TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Dr. A. Meru, Mkurugenzi mkuu wa Export Processing Zone Authority (EPZA), amesema utaratibu unaotumiwa na makampuni kubadilisha majina: mfano Sheraton kuwa MovenPick, Airtel kuwa Zain, Mobitel kuwa Tigo, n.k., hauambatani na ukwepaji wa kulipa kodi. Amesema ukwepaji huo wa kodi haupo kwani mkataba unausisha mradi (project) wala sio jina la kampuni. Pia alisema utaratibu wa kubadilisha majina ni wa kawaida kwa makampuni mengi duniani wala hili halifanyiki Tanzania tu. Aliongeza kuwa EPZA inatoa likizo ya kutolipa kodi (tax holiday) ya miaka kumi. Muda huo ukiisha lazima kampuni ilipe kodi bila kujali ilibadilisha jina ama la.
Dr. Meru aliyasema haya wakati wa Mhadhara wa wazi kwa Umma (Public Lecture) uliondaliwa na Engineers Registration Board (ERB) na kufanyika Luther House (Dar-es-Salaam) jana huku yeye akiwa mzungumzaji mkuu.
Source: ERB
WanaJF mnasemaji kuhusu maelezo haya ya Mkurugenzi mkuu wa EPZA?