuchukuliwa mtu atambuapo jina lake halipo katika orodha ya wapiga kura?
3. Je, muda utatosha kuhakikisha uthibitifu wa wapiga kura hawa?
4. Kwanini hadi sasa Serikali iko kimya kuhusu hili?
5. Je, Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imeyaona mapungufu haya na nini hasa ni mpango wao?
6. Wapiga kura(wananchi) hatuoni hili? Wananchi(mmoja mmoja) wamejiandaaje endapo wasipokuta(hutakuta) jina lako despite kujiandikisha au kujiandikisha na kuhakiki?
Ni dhahiri hii italeta dosari katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu. Vyama vya siasa vimepangaje wapiga kura wao? Serikali inasimamiaje hili kuhakikisha misingi ya kiongozi aliyepatikana kwa haki na atakayesimamia Utawala bora anapatikana?
Nchi hii ilikuwa ya amani(sasa ni utulivu), lakini tusitegemee hata utulivu huu kuwepo Oktoba 25 na baada ya hapo, hasa kwa watu walioamka saa tisa usiku na kulala vituoni ili kujiandikisha na kuambulia kuandikishwa mchana na wengine jioni then akose jina lake kisha umwambie asipige kura?!
Tulijua kuwa mwaka 2015 kutakuwa na Uchaguzi Mkuu, tukajua kuna umuhimu wa kuwa na "daftari la wapiga kura" na tukajua changamoto zote(anticipation) za Electronic device, mlolongo wa uandikishwaji, mchakato wa kuhakikisha mtu aliyejiandikisha lakini bado tukafanya jambo hili kama wote tulikuwa tumesafiri na kurudi nchini kwa pamoja na kukuta taarifa hizi.
Ingawa ni dosari lakini ni aibu kubwa kutokuwa na umakini katika mambo yanayoweza kuamua mustakabali wa Taifa kwa kuyafanya kama 'crash program'.