Kifungu hiki hakiwezi kitumika katika nchi zetu ambazo zinaua kirejereja...
Mfano ni Rais wa zamani wa Sudan, Rais Al Bashir alituhumiwa kutenda makosa nchini kwake Sudani, na Sudani sio mwanachama wa Mahakama ya ICC; hakuna nchi yeyote iliyokuwa na uwezo kisheria kulipeleka suala hilo ICC, wala Mwendesha mashitaka kisheria hakuruhusiwa kuanzisha mchakato yeye mwenyewe, hadi pale Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipotoa Azimio la kupeleka maombi ICC ndipo mchakato wa kutoa hati ya kumkamata ulianza. Kama Balaza la Usalama lisingefanya hivyo hakuna chombo kingine kisheria ambacho kingeisukuma ICC kuanzisha mchakato dhidi ya Rais Omar Al Bashir.