Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
hiki kipindi kinarushwa katika channel inaitwa E-Entertainment. huwa naona jinsi wanawake maarufu wanavyohangaika kufanyia miili yao plastic surgery hadi nakoma. wanapendelea uso matiti na tumbo. wanafanya hivyo kwa ajili ya nani? wanaingia gharama kubwa sana za upasuaji na kumpa changamoto Mungu. Hii inanipa picha kuwa bado wanawake wengi hawajiamini. Nachoshukuru ni kuwa wanaofanya hayo idadi yao kubwa ni wazungu wanaokaribia asilimia 100. Blacks sijawaona ila haimaanishi kuwa hawafanyi. pia simaanishi kuwa wanaume hawafanyi. wanafanya kwa faida ya nani?