Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Sikumbuki ilikuwa kitu gani lakini ninachokumbuka ni kuwa nilikuwa likizo Tabora niko uani na bibi yangu Zena bint Farijala 1965 nadhani ilipigwa nyimbo ya Salum Abdallah katika radio bibi akaniona nimeifurahia ile nyimbo ndipo akaniambia, ''Salum Abdallah alikuwa rafiki sana ya baba yako. Akija Tabora na bendi yake lazima aje hapa nyumbani kumsalimu baba yako.''
Bila shaka hii ilikuwa katika miaka ya 1950 wakati Salum Abdallah anaanza muziki wake.
Naikumbuka ''gramaphone'' ya mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed na santuri za Salum Abdallah ''label'' yake ilikuwa inaitwa ''Jambo.''
Miaka mingi baadae nikiwa Nairobi, Muthaiga nyumbani kwa Peter Colmore tukila chakula cha mchana na rafiki yake mmoja Mwingireza mwenzake tukawa tunazungumza kuhusu mwanzo wa utangazaji wa radio Tanganyika kupitia ''Sauti ya Dar es Salaam,'' 1952.
Huyo rafiki yake Colmore akamtaja Salum Abdallah na kampuni ya Jambo iliyokuwa ikirekodi muziki wake.
Kampuni hii ilikuwa ya Mwingereza akiitwa Guy Johnson.
Hadi leo bado ninazikumbuka nyimbo zile za Salum Abdallah nilizosikia labda nina miaka mitano hivi nyumbani kwa mama yangu Mtaa wa Kiungani, Gerezani.
Sina hakika na majina ya hizi nyimbo ila nakumbuka maneno yake.
Kuna nyimbo moja Salum Abdallah anasema, ''...na hapa nilipokuwa nipo chini ya mkungu nangoja litoke jua liangaze ulimwengu...''
Hizi nyimbo inasemekana zimepotea.
Fred Macha alipata kufanya mahojiano na mke wa Salum Abdallah na Fred akamuomba amuonyeshe santuri za mumewe.
Hakuwa hata na moja.
Msiba mkubwa.
Frank Humplink alikuwa rafiki baba yangu nikifika Lushoto lazima niende kumwakia nyumbani kwake.
Mzee Humplink hakuwa hata na santuri yake moja pale nyumbani.
Siku moja nilimuona Salum Abdallah Mtaa wa Stanley na Nyamwezi, mbele ni Mtaa wa Swahili.
Kulikuwa na Cuban Marimba Chacha Band Branch.
Nimemkuta amekaa ndani na mwenzake, Salum Abdallah kashika guitar anapiga.
Ilikuwa mwaka wa 1964.
Sikunyanyua mguu.
Mwaka uliofuatia Salum Abdallah akafariki.
Muda mrefu natafuta picha za Salum Zahoro na Kiko Kids sijazipata juu ya kupita hata kwa ndugu zake na yeye mwenyewe.
Salum Zahoro nilikutananae kiasi cha miaka 20 iliyopita karibu ya Shule ya Uhuru alikuwa akisubiri usafiri na mimi nilikuwa na binamu yangu Bi. Zuhra bint Hussein Milala ambae amefariki wiki iliyopita.
Tulikwenda kumwamkia nami hapo ndipo nilipopata kumuona kwa karibu.
Mtu mtanashati nilipoangalia nguo alizovaa na Allah amemjalia sura jamil sana.
Salum Zahoro akifahamiana na baba yangu toka ujana wao na alikuwa na kila santuri yake akiwa na Kiko Kids.
Hadi leo naikumbuka record player na radiogram za baba ambazo alikuwa kaipiga miziki yake aliyokuwa akiipenda.
Nakumbuka ni baba ndiye aliyenifahamisha kuwa Salum Zahoro alikuwa akipiga mandolin siyo guitar.
Picha hiyo hapo chini inamuonyesha Salum Zahoro akipiga Electric Mandolin akiwa na Shikamoo Jazz Band.
Juu ya mchango wa Salum Abdallah kwa nyimbo zake za kuhamsisha Watanganyika wakati wa kudai uhuru mfano wa ''Ndege Mwekundu anampiga Ndege Mweupe na Ndege Mweupe anampiga Ndege Mweusi,'' mji wa Morogoro umeshindwa kumpa Mtaa Salum Abdallah.
Katika miaka ya 1980 nilimtembelea Mama Jamila dada yake Salum Abdallah na nikakutana hapo nyumbani kwake na mzee mmoja anaitwa Kivuli.
Katika mazungumzo nilimwambia kuwa baba yangu alianza kazi Morogoro Posta akiwa kijana.
Mzee Kivuli akaniambia, ''Wewe Mohamed mwanangu nikimfahamu vyema baba yako na alikuwa rafiki sana na kaka wa huyu mama mwenye nyumba hii, Salum Abdallah.''
Haya ndiyo maisha yetu historia zetu zote ziko mikononi mwa ndugu na jamaa na si muda mrefu zote hizi zitatoweka na tutabaki taifa lisilo na mashujaa wake.
Duka la Assand Sound Limited (ASL) chini ya duka lao River Road, Nairobi wenyewe walipata kuniambia kuwa wana ''vault,'' na humo wana miziki yote ya Afrika ya Mashariki.
Inahitajika juhudi kidogo sana ya kuweza kupata miziki yote ya Tanganyika toka enzi na enzi tukaileta nyumbani na kuihifadhi kwa ajili ya kizazi kijacho.
Miziki hii imebeba historia kubwa kama kielelezo cha nchi yetu.
Picha za chini kushoto katikati ni Salum Abdallah, Frank Humplink akiwa Nairobi miaka ya 1950/60 na mwisho ni Peter Colmore na huyo aliyenae ni rafiki yake jina sikuhifadhi aliyenipa historia ya kampuni ya Jambo iliyokuwa inamilikiwa na Muingereza Guy Johnson.