Dr. Aliyekuwa Katibu Mkuu Necta asitisha utekelezaji Mtaala Form One 2023

Dr. Aliyekuwa Katibu Mkuu Necta asitisha utekelezaji Mtaala Form One 2023

Annie X6

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2023
Posts
704
Reaction score
1,331
Sijui anaitwa msonde!? Ambaye ni naibu katibu Mkuu Tamisemi Ameelekeza kistopisha ufundishaji wanafunz wa kidato cha kwanza mwaka huu 2023 sababu kubwa ikiwa ni KKK.

Walimu Wakuu wote nchini wanatakiwa kutekeleza order ya mkubwa huyo.

Najiuliza hivi mauzauza haya yatakoma lini.

Badala ya kutetea walimu wapewe haki zao anawachimbia kaburi. Mtoto ameanza nasari, la Kwanza mpaka la Saba hajui kusoma na kuandika, je sasa anapoteza muda wa kaz gani.

SOMA HAPA.

SOMA NA HAPA.
 
Siasa ilipoingia kwenye elimu ikaharibu utendaji katika sekta ya elimu.
Viongozi wa kisiasa wamekuwa wanaingilia kwa kutoa matamko na vitisho kwa walimu:
1."Ole wake asiyefaulisha wanafunzi"
2."Mwalimu ashushwe madaraka kwa vile wanafunzi wamefaulu wachache"
3."waache wanafunzi waliofeli darasa la 4,waendelee na darasa linalofuata mtihani darasa la 7 utamchuja"
4.Viongozi wa kisiasa kulazimisha kutoa taarifa za wingi wa ufaulu badala ya ubora wa elimu inayotolewa.
 
Fundisheni tu, chap inakuwa may na rikizo mnaenda.

Likija pepa linafyeka watoto wote wa wanyonge.
 
Kwamba Wanafunzi Wamefika Sekondari bila kujua kusoma na kuandika na kuhesabu, je wamefikaje huko hadi mtaala usitishwe?
Tatizo la Nchi hii ni Siasa Nyingi.
Mtoto anavukaje kwenda Elimu ya Sekondari Hajui KKK.
Hapo mwenye Kosa moja kwa moja ni Wizara ya Elimu, waliwezaje kuwapitisha watoto ambao hawawezi kusoma na kuandika.?
Hii ni skendo ambayo wizara ya elimu inatakiwa kujibu.
 
Watoto wasiojua kusoma na kuandika ukiwahoji wanasema ukweli walielekezwa.

Fuatilia utaleta jibu hapa.

Kuna vitu vimeoza.
 
Sijui anaitwa msonde!? Ambaye ni naibu katibu Mkuu Tamisemi Ameelekeza kistopisha ufundishaji wanafunz wa kidato cha kwanza mwaka huu 2023 sababu kubwa ikiwa ni KKK.

Walimu Wakuu wote nchini wanatakiwa kutekeleza order ya mkubwa huyo.

Najiuliza hivi mauzauza haya yatakoma lini.

Badala ya kutetea walimu wapewe haki zao anawachimbia kaburi. Mtoto ameanza nasari, la Kwanza mpaka la Saba hajui kusoma na kuandika, je sasa anapoteza muda wa kaz gani.

Hujaeleweka. Hariri halafu ongezea nyama zaidi.
 
Tatizo la Nchi hii ni Siasa Nyingi.
Mtoto anavukaje kwenda Elimu ya Sekondari Hajui KKK.
Hapo mwenye Kosa moja kwa moja ni Wizara ya Elimu, waliwezaje kuwapitisha watoto ambao hawawezi kusoma na kuandika.?
Hii ni skendo ambayo wizara ya elimu inatakiwa kujibu.
Wanachotaka tamisemi kila mwanafunzi wa form1 awe anamudu lugha ya kingereza kwa muda wa wiki 6
 
Back
Top Bottom