Kesi ambazo sio za msingi ni wakati wa kuzifuta hasa kwa upinzani. Kesi nyingi ni za kuongea au kumpinga Hayati Magufuli kimawazo lakini DPP amegeuza kuwa kesi za uchochezi. Lakini hata kisheria Raisi mwenyewe hayupo tena hivyo futa kesi zisizo za msingi au Rais Mama Samia atakufuta kazi wewe.
Rais huyu mpya ajenda yake ni uchumi sio malumbano au mabambikiziano ya kesi ambazo hazisaidii mtanzania zaidi ya wapambe wachache. Kitendo cha kumchagua Mpango kinaonesha Mama wetu huyu hajachagua kwa sifa za kisiasa bali uchumi wetu kwanza.
Kesi zote za kisiasa ni wakati wa kuzifuta kwa manufaa ya umma.