VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Tanzania hii si ile. Watanzania hawa si wale. Wakati wetu (tukiwa kwenye kutumikia Serikali na chama), ilikuwa rahisi kama kula bisi kuwaaminisha watanzania juu ya jambo fulani.
Ilikuwa rahisi kuwaambia Tanzania kuwa jezi za Simba ni za njano na za Yanga ni nyekundu. Na waliamini. Propaganda zilitamalaki.
Kulikuwa na sababu. Wengi wetu hawakuwa na elimu na utambuzi. Elimu ya darasani na hata ile ya mtaani iliwafikia watu wachache sana.
Wengi walikuwa mbumbumbu wa kielimu na kiutambuzi. Walikuwa na macho lakini hawakuwa wanaona. Walikuwa na masikio lakini hawakuwa wanasikia. Watanzania wa sasa, wanaona na wanasikia.
Kitendo cha watanzania wa kila aina kujitokeza na kupinga kwa namna mbalimbali Mkataba wa DP World wa kukodishwa Bandari zetu za Tanzania Bara si cha bahati mbaya.
Ni kwakuwa muda umefika. Watanzania wamefikia kwenye ukomavu wa kifikra; kimbinu na kiutendaji. Watanzania hawa hawayumbishwi na hawatishwi.
Watanzania wa aina hiyo wapo kila mahali: kwenye Serikali; chamani; kwenye wasomi; kwenye vyombo vya ulinzi na usalama; mitaani; mitandaoni; mijini na vijijini.
Amini nawaambia, hakutafichwa chochote chenye ukakasi na viongozi wetu kisiwekwe hadharani na watanzania hawa. Hata mikataba itakayofuata kuihusu Bandari yetu au popote pale, itaanikwa kama itapangwa kufichwa.
DP World imeonesha sura halisi ya watanzania wa sasa. Imeonesha jinsi watanzania wanavyoweza kupinga, kukosoa, kuongea, kujiamini, na kutobabaishwa na vitisho au propaganda.
Viongozi wetu wa Serikali na CCM wanapaswa kutishwa kuliko kawaida. Watishwe zaidi na jinsi watanzania wanavyopuuza mikutano ya viongozi wa CCM wanaozunguka nchini kuaminisha wananchi kuwa Mkataba wa Bandari ni mzuri.
DP World ni mwanzo tu, mengi yatafuata. Wa kujifunza na ajifunze sasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mbeya)