DP World hawakutaka kuwekeza Tanzania, walilazimishwa

CONSISTENCY

Senior Member
Joined
Feb 16, 2023
Posts
135
Reaction score
309
Baada ya kuona watanzania wamekataa mkataba wao uliohusu umiliki na uendeshaji bandari zote nchini Tanzania,
DP World wameamua kufichua ukweli kwamba walilazimishwa kuwekeza Tanzania kutoka kwa Rais Samia, hivyo wamesema iliwabidi kuweka mkataba wa hovyo na usiokubalika ili kukataa uwekezaji wao nchini Tanzania kwa namna yake.

DP world wamesema hayo baada ya Wananchi watanzania kukataa mkataba huo na kwenda mbali zaidi hadi kwenye vyombo vya umoja wa mataifa kutoa taarifa na tahadhari kuhusu mkataba wa hovyo kati ya nchi ya Tanzania na kampuni inayojihusisha na uendeshaji wa bandari duniani iliyopo dubai DP World.

Pia watanzania walienda katika kurasa mbalimbali za kijamii zinazotambulisha kampuni hiyo ya DP world kwa kuonesha masikitiko na malalamiko yao kwa kampuni hiyo kwa madai kwamba kampuni hiyo haihitajiki nchini Tanzania kwani mkataba huo una lengo la kupokonya uhuru wa nchi na kufanya watanzania kuwa watumwa kwa miaka mingi,
kitendo hicho kimechafua pakubwa taswira ya kampuni hiyo kimataifa.

Hivyo huu ni wito kwa Rais samia, siku nyingine usilazimishe wawekezaji ambao hawako tayari na hiyo ndio imekufanya ukubali masharti ya kishetani kabisa ambayo hata haujayatafakari.

Pia rais samia jifunze kufata taratibu za dhabuni unapotaka wawekezaji eneo fulani sababu, duniani kuna kampuni nyingi kubwa na nzuri zinazohusika na uendeshaji wa bandari, kampuni nyingine ni kubwa kuliko hata hiyo DP World iliyokupa mkataba wa kishetani na usiotekelezeka

Hivyo Rais samia rudi bungeni na kufuta huo mkataba baada ya hapo tangaza dhabuni kuhusu uendeshaji na watanzania tuna uhakika utapata kampuni nzuri ambayo haitokupa masharti ya kishetani yatakayokufanya ukosane na wananchi unaowaongoza

Zifuatazo ni kampuni kubwa duniani zinazohusika na uendeshaji wa bandari
1. PSA International - singapore
2. COSCO Shipping Port - China
3. APM Terminals
4 Hutchson Port Holdings - Hongkong
5. AP Mollers Terminals - Netherlands
6. China Merchants Ports Holdings
7. Terminal Investment Ltd - Switzerland
8. International Container Terminal - Phillipines
9. Eurogate Container Terminal - Germany
10. Evergreen Marine Corporation - Taiwan
11. N.k

Miongoni mwa hizo kampuni zina ukubwa na ufanisi zaidi kuliko hata hiyo DP World iliotoa mkataba wa ajabu.

Hivyo rais samia futa huo mkataba wa ajabu na DP world kisha tangaza dhabuni au serikali itafute wawekezaji wenye uwezo wasio na masharti ya kitumwa kama hao waarabu wa DP World.
 
Kama hao DP wameongea hivyo,basi duniani huko tunaonekana wajinga sana
 
Hajachelewa auvunjilie mbali kutuliza vumbi lililotimka
 
Magu alikuwa raisi wa hovyo kuwai kutokea duniani lakini mama amekuwa hovyo maladufu
 
Linawezekana?.
 
Wamelazimishwa alaf wao tena wahonge hela watu ili wapigiwe chapuo,

Kwahivyo Mbunge Msukuma, kitenge, na wengineo wamehongwa na nani kupush agenda
 
Ndo uone watanzania walivyo vilaza
 
Tunaomba chanzo cha taarifa hii kama uthibitisho ni kweli wamesema hivyo.
 
Mleta mada usipokuwa makini, tutakuona wewe ni sawa na Zenbwela, Msukuma, kitenge au Kibajaj😠
 
Back
Top Bottom