Mikocheni,,,
Tatizo lako ni kuwa wewe huijui historia ya TANU.
Sikulaumu hauko peke yako wewe ni moja wa kundi kubwa sana wa wasiojua.
Mimi ''sidhanii'' katika historia hii nimefanya utafiti na nimeandika kwanza kitabu
na nina ''paper,'' nyingi nimeandika kuhusu somo hili kiasi nimeshirikishwa katika
miradi miwili ya kuhifadhi historia hii.
Nimeshiriki katika mradi wa Oxford University Press, Nairobi na wamechapa kitabu
nilichoandika, ''The Torch on Kilimanjaro,'' (2007).
View attachment 1178395
Nimeshiriki katika mradi wa Dictionary of African Dictionary (DAB) uliokuwa chini
ya Havard na Oxford University Press, New York (2011).
Kitabu cha
Sykes kimepitiwa na wanahistoria maarufu wanaoijua historia ya Tanzania
kama
John Iliffe, Jonathon Glassman na
James Brennan.
Ukimtoa
Iliffe hao wawili waliobakia tunafahamiana kwa miaka na kilichotukutanisha
ni historia hii.
Ningeweza kuendelea zaidi.
Lakini kubwa katika waasisi wa African Association (1929) aliyeandika historia hiyo ni
Kleist Sykes na walikuwa watu 9 hakuna aliyeandika historia hiii na moja ya sababu
ni kuwa michango yao haikuwa mikubwa sana na haikudumu kwa muda mrefu hivyo
hawakuwa na mengi ya kuandika.
Katika waasisi 17 wa TANU (1954) hakuna aliyeweza kuandika historia yake ukimtoa
Abdul Sykes na yeye aliweza kufanya hili kwa kuwa alikuwa anaijua historia yote na
alikuwa na nyaraka.
Jambo la kusikitisha ni kuwa historia hii
Abdul hakumaliza kuindika kwa sababu
palizuka sintofahamu kama hizi tunazojadili hapa hivi sasa.
Wewe huijui historia hii lakini hutaki kuwasikiliza wenye kuijua.
Hivi tunavyojadili, kutokana na kitabu cha
Sykes Prof. Shivji na wenzake wanaandika
kitabu cha maisha ya
Mwalimu Nyerere nia ikiwa pamoja na mengine, kujua nini
ulikuwa mchango wake katika kuunda TANU.
Naamini unauona mnyororo huo wa TANU kuanzia kwa
Kleist Sykes hadi kwa
wanae
Abdul na
Ally katika historia hii.
Ikiwa ipo historia ya TANU isiyo kuwa hii hadi hivi sasa kitabu kipo mwaka wa 20
bado hakijaandikwa.