Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
DOWN MEMORY LANE (SEHEMU YA PILI)
INAENDELEA... IKIMWANGAZA SALIM HIMIDI
Kushoto ni Salim Himidi, Ahmed Rajab na Waziri Simba Trafalgar Square London 1960s katikati
Waziri wa Nchi za Nje wa Comoro Salim Himidi akihutubia UNO
INAENDELEA... IKIMWANGAZA SALIM HIMIDI
Kushoto ni Salim Himidi, Ahmed Rajab na Waziri Simba Trafalgar Square London 1960s katikati
Waziri wa Nchi za Nje wa Comoro Salim Himidi akihutubia UNO
Rafiki zangu wawili wote ni waandishi wa sifa na wote wakiwa Ulaya baada ya kusoma makala iliyopita niliyomtaja Salim Himidi niliyemtaja kwa sifa kubwa nimekuwa kama nimechokoza nyuki wakali kwani wameniangushia vitu si vya kawaida.
Mmoja kaniandikia ananiambia, ''Umemzungumza vizuri Salim Himid. Shukran. Huyu ni mtu mwenye vipaji vingi...an intellectual per excellence.''
Huyu aliyeandika maneno haya namfahamu na si mtu wa kutupa maneno yake ovyo.
Nimeona nina wajibu nika-share na nyie ndugu zangu yote waliyonikusanyia na kunirundikia mimi peke yangu zikiwapo na picha zenye umri wa zaidi ya miaka 50.
Huu kwangu ni mzigo mzito.
Kuna mhariri wa gazeti kubwa sana Afrika Mashariki nilimpelekea makala ya Sal Davis ambae kwa miaka mingi alikuwa katoka katika ‘’lime light,’’ kapotea hayuko kabisa.
Mhariri kaipenda makala lakini akanipigia simu kutoka Nairobi akanambia gazeti lake haliwezi kunipa mimi publicity ya bure. Mhariri kasema maneno haya kwa kuwa nilimweleza Sal Davis kupitia kumbukumbu zangu na za wenzangu tuliokuwa tukimuusudu katika miaka ile ya 1960 wakati Sal Davis jina na muziki wake ulitawala, ‘’air waves,’’ zote Afrika ya Mashariki.
Nakumbuka nilianza na makala yangu natambuka kizingiti cha nyumba ya baba yangu mkubwa Bwana Humud Salum Abdallah aliyekuwa akiishi Mtaa wa Kipata, naingia ndani nasikia kutoka radio yake kutoka TBC inapigwa nyimbo ya Sal Davis , ‘’Makini.’’
Hii ilikuwa mwaka wa 1963.
Mhariri hakupenda hii akanambia ondoa hayo yako tuandikie makala ya Sal Davis.
Lakini kabla ya kukata simu akaniuliza imekuwaje nimemjua Sal Davis kwa kiasi kile?
Nikamwambia ni Land Lord wangu hapa Dar es Salaam.
Niliiandika upya makala ile na ilipochapwa katika gazeti washabiki wa Sal Davis sasa watu wazima wakawa wanauliza yuko wapi Sal Davis na anafanya nini hivi sasa.
Sasa marafiki wa Salim Himidi nao wameniandikia nami ninaandika lakini kwa mtindo ule ule uliokataliwa na Mhariri yule wa gazeri la Kenya.
Katika hiyo picha ya kwanza niliyotumiwa wa kwanza kushoto ni Salim Himidi, Ahmed Rajab na Waziri Simba.
Hawa vijana watatu walipiga picha hii katika miaka ya katikati 1960 na wote walikuwa wanafunzi Waziri Simba akiwa Sandhurst Royal Military Academy.
Hii picha mimi nimeiona 1966 hivi hapo katikati nyumbani kwa kina Simba Waziri Mtaa wa Tandamti kanionyesha mdogo wake Simba Waziri marehemu Iddi Waziri aka Iddi Rumania, brilliant footballer jina hilo la ''Rumania,'' alipewa baada ya kwenda na Yanga Rumania.
Baada ya miaka mingi kupita baada ya kufika Uingereza nikajua kuwa ile picha niliyoiona nikiwa na umri wa miaka 14 hivi ilipigwa Trafalgar Square.
Alama kubwa ya Trafalgar Square ni hawa njiwa katika picha.
Wakati ule haukunipitikia hata kwa mbali kuwa itakuja wakati nitakuwa naingia na kutoka Uingereza kama mchezo.
Ahmed Rajab alinipitisha Trafalgar Square siku moja kunionyesha wanafunzi waliokuwa wakija kwenye Ubalozi wa Afrika Kusini uliokuwa sehemu zile ambao walikuwa wakijifunga minyororo nje ya ubalozi ule kama kampeni ya kushinikiza Nelson Mandela afunguliwe kutoka jela.
Wanafunzi hawa walikuwa wakipeana zamu ya kuja kujifunga minyororo kwenye nguzo hapo nje ya ubalozi kwa mwaka mzima.
Hawa kaka zangu wote wamefanikiwa katika maisha na nikisema niandike waliyokamilisha hatutotoka hapa haraka na hawa wote ni watu ninaowajua vizuri na kwa karibu sana.
Ahmed Rajab haitaji kuelezwa.
Simba Waziri Simba amestaafu jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) akiwa Brigadier General.
Namkumba London miaka ya 1990 na Mercedes Benz nyeusi yenye namba za kibalozi akiwa Military Attache.
Siku moja tukakutana Tehran Iran kwenye mkutano...picha ya mwisho.
Turejee kwa Salim Himidi.
Mmoja wa marafiki zake Salim Himidi kaniandikia maneno haya:
''Salim aliwahi pia kuombwa na waliomfunga baada ya mapinduzi kuwasaidia.
Alikuwa Katibu Mkuu Ikulu na Mshauri wa Rais Said Mohamed Djohar na Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya Mohamed Taki Abdulkarim.
Wakati wa utawala wa Ali Saleh alikuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa wa ngazi ya juu na akiangaliwa kuwa mtu wa pili kisiasa katika ngazi ya utawala.
Aliwahi pia kuwa Waziri wa Ndani, habari na msemaji wa serikali.
Alifanikisha Comoro kujiunga na Umoja wa Mataifa kutokana na kipaji chake cha diplomasia.
Salim Himidi binafsi anamshukuru Dr. Salim Ahmed Salim na mchango mkubwa wa Tanzania katika kusaidia ukombozi.
Dr. Salim aliyejuwana na wajina wake tokea ujanani wakiwa Zanzibar mbali ya kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa alikuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kupambana na Ukoloni ya Umoja huo (UN Decolonisation Committee) kwa muda wa miaka 10.
Kama ilivyo ada yangu nilimuomba Salim Ahmed Salim aandike memoirs zake kama nilivyomuomba kihutubia Umoja wa Mataifa akiwa kavaa kofia nzuri ya Kingazija.
Nikiwa Paris na Salim alinihadithia mchango mkubwa wa Salim Ahmed Salim katika masuala ya ukombozi na vipi walivyoingiliana katika mawanda ya diplomasia achilia mbali kuwa wote ni Wazanzibari.
Hii picha ya nne ni gazeti lililokuwa katika Maktaba yangu kwa miaka mingi sana cover yake ilikuwa hiyo picha ya Salim Ahmed na siku nilipokutananae nilimpa kama zawadi kutoka kwangu na ikasadifu kuwa hakuwa na gazeti hili katika maktaba yake.
Kama ilivyo ada yangu nilimuomba Salim Ahmed aandike ''memoirs,'' zake kama ninavyomuomba somo yake Salim Himidi kufanya hivyo.