Waungwana na wajuvi habari zenu:
Naomba kufahamishwa nijue;
Hata kumwachia mtu yoyote na asihojiwe wakati wowote hata kama iwe ni kesi ya Mauaji, Uamsho au Escrow!!!
Naomba kufahamishwa nijue;
- Je; DPP anaweza kufuta/ au kuondoa kesi hata pale baada ya mashahidi wake wote kutoa ushadi na ikathibitika kuna kesi ya kujibu?
- Anaposema hana nia ya kumshitaki mhalifu huwa ni maoni yake mwenyewe au ni sheria?
- DPP anakuwa kaendesha kesi na baadae kufuta au kuiondoa huwa kuna fidia yoyote kwa mtuhumiwa aliyekuwa ameshikiliwa kwa mashitaka?
- DPP anatumia chombo gani kuchunguza hadi anapofikia hatua ya kutokuwa na nia ya kushtaki wakati tayali polisi huwa wameshakusanya vielelezo na kukamta?
- Je; Serikali haioni kwamba ni wakati sasa iweke ukomo wa mda kwa DPP kufuta kesi iliyonguliwa, (mfano, siku 60 baada ya kusomwa kesi, DPP asiruhusiwe kufuta kesi hadi ikamilike, vinginevyo itafsirike jamhuli Imeshindwa?
Hata kumwachia mtu yoyote na asihojiwe wakati wowote hata kama iwe ni kesi ya Mauaji, Uamsho au Escrow!!!