Dr. Harith ghassany aeleza usahihi wa utafiti wa kitabu chake: "kwaheri ukoloni kwaheri uhuru"

Dr. Harith ghassany aeleza usahihi wa utafiti wa kitabu chake: "kwaheri ukoloni kwaheri uhuru"

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
DR. HARITH GHASSANY AELEZA USAHIHI WA UTAFITI WA KITABU CHAKE: "KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU"



Tanbihi ya Tanbihi: Kumbukumbu, Kusahau, na Zanzibar Mpya


Na Harith Ghassany

Madhumuni ya maandishi haya mafupi si kumjibu Mzanzibari mwenzangu na kaka yangu Ahmed Rajab, mwandishi maarufu na mwenye kusifika barani Afrika. Nia yangu ni kuweka sawa baadhi ya dhana zake kwa manufaa ya Zanzibar ndani ya wakati huu tulionao.


Mwandishi maarufu wa riwaya, Milan Kundera, aliandika: "Mapambano ya binaadamu dhidi ya nguvu [za dola] ni mapambano baina ya kumbukumbu na kusahau." Suala kuu la kwa kila Mzanzibari aliyeishi kabla au baada ya miaka 50 iliyopita ni, anakumbuka au anakumbushwa nini, anasahau au anasahaulishwa kitu gani, na kwa nini? Suala hilo ni la kwanza kabisa. Suala la chuki, kulipizana kisasi, au kusameheyana bila ya kusahau, ni masuala ya mtitiriko wa suala kuu.


Kwa hiyo, tunapolizungumzia suala la kumbukumbu na kusahau, la kwanza la kujiuliza na kulizingatia ni, tunakumbuka au kusahau kitu gani? Na hicho kinachokumbukwa ni kipi na jawabu yake inatokana na kundi au makundi yepi kati ya makundi matatu aliyoyataja Rajab:
1. La wahusika
2. La walioshuhudiya
3. La walioyasikiya


Rajab kajiweka kwenye kundi la pili na kuzidi kujiaminisha na aaminike, ameandika kuwa ana ushahidi wa maandishi wenye kuthibitisha yale anayoyakumbuka. Nimefurahi sana kulijuwa hilo kwa sababu tuna mfano mzuri sana wa kufananisha usahihi wa nguvu za historia ya maandishi ya wakati wa tukio na udhaifu wa "historia simulizi" za baadae.


Napenda kumuomba kaka yangu mpenzi atupatie japo kopi ya kumbukumbu za maandishi ya mkutano wake na marehemu Abdalla Kassim Hanga pamoja na Wazanzibari wenzake wawili, ili tupate kipimo cha kuyapima yale ambayo yeye ameyahifadhi kama ni shahidi wa maandishi.


Lakini turudi nyuma kidogo kwenye kumbukumbu na kusahau hata bila ya kujaribu kuyakumbuka au kuyasahau yaliyotokeya katika mkutano wa miaka 47 iliyopita.


Kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru," (na si "Kwaheri Uhuru, Kwaheri Ukoloni," kama alivyoandika Ahmed Rajab kwenye sehemu ya pili ya makala yake ya "Tanbihi"), kina kurasa 496. Kati ya hizo ni kurasa tatu tu, ukurasa 267-270, zenye kuuzungumziya mkutano wa London baina ya Wazanzibari watatu na Hanga. Lakini hizo kurasa tatu ni muhimu katika muktadha wa maudhui ya kukumbuka na kusahau kwa sababu, na Mungu awazidishie afya Ahmed Rajab na Bwana Salum Hamdan ambaye anaishi Maskati, Oman, watu wawili hao wenye kuhusika moja kwa moja na suala la changamoto za kuandika historia, Alhamdulillah, wote wawili wako hai na wana akili zao.


Kwanza napenda kumkumbusha msomaji kuwa Bwana Salum Hamdan ni wa kundi la pili, la waliyoshuhudiya, kama anavyojinasibunalo Ahmed Rajab. Tafauti yao ni Ahmed Rajab ameweka kumbukumbu ya maandishi ambayo narudiya tena, tutamshukuru sana akitupatiya ili tujifunze namna ya kuzizidhibiti changamoto katika suala zima la kuisajili historia na athari zake mbaya na nzuri za baadae.


Mzee Salum Hamdan ni mzee wa hikma na busara. Nilipokwenda kuonana naye kwa mara nyengine ili nizisajili kumbukumbu zake, aliniambia nisubiri mpaka atakapozungumza na Ahmed Rajab kwa sababu kuna mambo ambayo huenda akawa ameyasahau au hayakumbuki vizuri. Na hapo ndipo msomaji wa kurasa 267-270 katika kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru," atakutana na maneno yafuatayo ya Salum Hamdan yenye kuonyesha kuwa alikuwa shahidi wa mkutano ambaye aliamua kuzungumza na Ahmed Rajab kabla ya kuzungumza na mwandishi (Harith):


"Sasa tulivyokuwa London yeye [Ahmed Rajab] kataja watu watatu tu." Ukursa 267.
"Nnavyokumbuka mimi Oscar akatwambia sikilizeni bwana." Ukurasa 268.
"Ndivo navokumbuka mie na ndivo anavokumbuka Ahmed [Rajab]." Ukurasa 268.


"Mimi skumbuki ile nilikwenda railway station. Kile mimi sijakumbuka. Kama ulivosema, mimi nyumba nilikuwa naijuwa, sina haja ya Kasembe kunpeleka. Lakini inaweza kuwa nimekwenda mimi na Kasembe kumpokea Ahmed Rajab. Yeye Ahmed kafikiri tu na mie ni mgeni. Hajajuwa kuwa mimi na Kambona tunajuwana na jirani, na nyumba yangu mie na yake si mbali." Ukurasa 268. "Yeye Ahmed amekumbuka mambo mimi sijayakumbuka." Ukurasa 268.

Mh.OscarKambona19631966_250_310_s_c1.jpg

Oscar Kambona​


Inasikitisha kuwa mwandishi gwiji na mahiri kama Ahmed Rajab angalau kusema kuwa Salum Hamdan alizungumza na yeye kama mwenzake kuyathibitisha yale walioyashuhudia pamoja na Hanga kabla ya kumpa mkusanyaji (Harith) taarifa za mkutano wa London. Ahmed Rajab kashindwa kuwa mkweli na muwazi na badala yake kaamua kujaribu kunirushia ndoo ya tuhuma yenye uchafu wa "msimamo wa kisiasa," "dhana Fulani," "kupotosha historia," "kutoa maelezo kinyume na matukio halisi yalivyotokea," na kumumunya "wanaoendeleza chuki wakikataa kusamehe." Hee!


[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
20150605_181653.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]Lumumba[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Kama tayari nilikuwa nina dhana fulani, kwanini nilizitupilia mbali simulizi za kina marehemu Ali "Lumumba" na wengineo, na kumfuata Mohamed Said Tanga na kuonana na wazee wazito wa Dar es Salaam? Marehemu Mzee Hamza Aziz ambaye alikuwa Kamishna wa Polisi aliniuliza suala dogo lakini zito. Aliniambia, "Sikiliza kijana. Inataka kwanza ujiulize yale Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa huku kwetu Tanganyika au kule kwenu Zanzibar?" Hapo ndipo nilipoipata ile Wazungu wanayoiita "gestalt switch" au "paradigm shift." Haikuwa dhana wala uhodari wangu. Na hiyo ilitokeya baada ya kupoteza kama miaka miwili Zanzibar kuyatafuta Mapinduzi mchana kwa vibatari na kandili ndani ya vichochoro vya Mji Mkongwe na N'gambo yake!


[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]
20150530_055917.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]Dr. Harith Ghassany na Mohamed Said[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Hayo yote bado sijayaona umuhimu wake kwa sababu kuna faida au somo gani katika kukumbuka au kusahau kama Oscar Kambona ndiye au siye aliewaita Wazanzibari kwake au kama alimtuma Kasembe? Muhimu Ahmed Rajab alifika kwa Oscar Kambona na angelitaka angeliamua kutohudhuria mkutano baada ya kutambua kumbe Kasembe hakuwaambia alikuwa amewachukuwa kwenda kwa kitimbakwiri na msaliti wa ukombozi wa Afrika - Oscar Kambona. Haingii akilini hata kidogo kuwa Ahmed Rajab abebwe tu na Kasembe kama pakacha la madoriani halafu ajikute anafunguliwa mlango na Kambona!


Narudia tena. Yote hayo si muhimu kwa sababu suala muhimu kwa kila Mzanzibari ni kukumbuka au kusahau namna Zanzibar ilivyotoweka na kupotea au kupotezwa kama ni nchi yenye mamlaka kamili kupitia tukio la tarehe 12 Januari, 1964, na yaliofuatiliya. Suala si nani alikuwa akitawala, uhalali au uharamu wake. Suala ni kupotezwa nchi kwa kuvamiwa na baada ya muda mfupi kumezwa ndani ya muungano. Ni kama vile kumbaka mwanamke halafu ukaamua kufunga pingu za maisha naye kwa kufanya harusi!


Na ndio maana mazungumzo ya Hanga kwa mujibu wa Salum Hamdan niliyaweka katika mlango wa "Hayeshi Majuto Yao." Bwana Salum Hamdan ambaye yuhai amemnukuu marehemu Hanga:


"…sisi Mungu atusamehe, tumefanya mambo mengi ambayo mabaya, tumedhulumu, tumechukuwa watoto na wake za watu, na Mwenye Enzi Mungu anisamehe na ninajuta kwa haya nlioyafanya." Ukurasa 269.


Kinyume cha Salum Hamdan, Ahmed Rajab kayasahau maneno ya Hanga yaliyonukuliwa na Salum Hamdan lakini ameyakumbuka maneno aliyojisafisha nayo Hanga kwa kumtusi Kambona.


Salum Hamdan ameeleza, "Lakini inasikitisa kuwa tangu wakati ule yeye [Hanga] yupo pale London habari zishafika Cairo. Walioko Cairo maambassador wa pale wameshapeleka habari Tanzania kwa Mzee Nyerere. Ikawa serikali inavosikia wamekaa wakimgojea arejee tu. Yeye Hanga hajajuwa, wala sisi hatujajuwa." Ukurasa 270.


Anaandika Rajab: "Kutoka Conakry, Hanga alirudi nyumbani, akipitia Cairo, ambako alikuwa mgeni rasmi wa Ahmed Diria Hassan, Balozi wa Tanzania nchini Misri. Aliporudi Dar es Salaam ndipo Hanga alipokamatwa kwa amri ya Rais Julius Nyerere na akapelekwa Zanzibar ambako aliuliwa kikatili." Ahmed Rajab hajui au hakumbuki kuwa kumbe Hanga alikuwa ameshauliwa kutoka Cairo.


Kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru," si kitabu kilichosimama juu ya midomo ya simulizi peke yake. Kila mlango wa kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru," una marejeo ambayo yanatokana na "primary" na "secondary" "sources." Kwenye utafiti wa kihistoria, "primary" "sources" ni marajeo ya watu ambao walishiriki na waliyashuhudia yale ambayo wanayazungumzia. "Secondary" "sources" zinaweza zikawa ni vitabu ambayo vinategemea nini watu wengine wameandika na mwandishi mwenyewe si mwenye kuyashuhudia yale yalioandikwa au kusemwa. Simulizi za wazee si zangu mimi bali ni za wazee walioshiriki moja kwa moja au kwa karibu sana na tukio la Zanzibar la 1964. Na ikumbukwe pia, historia ya maandishi inatokana na historia ya simulizi. Yakumbuke ya Jibrili, Wahyi, na kukusanywa kwa Qur'an.


Kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru," kina milango ishirini na moja.


Sasa wacha twende mlango kwa mlango:
1. Kwenye "Mapitiyo kwa Jumla" kuna endnotes (mapitio) 24.
2. Mlango wa Kwanza una mapitio 25.
3. Mlango wa Pili una mapitio 42.
4. Mlango wa Tatu una mapitio 27.
5. Mlango wa Nne una mapitio 6.
6. Mlango wa Tano una mapitio 19.
7. Mlango wa Sita una mapitio 11.
8. Mlango wa Saba una mapitio 15.
9. Mlango wa Nane una mapitio 20.
10. Mlango wa Tisa una mapitio 14.
11. Mlango wa Kumi una mapitio 2.
12. Mlango wa Kumi na Moja una mapitio 16.
13. Mlango wa Kumi na Mbili una mapitio 18.
14. Mlango wa Kumi na Tatu una pitio 1.
15. Mlango wa Kumi na Nne una mapitio 18.
16. Mlango wa Kumi na Tano una mapitio 2.
17. Mlango wa Kumi na Sita una mapitio 6.
18. Mlango wa Kumi na Nane una mapitio 2.
19. Mlango wa Kumi na Tisa una mapitio 84.
20. Mlango wa Ishirini una mapitio 47.
21. Mlango wa Ishiri na Moja una mapitio 3.


Na ukiingia na ukazama ndani ya hayo mapitio ndipo utakapoweza kuunganisha na kuona wapi penye udhaifu wa sahau na wapi ambapo sahau imepikuliwa na maandishi ambayo hata mwenye sahau utamuona anajikuta hajui au hakumbuki kitu. Wakati kweli nguvu za kukumbuka na kusahau zina uwezo wa kutupiga chenga, jee, maandishi ambayo ni "primary sources" ambayo yako karibu sana ki wakati na tukio lenyewe, hayana uzito wowote kwa gwiji wa fani ya habari na uandishi mtamu kama ndugu yetu Ahmed Rajab? Au tuseme hakuwa na wakati na alizisoma zaidi simulizi za wazee na ndio maana akaona udhaifu katika "methodology" ya uandishi wa "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru?" Au alizilenga kurasa tatu tu kati ya kurasa 496?


Kuridhika nako kuna miko yake. Mtu anaweza akakubali lakini asiridhike na jawabu wala ushahidi. La msingi, kama nimekosea au nimedanganywa, kama ni muwongo au nimezuwa; Alhamdulilllah, uhai na uwezo wa wengine kuja na maelezo mbadala na yenye kusimama na hoja zenye ushahidi, bado upo. Suala: kwanini hawakosowi pale wanapoona pametiwa chumvi au pamepotoshwa kwa kulitimiza lengo la mwandishi au la watu fulani? Tumeweke wapi Salum Hamdan? Katika kundi la waliyoshuhudiya au katika kundi walioyasikiya tu na kumkabidhi mwandishi wa makala hii?


Naanza kuamini na kuridhika kuwa kuna tatizo kubwa zaidi hata kuliko kukukmbuka au kusahau. Kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru," kimewashitusha, kimewaporomosha na kuwashusha daraja baadhi ya watu katika majivuno na majigambo waliyokuwa wakijivunia siku zote za Uwao. Kilichowashtuwa zaidi kuwa kimepokewa na kukubalika na hata wale ambao hawakubaliani nacho wameamuwa kukaa kimya.


Kimewashangaza kuona kimefikia kua kigezo cha ushahidi wa kusadikika na kukubalika Bungeni, hiyo ilikuwa fimbo. Walitamani angekuwa kiongozi au viongozi fulani kuipata sifa hiyo. Ahmed Rajab anashaka juu ya nini hali anajuwa kuwa niliyoelezwa yanatokana na mashahidi wa matukio hayo na washiriki wengine bado wahai na hadi leo hakuna aliyeyapinga maelezo yao. Vipi yeye awe na shaka nayo! Yeye na walio kama yeye hawaji na ushahidi au kitu kipya. Ni ushahidi wa kukosoa na kupanga hoja kwa kutumia kipaji cha uandishi na mantiki za kupinduwa hoja.


Katika mapambano baina ya kukumbuka na kusahau, kinachotakikana khasa ni ukombozi wa kiroho kwanza, na wa kiakili baadae, wa kila Mzanzibari, anaeishi ndani au nje ya Zanzibar na vizazi vyao. Ni ukombozi wenye kukubali, tena kwa hoja zenye kusimama juu ya ushahidi juu ya yale ambayo yamekuwa yakiogopwa kuzungumzwa hata kwa siri tena kwa zaidi ya nusu karne. Kinachotakikana ni uongozi mpya wa kizazi kipya ambacho kiko tayari kuinusuru Zanzibar kutokana na maradhi ya ukaidi na kujipambiya sifa ili kujitawadhisha na utawala.


Zanzibar imezungukwa na bahari ya ushahidi wa kuvamiwa kutoka kila upande wa roho na mwili wake lakini bado ina baadhi ya magenerali ambao wameamua kuingia kwenye vita vya kuinusuru huku wakiwa hawana hakika baina ya kuuandama "umimi" au kuyaweka juu kabisa maslahi ya Zanzibar na maslahi ya Wazanzibari ambao wengi wao ni watu wema na wanyonge.


Kizazi kipya hakikubali tena kudanganywa na kuingiliwa na mchwa wa miaka 51 iliopita. Kizazi kipya ni aina ya mbao mpya ambayo mchwa hawezi kuila. Mchwa aliebakiya Zanzibar na nje ya Zanzibar ni yule ambaye ameshaila fimbo ya Nabii Suleiman.


Na hadithi ya Musa ndani ya nyumba ya Firauni haijamalizikia na tukio la kihistoria liliomo ndani ya vitabu vitukufu vya Qur'an na Bibilia. Wakati hauko tena mbali Firauni wa Zanzibar akatoa shahada huku anazama.



Hapo ndipo suala la kukumbuka na kusahau litakapokuwa na maana mpya kwa Zanzibar Mpya na vizazi vyake – Ameen.
 
kumekucha.
AcbjL9g9i.jpg


KadodaII,
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Sheikh Suleiman Takadir akipanda
jukwaani ili kumkaribisha Mwalimu Nyerere alikuwa akisoma dua kisha anasema,
"Kwaaachaaa!"

Wana TANU wanajibu "Kweupeee!"
Ile "Kwacha" maana yake ilikuwa "Kumekucha."

Ujumbe kwa mkoloni ilikuwa Watanganyika wako macho weshaamka.
Sijui kwa nini umeandika neno hilo.
 
KadodaII,
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Sheikh Suleiman Takadir akipanda
jukwaani ili kumkaribisha Mwalimu Nyerere alikuwa akisoma dua kisha anasema,
"Kwaaachaaa!"

Wana TANU wanajibu "Kweupeee!"
Ile "Kwacha" maana yake ilikuwa "Kumekucha."

Ujumbe kwa mkoloni ilikuwa Watanganyika wako macho weshaamka.
Sijui kwa nini umeandika neno hilo.

Asante kwa ilm.
 
Mmmh! wamemchokoza mtafiti wa kimataifa sasa tunamgoja ahmed rajabu atupie mzingo kwenye raia mwema na atuoneshe part ya shajara aliyoitangaza

Mmmmh ila hawa jama sio wakuchezewa kwa uwanja huu.
 
Mtoa post tunangoja kitabu kingene kabla hujafa,- audhubillahi mindhaalika
 
Nilipenda uchambuzi wa Ahmed Rajab. Sishangai Mzee Mohd Said kuleta haya ya Ghassany!! Hao wawili kwa kuumba maneno hakuna mfanowe.

Mwandishi tuwekee uchambuzi pia Ahmed Rajabu uliotokea kwenye RAIA Mwema
 
Nilipenda uchambuzi wa Ahmed Rajab. Sishangai Mzee Mohd Said kuleta haya ya Ghassany!! Hao wawili kwa kuumba maneno hakuna mfanowe.

Mwandishi tuwekee uchambuzi pia Ahmed Rajabu uliotokea kwenye RAIA Mwema

Si uuweke wewe uliyeupenda> upo jukwaa huru hapa.
 
mkutano wangu
na Hanga
Ahmed Rajab Toleo la 408 4 Jun 2015
Ahmed Rajab
ahmed@ahmedrajab.com
More information about text formats
Text format
KUMBUKUMBU na usahaulifu. Kalima hizo mbili
zina umuhimu mkubwa katika fani ya uandishi wa
historia. Katika fani hiyo, “kumbukumbu” na
“usahaulifu” huwa na siasa zake na nguvu za
aina yake.
Uandishi wa historia una miiko na maadili yake.
Ni mwiko kwa wanahistoria pamoja na waandishi
wa mambo ya kihistoria kupotosha historia kwa
kutoa maelezo kinyume na matukio halisi
yalivyotukia. Na huo ni mwiko mkubwa.
Miongoni mwa maadili ya uandishi wa historia ni
kwanza, kuyafatiisha mambo na kuyachunguza
kwa kina; na pili, kutoa maelezo yaliyo sahihi bila
ya upendeleo. Hii si kazi nyepesi hasa kwa wale
wenye misimamo ya kisiasa.
Kwa hakika, hiyo si kazi nyepesi hata kwa wasio
na misimamo ya kisiasa kwa sababu mara
nyingine kutokuwa na msimamo wa kisiasa
kwenyewe ni sawa na kuwa na msimamo wa
kisiasa.
Uandishi wa historia unazidi kutatanisha pale
mwandishi anayeandika kuhusu matukio ya
kihistoria anapowategemea wasimulizi wenye
hakika kwamba ni wao tu wenye ukweli.
Wasimulizi hao hutegemea kumbukumbu zao bila
ya kusaidiwa na ushahidi wa maandishi wenye
kuthibitisha wanayoyakumbuka.
Historia ya wasimulizi hao ndio ile iitwayo
“historia simulizi” yaani historia isiyoandikwa,
inayotegemea simulizi za wahusika wa matukio
au za walioyashuhudia matukio au za
walioyasikia tu matukio. Historia ya aina hiyo ina
changamoto zake; tena ni nyingi na kubwa.
Changamoto za aina hiyo lazima alipambana
nazo Dk. Harith Ghassany alipokuwa akiandika
kitabu chake “Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru,”
chenye kuhusika na Mapinduzi ya Zanzibar ya
Januari 12, 1964.
Katika daraja za nani wa kuwategemea na kwa
kiwango gani cha kuwategemea kati ya makundi
hayo matatu, hao wa mwisho, walioyasikia tu, si
wa kutegemewa sana wala kupewa uzito
mkubwa. Huwezi kuyapa nguvu masimulizi yao
kama ya wale walioshuhudia au ya walioshiriki
hasa katika matukio yanayohusika.
Lakini hata yale makundi mawili ya mwanzo — ya
walioshuhudia na walioshiriki katika matukio —
yana mushkili wao. Mushkili huo unatokana na
“kukumbuka” na “kusahau.”
Kwa kiwango gani wasimulizi hao watataka
kukumbuka na kwa kiwango gani watataka
kusahau? Hapo ndipo zinapoingia siasa za
kukumbuka na kusahau katika masimulizi ya
mambo yaliyokwishatokea.
Kutegemea uamuzi wao, masimulizi yao
yanaweza yakawakanganya watu wenye kutaka
kuujua undani wa kitu, kwa mfano undani wa
matukio yanayohusishwa na mtu au jambo fulani.
Siasa za kukumbuka na kusahau ndizo
zinazowakanganya vijana wa leo wasiweze, kwa
mfano, kuujua ukweli na undani wa mengi
yaliyojiri wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar. Kuna
namna mbili ya kuyaangalia Mapinduzi hayo.
Njia moja, ni kuyaangalia kama tukio au mfululizo
wa matukio. Njia ya pili, ni kuyaangalia kama
mchakato ambao baadaye umekuwa na mfumo
au umbile la aina yake. Kuna utatanishi kuhusu
masimulizi ya aina zote hizo mbili za kuyaangalia
Mapinduzi hayo.
Yameandikwa mengi kuhusu tukio na mchakato
huo na kila upande unashikilia kwamba
masimulizi yake ndiyo yaliyo sahihi.
Hapo ndipo tunapokumbana na tatizo jingine: la
fasiri, fasili, tafsiri na ufafanuzi wa maelezo ya
masimulizi ya kihistoria. Hata watu wakipewa
maelezo sawa ya yaliyotokea bado wanaweza
wakawa na fasiri tofauti za maelezo hayo. Ndio
maana utata wa masimulizi kuhusu Mapinduzi ya
Zanzibar bado unaendelea kutinga.
Msikilizaji au msomaji wa masimulizi ya kihistoria
siku zote huwa anapaswa awe makini na atumie
akili yake kufikia uamuzi baada ya kuyasikia
anayoyasikia au kuyasoma anayoyasoma kuhusu
tukio lolote la kihistoria.
Kukumbuka na kusahau mambo yaliyopita ni
vitendo muhimu katika kusimulia mambo ya
kihistoria, yasio ya hadithi tu. Kwa mwenye
kusimulia matukio ya kisiasa vitendo hivyo huwa
ni vitendo vya kisiasa; yaani huwa ni vitendo
vyenye kuchukua msimamo wa kisiasa.Ama
msimulizi anachagua nini cha kukumbuka au
anachagua nini cha kusahau.
Wasimulizi wa aina hii wanakuwa wanawafaa
sana waandishi wenye msimamo wa kisiasa na
wenye kutaka kuuthibitisha kuwa ndio ulio wa
kweli. Kuna hoja nyingi katika kitabu cha
“Kwaheri Uhuru, Kwaheri Ukoloni” zinazonifanya
nifikirie kwamba tangu mwanzo mwandishi
alikuwa na dhana fulani aliyokwishaijenga na
halafu akatumia nguvu zake zote kutafuta boriti,
saruji na mawe kuiimarisha.
Hamna shaka yoyote kwamba alifanya jitihada
kubwa ya kuwatafuta watu wataokikata kiu chake
cha kujua nini kilichosababisha Mapinduzi na nini
hasa kilichotokea.
Bahati mbaya baadhi ya wasimulizi wake
walikumbwa na lile tatizo la “kusahau” na
kumueleza mwandishi kile ambacho wakihisi
mwandishi akitamani aelezwe.
Wakati mwingine huwa ni ajali tu kwamba
msimulizi husahau katika masimulizi yake ya
tukio au jambo fulani kwani ubongo wa
mwanadamu hauwezi kuyakumbuka yote
yaliyopita. Ndio maana kuna watu ambao
wamejizoesha kuwa na shajara yaani kitabu cha
kumbukumbu za kila siku za mambo yao ya
kawaida.
Wengine huandika kumbukumbu za mambo
makuu tu yanayowakuta maishani mwao.Hufanya
hivyo kwa sababu wanatambua ya kwamba kuna
uwezekano wa kukumbuka vibaya baadaye.
Binafsi nimo katika kundi hili la pili.
Nina kawaida ya kuandika kumbukumbu zangu za
mambo makuu niliyoyashuhudia au niliyoshiriki.
Miongoni mwa kumbukumbu zangu ni maelezo
marefu ya siku niliyokutana London na Abdallah
Kassim Hanga, aliyewahi kuwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Waziri
katika serikali ya Muungano. Wakati huo alikuwa
ametolewa kwenye Baraza la Mawaziri.
Katika sehemu ya pili ya makala yake kuhusu
Hanga iliyochapishwa katika toleo lililopita la Raia
Mwema, Mohamed Said amenukuu kutoka kitabu
cha “Kwaheri Uhuru, Kwaheri Ukoloni” kuhusu huo
mkutano wangu na Hanga nikiwa pamoja na
mwenzangu Salim Hamdan, ambaye kwa sasa
anaishi Maskati, Oman.
Kiini cha yaliyomo katika nukuu hiyo, yaani wasia
aliotupa Hanga,ni sahihi lakini kuna machache
yanayohitaji kusahihishwa.
Mkutano huo nilikwishaueleza, ingawa kwa
muhtasari, katika Raia Mwema, toleo namba 168
(ZANZIBAR: Siasa za chuki na wasia alionipa
Abdallah Kassim Hanga…)
Nachukua fursa hii kuyasahihisha hayo machache
yaliyomo kwenye nukuu iliyochapishwa wiki
iliyopita.
Oscar Kambona siye aliyetwita kwake.Kusema
kweli ingelikuwa nimeambiwa kwamba Kambona
alitaka nende nyumbani kwake, pengine
ningegoma. Nisingalikwenda.
Siku hizo Kambona akinuka miongoni mwetu
tuliokuwa tunafuata siasa za “kimaendeleo” kwa
sababu ya ushirikiano wake na wakoloni wa
Kireno waliokuwa wakiwagandamiza wananchi wa
Angola, Guinea-Bissau na Cape Verde pamoja na
Msumbiji.
Mahusiano yetu yalibadilika baadaye kuanzia
miaka ya kati ya 1980 alipokuwa mara kwa mara
akija ofisini kwenye gazeti la “Africa Analysis”
nililokuwa nikilihariri.
Tulikwenda kwa Kambona baada ya mtangazaji
mwenzangu wa BBC, Emmanuel Vivian Kassembe,
kunambia kwamba Hanga akitaka kuniona mimi
pamoja na Wazanzibari wengine wawili, Salim
Hamdan na Abdul Latif Mohammed Nura
(maarufu kwa jina la Khamis Nura.)
Nura alikuwa ni mtu wa karibu sana na Hanga na
alikwenda kusomea sheria Moscow, Urusi, kwa
msaada wa Hanga. Niliwajulisha wenzangu hao
na tukawa tunajitayarisha kwa Jumamosi kwenda
kuonana na Hanga, aliyepita njia kutoka Tanzania
akielekea Guinea. (Siku zile ilikuwa kawaida
kusafiri kutoka Afrika Mashariki kwenda Afrika
Magharibi kwa kupitia ama Paris au London.)
Kabla ya hapo sikujua kwamba Hanga alikuwa
London na nilipomuuliza yuko wapi, Kassembe
alikataa kunambia. Alitutaka tufike kwenye kituo
cha treni ya chini ya ardhi kwenye mtaa wa
Belsize Park saa tisa za jioni siku ya Jumamosi.
Sikujua kwamba Kambona akiishi mtaa huo.
Mimi na Salim tulifuatana kwenda kwenye miadi
yetu pamoja kwa sababu tukikaa nyumba moja.
Nura hakutokea kama tulivyoagana. Tulimsubiri
kwa robo saa halafu tukamfuata Kassembe
kwenda alikokuwako Hanga.
Baada ya Kassembe kugonga kengele ya mlango
na mlango kufunguliwa ndipo nilipotambua
kwamba kulikuwa kwa Kambona kwani ni yeye
aliyetufungulia mlango. Kambona mwenyewe
alituvua makoti yetu ya baridi na kuyatundika
huku tukilahikiana na akanyosha mkono akisema:
“Maalim yuko huko.”
Papo hapo akachomoza Hanga kutoka chumbani;
kilikuwa chumba cha pili mkono wa kulia baada
ya sebule.Humo sebuleni alikuwamo mtu
mwengine ambaye sikumuona na ambaye hadi leo
sijui alikuwa nani.
Kambona hakuwa na muda wa kutueleza
yaliyoandikwa kwenye nukuu ya wiki iliyopita
kwamba alitueleza. Kwa hakika, hatukuijua azma
ya Hanga ya kurudi nyumbani mpaka mwisho wa
mazungumzo yetu nilipomuuliza anapanga
kufanya nini.
Alinijibu hivi: “Unajua mimi nimeoa Guinea na
mke wangu amejifungua. Nakwenda kumpa jina
mwanangu na halafu nitarudi nyumbani”.
Kusikia hayo nilishtuka kwa sababu Zanzibar ya
siku hizo ilikuwa ikitisha.
Hanga akamgeukia Salim na kumwambia:
“Mtizame kijana huyu. Niogope nini? Mimi
sikufanya kitu. Si kuua, si kuiba”. Halafu
akaashiria kwa jicho chumba cha pili
walikokuwako kina Kambona na akatwambia:
“Angalau huyo ameiba pesa za TANU (Tanganyika
African National Union, chama kilichokuwa
kikitawala Tanzania-Bara.)
Sijui kama Hanga alitwambia hayo kwa dhihaka
au kama alisema kweli lakini tulicheka,
tukayaacha.
Kabla ya hayo, mwanzo kabisa wa mazungumzo
yetu, Hanga alisema: “Nataka kukuambieni, mimi
sina ubaya na Mzee”.
Huyo Mzee aliyekuwa akimtaja alikuwa Sheikh
Abeid Amani Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu
wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Tanzania. Halafu akatupa maelezo marefu ya kwa
nini Karume alimkalia vibaya kama yalivyoelezwa
katika kitabu cha Ghassany.
Miaka kadhaa baadaye niligundua kwamba
kulikuwa jengine lililomponza Hanga kwa Karume.
Nalo lilihusika na usuhuba wake Hanga na Saleh
Saadallah, aliyekuwa waziri wa Karume na
ambaye baadaye alifungwa gerezani na kuuawa.
Maelezo ya kadhia ya Saadallah ni ya siku
nyingine, si leo.
Ni kweli Hanga alitwambia kwamba alitaka
kuzungumza nasi kwa sababu, alisema, tutakuwa
“viongozi wa kesho” na akatuasa tusiwe na
ukabila.
Hanga alitueleza kwamba yeye aliwahi kuwa na
chuki za kikabila lakini baadaye aliuona ubaya
wake. Alipopelekwa Bara kuwa waziri baada ya
kuundwa Muungano, alifanya mpango wa
kuwapatia ajira Dar es Salaam waalimu
waliokuwa wamefukuzwa kazi Zanzibar.
Takriban wote walikuwa na asili ya Kiarabu.
Miongoni mwa aliowataja walikuwa Maalim
Shaaban Saleh Farsy, Maalim Salim Sanura na
Maalim Amour Ali Ameir.
Hanga akatueleza kwa masikitiko kwamba
wapinduzi wenzake wa Afro-Shirazi Party (ASP)
huko Zanzibar wakaanza kumsema kwamba
akipendelea Waarabu.
“Lakini mimi nilipowaleta Dar sikuwaona kama ni
Waarabu, niliwaona kama Wazanzibari,” Hanga
alitueleza.
Nakumbuka pia kwamba Hanga alinukuu Qur’an
hasa kisa cha Nabii Musa jinsi Mungu
alivyomnusuru na wafuasi wake na
akamgharikisha Fir’auni na kaumu yake.
Kweli nilimuuliza kuhusu Abdulrahman Babu na
alinijibu kwa kusema: “Babu na mimi sote ni
Marxists (wafuasi wa Karl Marx) na namtakia
kheri. Lakini yeye si tishio kwa Karume kama
mimi. Mimi ndio tishio”.
Miaka kadhaa baadaye Kambona alinieleza jinsi
Kwame Nkrumah, aliyekuwa uhamishoni Conakry,
Guinea, alivyomsihi na kumbembeleza Hanga
asirudi nyumbani.
Lakini hakumsikiliza. Yeye mwenyewe Kambona
pia alinambia kwamba alimshikilia asirudi lakini
hakumsikiliza pia.
Kutoka Conakry, Hanga alirudi nyumbani, akipitia
Cairo, ambako alikuwa mgeni wa Ahmed Diria
Hassan, Balozi wa Tanzania nchini Misri.
Aliporudi Dar es Salaam ndipo Hanga
alipokamatwa kwa amri ya Rais Julius Nyerere na
akapelekwa Zanzibar ambako aliuliwa kikatilI
 
Back
Top Bottom