DPP Mwakitalu ondoa uchafu huu ofisini kwako; Ukipuuza usitulaumu

Hawezi kuelewa huyo mpaka yamkute, Mimi Kuna mshkaji wetu baada ya kulipa mamilioni ya plea bargain, kafirisikia mbali, Sasaivi tuponae huku tunalima mpunga
 
Hawezi kuelewa huyo mpaka yamkute, Mimi Kuna mshkaji wetu baada ya kulipa mamilioni ya plea bargain, kafirisikia mbali, Sasaivi tuponae huku tunalima mpunga
Kuna jamaa mmoja alikuwa anaagiza mizigo kutoka China.. Sasa wafanyabiashara wenzake wakawa wanaunga.. Yaani wanachanga hela wanaweka kwenye account moja ili jamaa akiagiza mizigo yake basi na hao wafanyabiashara wengine wanaagiza vitu vidogo vidogo kwa pamoja.
Sasa DPP akamdaka.. Alijitetea kwamba mimi naagiza mizigo yangu lakini pia wafanyabiashara wenzangu pia kuna mizigo kidogo huwa wananituma.. Kwa hiyo wanaweka hela kwenye account yangu. Jamaa akapigwa kesi ya utakatishaji..
Kila miezi 4 DPP anazama gerezani vipi plea bargain.. Jamaa anakataa.. Akamaliza mwaka.. Ikabidi kiunyonge akubali plea bargain ili atoke... Alinyooshwa kama 100 M.. Sasa hivi hana mtaji tena wa kuagiza vitu.. Yaani walimfilisi... Ndio maana wafanyabiashara wengi walikimbilia Kenya. , Zambia. ,Uganda wengine mbali zaidi..
Kulikuwa na umafia wa chinichini wa watu kuchukuliwa fedha.. DPP alitumika vibaya
 
Huyu biswalo atajakufa kifo kibaya naomba na yeye apate majanga ka ya waliyo watesa watu
 
asiee,jamaa kumbe wameumiza watu sana
 
Mbona karibu wote ni wasukuma?
 
I can sniff damage here.
Watu mpaka namba zao za passports zimewekwa hewani, this is serious issue.

Ningekuwa mimi mamlaka ya upanguzi, ningeshaanza uchunguzi dhidi yao na walau ukipatikana ushahidi, nao wanaipitia njia waliyowapitisha wahanga wao.

Ukwasi wao ndo wa kwanza kukaguliwa kama unaendana na uwezo wa mishahara yao
 
Huyo Wankyo ana mbwembwe ,kumbe Ni toto dogo tu,
Kweli hao inabidi wafanyiwe mabadiliko,Dpp mpya aweke watu wake
Ofisi za serikali sio Mali ya mtu binafsi.

Kumshauri DPP mpya aweke watu wake ni ushauri mbaya maana ofisi sio Mali yake na yeye sio mwajiri, Ile ni mali ya watanzania wote.

Pili naona kama mleta mada naye yumo ndani ya hiyo ofisi kwa hizo details za wahusika alizotoa.
 
Huyo Wankyo na wenzie wana ukwasi wa kutisha ndiyo maana pozi kama watu wazima. Biswalo akiwatengenezea pepo kupitia Plea Bargain
Hayo ndio mambo watu walikua wakiaminishwa awamu ile hakuna nepotism na ufisadi...

Yule jamaa aliweza kufanya brainwashing sana ila pia uwingi wa wajinga Tz bado ni mkubwa ndio maana alifanikiwa kuwatumia kama mtaji
 
kwa majungu na fitina watanzania nawavulia kofia!! yaani ukifika ktk maofisi ya umma wanavyo limana!! utadhani wamesomea majungu na fitina. na cha kushangaza zaidi unakuta na kionhozi pia ana endekeza Majungu na fitina.
hebu tuache tabia hii sio nzuri kabisa, hebu fanyeni kazi punguzeni umbeya, umbeya tu. wakati mwengine hadi sisi wananchi tunakosa imani na taasisi zenu kwa sababu ya kusemana na kufitiniana.
Viongozi ktk kila idara za serikali ondoeni tabia hizi sehemu za kazi, hazifai kwani zina punguza ufanisi.
 
At last ile original JF is back...

Kuna binti mmoja kati ya uliowataja hapo nashangaa kumuona hapa wakati alikuwa binti mwenye maadili sana, wazazi wake walikuwa ni watu safi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…