Dossa Aziz Aliposahauliwa Kupewa Medali 1985

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
DOSSA AZIZ ALIPOSAHAULIWA KUPEWA MEDALI 1985

Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa.

Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh Abdallah Chaurembo.

Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima.

Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu.

Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana.

Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka.

Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandizi, maili chache nje ya Dar es Salaam.

Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.

PICHA: Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akimvisha Dossa Aziz medali Ikulu.
337375039_179499601512247_7206813553512566677_n.jpg
 
Historia nzuri. Niliwahi kusikia kuwa familia ya Hamza ilipora mali zilizoachwa na baba yao ikapelekea Dossa kuwa hana kitu akaukimbia mji.
 
Baba wa taifa alikua na roho ngumu Sana...hasa ukifikiria alichowafanya wale waliomkaribisha kwenye siasa na kupambana akubalike kwa hadhira ambayo ilikua haimtaki
 
Historia nzuri. Niliwahi kusikia kuwa familia ya Hamza ilipora mali zilizoachwa na baba yao ikapelekea Dossa kuwa hana kitu akaukimbia mji.
Gagna,
Aziz Ali alipokufa 1951 Hamza alikuwa mdogo hata kuoa bado.
 
Kuna sehemu umeandika kuwa siku za mwisho Dossa hakuwa vizuri kiuchumi, tofauti na kina Ally Sykes. Nini kilimfilisi huyu mzee wetu?
 
Back
Top Bottom