DPP amfutia kesi Mkurugenzi wa JATU PLC

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
DPP AMFUTIA KESI ALIYEJIPATIA BILIONI 5 KWA UDANGANYIFU

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) amemfutia kesi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka ya kujipatia Tsh. Bilioni 5.1 kwa njia ya udanganyifu

Ni baada ya kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Aprili 11, 2023

Mkurugenzi huyo alifikishwa Mahakamani Januari,2023 kwa kujipatia zaidi ya Tsh. Bilioni 5.1 kwa njia za udanganyifu

Chanzo: Mwananchi
 
Wananchi kujitwalia sheria mkononi ni kutokana na mfumo mbovu wa kutenda haki.

Watu wanatengeneza mashtaka mabovu ili kesi ziyumbe
 

Asee kwamba waliyo dai wamedhurumiwa (wenye hisa zao) wao ndiyo wamekosea msela hana hatia, daah !!
 
......nini kiko behind hiyo michezo Jatu na Mr Kuku...? Kuna shida mahala .....
 
Aisee uyu jamaa nilimosa nae peter isare gasaya form one hadi form four... Wamuache tu mwanangu
 
huwa naamini, hakuna siku dpp angetoa kesi yeyote, hasa ya aina hiyo, kama hakuna sauti kutoka juu. sidhani kama ni kitu rais, mbona angeshatumbuliwa kitambo.
 
Aisee! Kweli tuna haja ya kupata Katiba Mpya!
Watu wameapa kwa Misahafu na Biblia na bado wanaiba na kupindisha haki
Hiyo katiba inasaidia nini kama watu hawamjali Mungu na hawana maadili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…