DP world kupewa bandari, kanisa katoliki limekosa ushawishi?

DP world kupewa bandari, kanisa katoliki limekosa ushawishi?

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Posts
4,611
Reaction score
5,009
Salam kwenu Watanganyika na wazanzibari!

Tumeshuhudia Dp world wakiripotiwa kuwa wameanza majukumu pale bandari salama. Hatua kadhaa zimekuwa zikuchukuliwa kuweka mifumo yao sawia.

Sote tunafahamu, kanisa takatifu katoliki lilisimama na kinachosema upande wa wananchi kuhoji uhalali wa mkataba huo wa serikali na dp wedi. Sijui habari za EGA na IGA naona hazijafua dafu.

Tangia hapo sio kanisa lilitoka mbele kuonesha kubadili mtazamo wake ama lah.
Tunafahamu nguvu waliyonayo, hasa ukizingatia safari ya rais Vatican ambayo ilitajwa kama kwenda kueleza maamuzi haya ya serikali kuwapa bandari DP world.

Dp sasa wanaonekana viungani, je serikali imepata ushindi dhidi ya kanisa katoliki?

Ama je, kuna mipango gani kanisa linafanya kuendelea kuonesha ukubwa wake?

Kwa nijuavyo huwa waachi mambo yakajiendea tu hasa ambayo wanayakemea. Tutarajie nini hasa?

Maswali ni mengi.
 
Back
Top Bottom