Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Habari JF,
Kati ya Julai 11 na 12, 2012 Mwenyekiti wa Baraza la Madaktari la Tanganyika (Medical Council of Tanganyika) Dkt.Donan Mmbando alitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari kuwa "Baraza la Madaktari Tanganyika limepokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba, baadhi ya Madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kati ya tarehe 23 na 29 mwezi Juni 2012. Madaktari hao walipangiwa kutoa huduma kwa wagonjwa katika hospitali za Muhimbili, K.C.M.C, Rufaa Mbeya, Bugando, Amana, Temeke,St. Francis- Ifakara, Mwananyamala, Sekou Toure, Haydom na Dodoma. Kufuatia mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika kwamba, Madaktari waliogoma walikataa kutoa huduma za kitaalamu, ikiwa ni wajibu wao, na kwamba kitendo hicho kilihatarisha maisha ya wagonjwa katika hospitali husika na pia ni kinyume na maadili ya taaluma ya udaktari.
Kufuatia malalamiko hayo, Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la Kufanya Uchunguzi (Preliminary Examination) dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
"Baraza la Madaktari Tanganyika limebaini kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, Madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda (Provisional Registration)."
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika liliridhika kwamba madaktari wote wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo, usajili wao ulisitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012. Madaktari wote waliohusika walitakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya tarehe 17 Julai, 2012.
Tarehe 30 Novemba 2012 Nilikabidhiwa hati/ barua ya mashitaka.
Novemba 30,2012 Nilikabidhiwa nakala ya wito wa Mahojiano ambapo ilipangwa kufanyika siku ya Jumatano 11, Desemba 2012 saa mbili asubuhi katika Ukumbi waliouita "Ministry of Health and Social Welfare Conference Hall" na niliitikia wito huo bila kukosa .Majira ya mchana nilihojiwa na Baraza na wakadai kuwa hawawezi kuendelea na majadiliano kwa kuwa wamepitia nakala za barua zangu na hawakuona nakala ya barua ya utetezi .Jioni tulitakiwa kurudi kwa ajili ya kukabidhiwa maamuzi au hukumu ya Baraza. Niliporudi/tuliporudi jioni Baraza lilinijulisha kuwa nikaandike barua ya utetezi ili waweze kuniita na kuendelea na mahojiano.
Tarehe 12, Desemba 2013 (Siku moja baada ya maagizo ya baraza), niliandika barua ya utetezi na kukabidhi ofisi ya Msajili wa Baraza la Madaktari, ilipokelewa na kugongwa muhuri wa "imepokelewa" na kuahidi kuwa wangenijulisha siku ya mahojiano.
Nikiwa nasubiri kuitwa kwa mahojiano siku ya Alhamisi 27 Desemba 2012 niliona taarifa ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyotolewa na Msemaji wa Wizara Nsachris Mwamwajawa vyombo vya habari juu ya maamuzi ya Baraza la Madaktari Tanganyika. Na hii ni sehemu ya taarifa hiyo;
Baada ya taarifa hiyo ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nilifuatilia ili kujua nipo katika kundi gani la adhabu/maamuzi ya Baraza la Madaktari Tanganyika. Nilipofika katika ofisi ya msajili alidai kuwa mimi ni miongoni kwa wale walioitwa lakini hatukutokea katika mahojiano na hivyo baraza limepanga kutuhoji siku nyingine ambayo itapangwa na tutafahamishwa. Nilihoji kwa Msajili kwa sikuwahi kuwa sikuwahi kupewa taarifa juu ya wito huo wa Baraza lakini alidai kuwa Baraza linapanga kuwaita na kuwahoji wote ambao hawakutokea siku walipoitwa.
Ilipofika Machi 30, 2013 Nilijulishwa na Msajili Adv.P.M.Luena kupitia namba yake ya simu ya mkononi kuwa Mahojiano yatafanyika tarehe 09 Aprili 2013 saa tatu na nusu katika Ukumbi uleule ambapo mahojiano yalifanyika mwanzo.
Katika siku tajwa hapo juu nilifika katika mahojiano pamoja na interns wengine ambao hawakuweza kuhojiwa Desemba 11, 2012 kwa sababu ambazo sizijui.
Katika siku yangu ya mahojiano sikuwa na wakili wala shahidi japo nilielezwa kuwa nina haki ya kuwapo nao. Katika mahojiano hayo nilikiri kuwa nimeshiriki mgomo huo lakini nilipinga kusababisha athari za kiafya kwa wagonjwa ambao waliwekwa chini ya uangalizi wangu. Pamoja na kwamba wajumbe wengi walitaka nikubali kuwa nimesababisha vifo vya wagonjwa kutokana na kushiriki kwangu katika mgomo nilipinga hilo. Mwishoni kabisa niliomba Baraza lizingatie yafuatayo katika kutoa adhabu dhidi yangu;
i. Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika mgomo wa madaktari, kuitwa na kuhojiwa na Baraza, hivyo adhabu izingatie pia sijawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la kimaadili toka nimeanza internship yangu.
ii. Hata katika kituo changu cha kazi sijawahi kulalamiliwa na Mamlaka ya Hospitali, Mkuu wa Idara ama yeyote Yule juu ya utendaji wangu wa kazi.
iii. Shitaka la kushiriki katika mgomo na uhatarishaji wa hali za kiafya za wagonjwa lilikuwa linafanana kwa interns wote, hivyo basi adhabu izingatie hilo pia.
Hukumu:
Baraza liliamua kufikia uamuzi wa kunifutia usajili wangu na kwa maana hiyo basi sina uhalali wa kuendelea ama kuanza mafunzo ya internship ili kupata sifa za usajili na hivyo kuniwezesha kutekeleza majukumu ya kutibu.
Aprili 24,2013, Ofisi ya Msajili ilinipatia nakala yangu ya hukumu yenye Ref No: HEA/150/70/XXV/4 ya tarehe 12 Aprili 2013.
Binafsi nilishangazwa na hukumu hii kwa kuwa ndio hukumu yenye adhabu ya juu/kali kabisa ukilinganisha na interns wote ambao walihojiwa ukizingatia kwamba Kosa au shitaka dhidi yangu lilikuwa sawa/linafanana na interns wengine wote, lakini pia interns wote waliohojiwa walikiri kushiriki katika mgomo na Sijawahi kukutwa na hatia wala kupewa adhabu yeyote na Council ikiwamo onyo,onyo kali au kusimamishwa kwa muda.
Haki ya kukata rufaa: Kwa mujibu wa maelezo ya mdomo ya Msajili wa Baraza mbele ya Kikao cha Baraza alidai kuwa nina haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi haya ndani ya siku tisini.
HATUA NILIYOCHUKUA:
Niliamua kukata rufaa kupitia kwa wakili wangu Prof, Abdalah J Safari katika Mahakama kuu na kupangiwa Jaji Augustine Shangwa. Shauri hili lilianza kusikilizwa juzi ( tar 2 .09.2013) na limeahirishwa tena mpaka tarehe 03 oktoba 2013.

TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAAMUZI YA BARAZA LA MADAKTARI KUHUSU MADAKTARI WALIOGOMA
Kutokana na mgomo wa madaktari uliotokea kati ya tarehe 23 na 29 mwezi juni 2012.Wizara iliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la madaktari Tanganyika ili lifanye uchunguzi kuhusu madaktari hao .Idadi ya madaktari wote waliogoma walikuwa 394, kati yao madaktari 376 walikuwa ni madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo (Interns) kutoka hospitali za Muhimbili, K.C.M.C. Bugando, Mbeya Rufaa, St.Francis – Ifakara, Dodoma, Temeke, Mwananyamala, Amana, Haydom na Sekou Toure. Aidha, Madaktari waajiriwa(Registrar) 18 walishiriki katika mgomo huo kutoka hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Baraza lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo. Adhabu hizo zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo, onyo kali na kusimamishwa udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na miezi sita.Vile vile kuna Madaktari ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki katika mgomo na hivyo walifutiwa mashtaka.
MCHANGANUO WA ADHABU
Wizara inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la Madaktari. Wizara pia imeridhia kuwapa Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa. Hata hivyo fursa hii haitawahusu Madaktari wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
- Waliofutiwa mashitaka madaktari 49
- Waliopewa onyo madaktari 223
- Waliopewa onyo kali madaktari 66
- Kusimamishwa kwa muda madaktari 30
- Mashitaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria madaktari 4
- Mashitaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza madaktari 22
HITIMISHO : Kwa taarifa hii madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii barua kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa usajili na kuruhusiwa kuendelea na mafunzo kwa vitendo. Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ili kupewa barua zao kulingana na Adhabu walizopewa. Barua hizi zitatolewa kuanzia tarehe 2 Januari, 2013.Madaktari wote walio katika mafunzo kwa vitendo wanatakiwa kuanza kazi katika vituo vyao vya awali ifikapo tarehe 14 Januari, 2013.Hakuna muda utakaoongezwa kwa kipindi kilichobakia cha mafunzo kwa vitendo. Kwa wale wote waliopewa adhabu wataanza kutumikia adhabu hizo kuanzia tarehe ya adhabu hiyo ilivyotolewa.