Elections 2010 Dr. Kigoda apata mpinzani Handeni, Barua ya Chadema kushinda rufaa yafichwa..

MasterMind

Senior Member
Joined
Aug 26, 2010
Posts
102
Reaction score
0
katika zile harakati za kuhakikisha kigoda anashinda, msimamizi wa uchaguzi jimbo la muheza amebania barua ya kutupiliwa mbali pingamizi alilowekewa bw.saidi salehe mweto na mgombea wa ccm abdallah kigoda.

Hayo yalijulikana jana baada viongozi wa chadema mkoa wa tanga kufuatilia kwa tume ya uchaguzi taifa wakajibiwa kuwa uamuzi wa umeshatolewa tangu 25/8/2010 na kwamba waende handeni kufuatilia barua .

Chakushangaza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi handeni akapiga mkwara kuwa maamuzi hayajafanyika!

Baada ya kuambiwa kuwa taarifa zimetolewa makao makuu ghafla barua ikaonekana na ilitolewa tangu tarehe 25/8
 
Huyo msimamizi alitakiwa kupigwa viboko kwanza, harafu afukuzwe hayo maeneo kama adhabu. Hapo Takukuru wanasemaje?
 
Ni hapo.....
Takukuru watajifanya hawana taarifa.....
 
Hii inatoa picha gani! Kama chama twawala wanajiamini kwa nini wanafanya vituko hivi?
 
Duh, kwa mwendo huu tutafika? Kwanini CCM isibadili katiba kuwe na chama kimoja tuu kama hawataki wapinzani wagombee
 
Nchi hii sijui tunaenda wapi, kama unapenda siasa iliyo na democrasia, kwanini huogope kuwa na mpinzani?
hapa inaonyesha kiasi siasa iliyopo si komavu.
 
Wamezoea ujanja ujanja, mwaka huu jasho litawatoka.
 
takukuru walishamaliza kazi kwenye primaries... sasa wanakula shushu
 
katika zile harakati za kuhakikisha kigoda anashinda, msimamizi wa uchaguzi jimbo la muheza amebania barua ya kutupiliwa mbali pingamizi alilowekewa bw.saidi salehe mweto na mgombea wa ccm abdallah kigoda.

Hayo yalijulikana jana baada viongozi wa chadema mkoa wa tanga kufuatilia kwa tume ya uchaguzi taifa wakajibiwa kuwa uamuzi wa umeshatolewa tangu 25/8/2010 na kwamba waende handeni kufuatilia barua .

Chakushangaza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi handeni akapiga mkwara kuwa maamuzi hayajafanyika!

Baada ya kuambiwa kuwa taarifa zimetolewa makao makuu ghafla barua ikaonekana na ilitolewa tangu tarehe 25/8
Mwaka huu ni mwaka wa ukombozi lazima ang'oke KIgoda wanadhani dhuluma itakuwepo milele kila jambo na wakati wake wale wote walioweka mapingamizi tafadhali fuatilieni rufani zenu na aliyeficha barua apelekwa mahakamani kwa sababu anataka kupindisha demokrasia
 
katika zile harakati za kuhakikisha kigoda anashinda, msimamizi wa uchaguzi jimbo la muheza amebania barua ya kutupiliwa mbali pingamizi alilowekewa bw.saidi salehe mweto na mgombea wa ccm abdallah kigoda.

Hayo yalijulikana jana baada viongozi wa chadema mkoa wa tanga kufuatilia kwa tume ya uchaguzi taifa wakajibiwa kuwa uamuzi wa umeshatolewa tangu 25/8/2010 na kwamba waende handeni kufuatilia barua .

Chakushangaza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi handeni akapiga mkwara kuwa maamuzi hayajafanyika!

Baada ya kuambiwa kuwa taarifa zimetolewa makao makuu ghafla barua ikaonekana na ilitolewa tangu tarehe 25/8

SItaki kuamini kuwa hilo linaweza kufanyika nchini mwetu; ni UFISADI kati sura yake halisi na kama ni kweli Wana Handeni wasubiri kurudiwa kwa uchaguzi kama Kigoda akishinda, ni wazi kuwa hakuna sababu ya Mahakama kutoufuta uchaguzi huo maana haukidhi kigezo chochote cha Uchaguzi huru. Huyo Msimamizi wa Uchaguzi ameitia NEC aibu kubwa sana na anastahili kufukuzwa kazi mara moja.
 
Huyo msimamizi alitakiwa kupigwa viboko kwanza, harafu afukuzwe hayo maeneo kama adhabu. Hapo Takukuru wanasemaje?
ha ha ha unanikumbusha yule mkuu wa wilaya moja kule Bukoba aliyewalamba walimu viboko :becky: angetufaa kwenye zoezi hili - tuna wasimalizi wengi tu wanatakiwa kuchapwa Viboko, hata tendwa naye nafikiri angepata vitano au sita hivi ili akome kuitetea ccm.
 
Tendwa inabidi apate Bakora Sita.

Tatu siku anaingia jela na tatu siku anatoka akamuonyeshe Mkewe (Maneno ya JKN).

Baada ya hapo, anafuata Sitta Mwinyi, Anna Mkapa na kumalizia na Bi Mkubwa....

View attachment 13748

Aisee kumbe wapo wengi tu wa kuchalazwa viboko. :becky:
 
Ningekuwa mgombea wa CHADEMA, ninge-file huyo msimamizi wa uchaguzi akaondolewa. Huwezi kuwa na imani na mtu ambaye anaficha barua tu, sasa matokeo ya kura katika uchaguzi itakuwaje?
 
attachment.php

Hii imenichekesha sana
 
Back
Top Bottom