DPP amng'ang'ania Ponda

DPP amng'ang'ania Ponda

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP),Dr.Eliezer Mbuki Feleshi amewasilisha Taarifa ya Kusudio la kukata Rufaa dhidi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.

Taarifa ya Kusudio la Kukata Rufaa limewasilishwa na DPP Mahakama Kuu yaTanzania,Kanda ya Dar es Salaam. DPP anapinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomkuta na hatia Sheikh Ponda kwa kosa moja na kumweka kama mwangalizi wa amani kwa mwaka mmoja.

Taarifa hizi zimethibitishwa na DPP mwenyewe. Waungwana wa Tanzania,mnaonaje suala hili? Tupo pamoja na DPP wetu?

Imeripotiwa pia kwenye Daily News la leo tarehe 2/6/2013.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Shehe ponda aionya serikali



KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amewatangazia Waislamu kwamba mihadhara iliyopigwa marufuku na Serikali, itaendelea kufanyika kama kawaida na atakayeendelea kuikataza watakabiliana naye kwa nguvu zote.

Sheikh Ponda aliyasema hayo jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kwenye mamia ya Waislamu waliokusanyika kwa ajili ya kongamano la kujadili mada mbalimbali, ikiwamo uhuru wa Waislamu na haki zao na usalama wa watu, miradi na mali zao.

"Tunatoa tamko kwa Waislamu, mihadhara iliyopigwa marufuku itaendelea kufanyika kama kawaida, Waziri wa Mambo ya Ndani azingatie kauli hiyo, hatuogopi ujinga, tunataka utaratibu ufuatwe, atakayekataza mihadhara kufanyika tutakabiliana naye kwa nguvu zote," alisema Ponda.

Alisema kwamba, Waislamu wamekuwa hawasikilizwi katika mambo mengi wanayoomba kufanyiwa, lakini kwa upande wa maoni waliyotoa katika Katiba Mpya wanategemea kuyaona yakiwamo.

"Endapo maoni ya Waislamu hayataonekana katika Katiba mpya, tutaanzisha mtiti hadi kiama, hatuogopi mtu, hapa tulipofikishwa hatukubali,"alisema Sheikh Ponda.

Alisema kwamba, walipeleka mapendekezo serikalini, kwamba iundwe tume ili waweze kupeleka madai yao, lakini hadi sasa tume hiyo haijaundwa.

"Kwa hiyo, hatutarudi nyuma kudai haki zetu, tutatumia mazungumzo, kuandika na kusema, kufanya mihadhara na makongamano, kufanya maandamano mchana na hatimaye kufanya maandamano usiku na mchana.

"Pia, tunatarajia kufikisha mahakamani kesi nzito tatu kuhusu viongozi, sitazitaja kwa kuwa bado ni mapema mno," alisema.

Naye Sheikh Kondo Bungo, akizungumzia matukio yanayotokea nchini, alisema Serikali inayo majibu ambayo yanatakiwa kuwekwa wazi ili wananchi wayajue.

"Kuna dhana potofu imejengwa ili kuonyesha Waislamu ni hatari, Zanzibar kumetokea mauaji ya Padri Mushi, makachero kibao wamekwenda huko, baada ya siku mbili kanisa likachomwa, kweli kuna mzanzibari gani mwenye kuweza kufanya tukio kama hilo katika mazingira ambayo makachero wamejaa?

"Waislamu hatuna ugomvi na Wakrito, chuki iliyopo ya kidini inapandikizwa na Serikali, kwa hiyo wakiristo waungane na Waislam kuifanya Serikali iseme ukweli juu ya matukio hayo,"alisema Kondo.

Akizungumzia umoja wa Waislamu, Sheikh Nassoro Mohammed, alisema mkutano wao huo unathibitisha Waislamu ni wamoja na hawana ugomvi na Wakrito isipokuwa ugomvi wao upo kwa Serikali.

"Hatuna ugomvi na Wakristo bali ugomvi wetu upo kwa Serikali kwani kuna haki zetu tunalalamikia hatupewi, mtu akidai haki asipigwe badala yake asikilizwe na kueleweshwa, tunashangaa kuona watu wakiijibia Serikali kuhusu madai yetu," alisema Mohammed.

Akizungumzia kufutwa kwa somo la dini kufanyiwa mtihani, Mwenyekiti wa Baraza la Wakuu wa Shule, Hussein Pilly, alisema wanacholalamikia wao siyo kufutwa kwa masomo ya dini bali kufutwa kwa mitihani ya masomo ya dini mwaka huu.

"Hakuna aliyesema Serikali imefuta somo la dini shuleni, somo la dini litaendelea kufundishwa, lakini halitafanyiwa mtihani, hicho ndicho tunacholalamikia kwa sababu wanafunzi watakata tamaa kulisoma,"alisema Pilly.

Kwa mujibu wa Pilly, kitendo cha somo la dini kutofanyiwa mtihani, kitasababisha madhara kwa Waislamu na Serikali kwa sababu somo hilo hadi kufikia hatua ya kukubaliwa kufanyiwa mtihani, mijadala ilifanyika na wadau wakakubaliana ingawa sasa mabadiliko yanafanyika bila wadau kushirikishwa.
 
swala la udini wamelipandikiza hao hao ccm na dpp wao saizi wanashindwa wafanye nn baada ya kuzembea upuuzi kama huu kutokea na wameshindwa kuudhiti.
 
Huyu DPP asituzingue naona kama hajajipanga au anaelekezwa tu la kufanya
 
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP),Dr.Eliezer Mbuki Feleshi amewasilisha Taarifa ya Kusudio la kukata Rufaa dhidi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.

Taarifa ya Kusudio la Kukata Rufaa limewasilishwa na DPP Mahakama Kuu yaTanzania,Kanda ya Dar es Salaam. DPP anapinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomkuta na hatia Sheikh Ponda kwa kosa moja na kumweka kama mwangalizi wa amani kwa mwaka mmoja.

Taarifa hizi zimethibitishwa na DPP mwenyewe. Waungwana wa Tanzania,mnaonaje suala hili? Tupo pamoja na DPP wetu?

Imeripotiwa pia kwenye Daily News la leo tarehe 2/6/2013.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
kwa staili hii huyu DPP kufungua kesi za kutumwa na kuzing"ang'ania tutashindwa kujua nani ana kosa na yupi hana,mchelea haki
 
Kumwachia Ponda sidhani kama ulikuwa ni udhaifu wa sheria bali ni huu mchezo wa kesi kuamriwa kwa hisia badala ya sheria.

Mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe
 
Let's me say ,,,,,,,,,,,, piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiippoooooooooooooooz
 
DPP, angalia sana... usitengeneze wajane na mayatima..... the world is already behind you! Akili za kutumwa changanya na za kwako
 
Hivi huyu anajua parole? Wala dpp asipoteze fedha zetu kuappeal. Atajirudisha mwenyewe ndani. Akili za kupulizia!
 
naamini DPP anafanya hivyo kipropaganda zaid,ili serikali ionekane haijaridhika na hukumu kwa lengo la kuwatuliza watu wa dini ya upande wa pili kwamba serikali ya tz inasisimamia haki.Naifananisha na rufaa ya Zombe ambayo ni huyu DPP aliifungua na mwisho wake ni ..et serikali imeshindwa kesi!

nb:mimi si mwanasheria ,naandika haya kama mtu huru kifikra
 
Kila kitu Kila jambo Kila maamuzi ya nchi hii sasa yana matege na makengeza hakuna kilicho sawa hata kimoja
 
Back
Top Bottom