Download kitabu cha ICC - The Hague bure

Sheria kwa Kiswahili

Senior Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
116
Reaction score
106
Wakati mwingine tumechanganya makosa yanayoshitakika ICC tukidhani ICC inashughulikia makosa yote. tumetengeneza tafsiri hii kwa ajili ya raia wa kawaida kabisa, ili watu tukisome na kujiepusha na yale yanayoweza kutufanya tuishie ICC au kusumbuliwa nayo.
 

Attachments

Kifungu hiki hakiwezi kitumika katika nchi zetu ambazo zinaua kirejereja...

Mfano ni Rais wa zamani wa Sudan, Rais Al Bashir alituhumiwa kutenda makosa nchini kwake Sudani, na Sudani sio mwanachama wa Mahakama ya ICC; hakuna nchi yeyote iliyokuwa na uwezo kisheria kulipeleka suala hilo ICC, wala Mwendesha mashitaka kisheria hakuruhusiwa kuanzisha mchakato yeye mwenyewe.

Hadi pale Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipotoa Azimio la kupeleka maombi ICC ndipo mchakato wa kutoa hati ya kumkamata ulianza. Kama Balaza la Usalama lisingefanya hivyo hakuna chombo kingine kisheria ambacho kingeisukuma ICC kuanzisha mchakato dhidi ya Rais Omar Al Bashir.
 
sijakuelewa, unauliza swali au unakosoa kipengele hicho?
 
Dah, kaka kitabu hiki ni kizuri. huo ukurasa wa 32 na 33 kuna madini fulani hapo ya kuteka watu na kunyanyasa watu na kufunga watu bila sababu, safi sana mwandishi. nilishawahi kukuona mahakama ya Tunduma kumbe umesoma kufika mbali hivyo...safi sana!
 
Shukrani sana kwa kitabu hiki adhimu, nimeweza kutofautisha kati ya ICC na ICJ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…