SI KWELI DP World yaingiza magari yake Bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kuanza kazi

SI KWELI DP World yaingiza magari yake Bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kuanza kazi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
F1oddlEXwAAkUkv.jpg

Picha hii inasambaa mtandaoni. Inadaiwa kuwa magari haya yapo Bandari ya Dar es Salaam, yameingizwa nchini na kampuni ya DP World tayari kwa kuanza kazi zake.
 
Tunachokijua
Julai 24, 2023, Mtumiaji wa Mtandao wa Twitter anayefahamika kwa jina la Think Different aliweka ujumbe unaotaka kupata ufafanuzi wa picha kutoka kwa msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kuhusu magari yenye chapa ya kampuni ya DP World yanayodaiwa kuonekana kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Madai haya yamekuja wakati ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia uwekezaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye bandarini, uwekezaji ambao umekutana na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya watanzania ikiwemo kufunguliwa kesi Mahakamani.

Ukweli wa Picha hii
Picha husika ilianza kuonekana mtandaoni Julai 22, 2023, saa 6:51 mchana, ambapo mtumiaji wa mtandao wa Twitter mwenye jina la Truckers of Tanzania aliichapisha ikiwa na maneno;

"DP World South Africa vyuma ni iPad 440 tu haina kuremba ila pale kwa wala Maharage wataleta zile gari pendwa zile zile za kula chapati 9 ndio uendeshe"

Hadi kufikia Julai 24, 2023, saa 10:15 alasiri, ujumbe huu ulisomwa na watu 2780, ilipendwa mara 51 na watu 5 walishirikisha wengine (retweet) ndani ya mtandao huo.

Kupitia uchunguzi wake, JamiiForums imebaini kuwa picha hii haijachukuliwa maeneo ya Tanzania na haina uhusiano na Bandari ya Dar es Salaam. Hata hivyo, hii ni picha halisi inayoonesha magari yanayomilikiwa na Kampuni ya DP World.

Madai haya yanakanushwa pia na Truckers of Tanzania kwenye ujumbe wa Think Different, ameandika;

"Fanya fact check mzee usikurupuke na vitu vya ajabu. Hii picha nilipost mimi ni Imperial Parking Yard South Africa....wabongo mkoje?"

Hivyo, Magari haya yanamilikiwa na Kampuni ya DP World lakini picha halisi haijachukuliwa kwenye mazingira ya Tanzania.
Kuna mtu alileta thread humu au mlienda kuokota mada huko ili mkanushe
 
"Wajinga ndiyo waliwao" ni wengi sana Tanzania.
 
Back
Top Bottom