Wakuu wanasheria, naomba msaada, ikibainika kuwa kamishina wa ardhi ametoa hati mbili tofauti kwa kiwanja kimoja kwa wakati tofauti, je, hapo haki inafanyikaje kumpata mmiliki mmoja abakie na kiwanja?
Haki ya kumiliki ardhi, Mara nyingi kumetokea na ukiukwaji wa taratibu zinazohusiana na usajili wa ardhi.
Hii kadhia mara nyingi husababishwa na utawala mbovu na matumizi mabaya ya ofisi katika ngazi mbalimbali zinazohusika na utoaji ardhi, matokeo yake kuzuka migogoro mbalimbali ya ardhi miongoni mwa wananchi.
Madai mengi kuhusu umiliki na utoaji vibali vya umiliki ardhi hutokea kkt njia nyingi miongoni mwa hizo njia zifuatazo ni miongoni mwao;
i. Umiliki
Hii hutokea wakati watu wawili au zaidi kudai umiliki juu ya kipande kimoja cha ardhi kila mmoja akidai kuwa ni mmiliki halali.
Hali hii hutokea wakati mamlaka mbili tofauti zenye kutoa haki ya umiliki ardhi kutoa vibali tofauti kwa watu wawili tofauti bila ya taarifa sahihi kwa kila mmoja juu ya umiliki wa ardhi.
-ii. Mgogoro kati ya sheria za kimila na sheria za nchi .
uwepo wa aina mbili wa haki za kumiliki ardhi ambazo ni sheria za nchi juu ya haki ya kumiliki ardhi na haki za kimila za kumiliki ardhi katika kipande cha ardhi hasa katika vitongoji vya miji ya eneo mara pia zimepelekea migogoro kwenye umiliki WA Ardhi.
Kwa kuwa hii ni assignment Fanya yafuatayo;
Soma cases
Prof. Bernard Kiree v Natarino Mwenda
Amritlal v city council of Nairobi (1982)1 KIR
Alhaji Dahou Saude v Alhaji Hallim Abdullah (1989)
Soma Ripoti ya Issa Shivji (Presidential of inquiry into land matters: Chapter 2 )
Soma Acts of the Parliament
-The Land Act, Cap 113
ss. 19,22,25,26,28, na 29.
Subpart 4 soma yote.
The Village land Act, Cap 114
The Courts ( LAND DISPUTES
SETTLEMENTS ) Act, 2002
Vitabu
Essays in Land Law in Tanzania by Mgongo Fimbo
Land Law Manual by Tenga , Ringo & Sist Joseph
Land as a Human Right: A History of Land Law and Practice in Tanzania by Abdon Rwegasira
The Land Law of Tanzania :
Cases Book : by Prof Mgongo G.
Fimbo
The Land law of Tanzania: Source book by R.W. James and G.M.
Fimbo
"If you wish to be a lawyer, attach no consequence to the place you are in, or the person you are with; but get books, sit down anywhere, and go to reading for yourself.
That will make a lawyer of you quicker than any other way" -Abraham Lincoln.