Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Mhe. Rais SSH naomba nikupongeze kwa ujasiri wa kufanya yale waliyotuaminisha hayawezi kufanywa na viongozi wa chama Cha Mapinduzi. Nikupongeze kwa kusikia kilio Cha wengi kuhusu tuhuma zinamkabili mtumishi wa Umma mmojammoja pamoja na tuhuma za Wana CcM.
Ulimteua Biswalo Mganga kuwa Jaji kwa roho njema kabisa. Umetimiza wajibu wako wakuheshimu taaluma yake na kuona wewe Kama binadamu anafaa kuwa jaji.
Mara tu ulipomteua wananchi walionyesha kutokukubalina na wewe na wakaweka ushahidi adharani kwanini si mtu sahihi kuwa Jaji.
Kilio hiki kimedumu kwa muda mrefu si kwa sababu watu wanamchikia Biswalo kinafiki ni kwa sababu alitekeleza majukumu yake kinyume kabisa na msingi wa ofisi yake. Alijivuna na hakuwaonea huruma wananchi, alijaza mahabusu Magereza na Leo anakupa kazi yakuwatoa badala uendelee na majukumu mengine. Alifanya makusudi na hakutaka kusikiliza Waziri wala katibu wa Wizara. Uzuri waliohudumu chini yake unawafahamu. Alijimilikisha madaraka ya nchi nzima na bila kalamu yake hakuna maamuzi. Huyu mtu hafai kuwa jaji kwa sababu wale aliogombana nao na aliowanyima haki ndio wakata rufaa wa leo na majalada yatakwenda kwake. Atawatendea haki?
Naamini unamjua vizuri na unajua sababu za kwanini aliyatenda haya, ila pamoja na yote si mtu sahihi kwenye nafasi ya mfumo wa kisheria wa nchi, mpangie kazi nyingine atakayoweza kuimudu bila kukutana na wale aliowasulubisha.
Wananchi wamesema adharani, Watanzania wamepingana kwa dhati na uteuzi huu na wewe mikono yako ipo safi. Tengua uteuzi huu kwa kuwasikiliza wananchi waliomwishtaki kwako. Hata Kama unampenda na ana mazuri unayoyajua. Wape Watanzania amani mpe Jaji mkuu amani katika muhimili wake wa kutenda haki.
Naamini mtihani alionao jaji mkuu ni mkubwa sana kwenye kipengele Cha kufanya kazi na Biswalo, majaji na mahakimu wanaumia kwa sababu nao pia aliwapa maelekezo yakuzima dhamana, aliingilia mfumo wote wa haki. Mpangie kazi nyingine, mchagulie bodi moja huko akaiongoze.
Ahsante.