Matokeo ya uchaguzi wa CHADEMA unaashiria “novus ordo seclorum” kwa chama ama ni “finis temporum”? Shemeji yangu mmoja bwana Mosha anasema ni ‘Mwanzo wa nyakati Mpya’ za siasa nchini. Yeye ni mshabiki wa Lissu. So he is very hopeful juu ya kukua kwa siasa za upinzania. Mimi kila nikitazama naona ni ‘mwisho wa nyakati’ kwa Mhe. Mbowe na upinzania wa CHADEMA. Pengine I am too conservative! Yote kwa yote, time will tell.
Tunahitaji kuona kitakachotokea hizi siku 30 za kwanza za uongozi wa kaka yangu Mhe. Lissu ili kupata jibu sahihi la predictions zetu wachambuzi. Tujue kama ataunganisha chama (maana kura 31 ni margin ndogo sana) ama atalipa kisasi.
Tujue ataendelea na maridhiano ama ataasi kila kitu cha Mbowe. Kama Mbowe naye atakuwa na moyo wa kusamehe na kumsaidia Lissu kazi ama ataamua kutoka jumla na kuwasusia chama.
Time will tell. Uchaguzi umeacha majeraha makubwa sana. Mbowe ana watu wengi na wameumia. Wakiwazodoa na kuwang’ong’a ama wakiwatenga watabaki na option ya kuachana na CHADEMA ama kuacha siasa kabisa. Kiufupi, kufanikiwa kwa Lissu ni kama atamuomba radhi Mbowe na kumshirikisha kwenye uongozi, na kama Mbowe atakuwa radhi kushirikishwa.
Lissu anamhitaji Mbowe kuliko Mbowe anavyomhitaji Lissu. Je, Lissu analiona hili?