Dr. Kikwete, Dr. Kigwangala, Dr. Bana, Dr. Tulimumu: Hakuna namana ya kutofautisha udaktari?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Dr. Joyce Ndalichako, Dr. Hussein Mwinyi, Dr. Mohamed Shein, Dr. Michael Kadeghe, Dr. Philemon Sarungi(Prof), Dr. Mgona sipakune Tulimumu, Dr. Maji marefu("Prof"), Dr. Hamis Kigwangala nk.

Hawa wote hapo juu wanaitwa na wengine kujiita madaktari. Hapo kuna madaktari walioteseka madarasani kusomea utabibu wa binadamu na wanyama, kuna waliobobea katika fani mbali mbali za kitaaluma lakini sio kutibu, kuna waliopewa udaktari wa heshima kutokana na utendaji wao au misimamo yao lakini hawajakanyaga darasani kuteseka na kitabu na kuna wanaojitwika udaktari.

Hoja yangu ni kuwa hivi hakuna namna ya kuwatofautisha madaktari hao wakati wa kuwataja ili mtu ajue anayetajwa ni daktari wa aina gani. Hivi mtu akiwataja Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Dr. Hamis Kigwangala na Dr. Joyce Ndalichako mtu wa kawaida asiyejua historia zao kikazi au kielimu atawatofautishaje? Kuna rafiki yangu mmoja ni Dr. anayefundisha chuo kikuu alipokuja kunitembelea, na jirani yangu nilipomtambulisha kwake kama Dr. akawa anataka msaada wa ugonjwa wake unaomsumbua muda mrefu. Je hakuna namna ya kuiandika au kuitamka hii Dr. ikiwa na kitu cha kuonesha kuwa huyu kapewa, kasomea au kajipachika?? Tusaidiane maana nchi hii ina madaktari wachache na wengi feki lakini wajibebea heshima wasizostahili. Kuna vyuo vikuu pia vinapoona havivumi au ni vya kiwango cha chini huwa vinakuwa sharp kutoa udaktari wa heshima hasa kwa viongozi wakubwa ili vitambulike.

Kuna vyeo kama Mwalimu, padri, mchungani, ustaadhi, dereva, urubani, mhandisi nk mara nyingi huwa vinaelekezwa kwa watu wenye taaluma husika. Mfano mtu hawezi akaitwa dereva au rubani kwa heshima wakati hana taaluma hizo. Hivyo watu hao wakitajwa huwa hakuna tatizo kwani wanajulikana ni wataalamu wa fani hiyo. Kwenye udaktari naona kuna nipa shida! Utawatambuaje?
 
Mkuu kuwa bayana na uoneshe njia ambayo pengine ungeona inafaa nasi tuweze kuwa wazi zaid.
 
Dr. Tulimumu concern yako ni nzuri sana. Ila haya ni mapokeo tuliyoyakuta hata sijui tutatofautishaje. Labda ukisha jua /ambiwa fulani ni Dr., swali la pili liwe Dr wa nini?
 
Last edited by a moderator:
Huyo nchimbi alienda urusi kuxma engl coz alivyorud afta miez 6 n dr teh teh teh teh
 
Dr Slaa je, au hili lipo sawa?

Huu ni mfumo wa kidunia mkuu
 
Tamaa za kujipachika kwenye makundi ya wateule (doctors)..
 
Dr.Karugira ,medical,Dr.Rwezaula medical,Dr,Dr.Kaigi....medical,phd....,Dr.Kikwete...zawadi..nk
 
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Dr. Joyce Ndalichako, Dr. Hussein Mwinyi, Dr. Mohamed Shein, Dr. Michael Kadeghe, Dr. Philemon Sarungi(Prof), Dr. Mgona sipakune Tulimumu, Dr. Maji marefu("Prof"), Dr. Hamis Kigwangala nk.

Hawa wote hapo juu wanaitwa na wengine kujiita madaktari. Hapo kuna madaktari walioteseka madarasani kusomea utabibu wa binadamu na wanyama, kuna waliobobea katika fani mbali mbali za kitaaluma lakini sio kutibu, kuna waliopewa udaktari wa heshima kutokana na utendaji wao au misimamo yao lakini hawajakanyaga darasani kuteseka na kitabu na kuna wanaojitwika udaktari.

Hoja yangu ni kuwa hivi hakuna namna ya kuwatofautisha madaktari hao wakati wa kuwataja ili mtu ajue anayetajwa ni daktari wa aina gani. Hivi mtu akiwataja Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Dr. Hamis Kigwangala na Dr. Joyce Ndalichako mtu wa kawaida asiyejua historia zao kikazi au kielimu atawatofautishaje? Kuna rafiki yangu mmoja ni Dr. anayefundisha chuo kikuu alipokuja kunitembelea, na jirani yangu nilipomtambulisha kwake kama Dr. akawa anataka msaada wa ugonjwa wake unaomsumbua muda mrefu. Je hakuna namna ya kuiandika au kuitamka hii Dr. ikiwa na kitu cha kuonesha kuwa huyu kapewa, kasomea au kajipachika?? Tusaidiane maana nchi hii ina madaktari wachache na wengi feki lakini wajibebea heshima wasizostahili. Kuna vyuo vikuu pia vinapoona havivumi au ni vya kiwango cha chini huwa vinakuwa sharp kutoa udaktari wa heshima hasa kwa viongozi wakubwa ili vitambulike.

Kuna vyeo kama Mwalimu, padri, mchungani, ustaadhi, dereva, urubani, mhandisi nk mara nyingi huwa vinaelekezwa kwa watu wenye taaluma husika. Mfano mtu hawezi akaitwa dereva au rubani kwa heshima wakati hana taaluma hizo. Hivyo watu hao wakitajwa huwa hakuna tatizo kwani wanajulikana ni wataalamu wa fani hiyo. Kwenye udaktari naona kuna nipa shida! Utawatambuaje?

Mbona umemsahau Dr Ramazan Mtoro Ongala?
 
Hata ukiambiwa ni Dr wa binadam; bado kuna maswali ya kujiuliza kabla ya kuomba consultation. Je ni Gyn, Psy etc? Hivyo uvivu wetu wa kujua tuuondoe kwanza.
Mimi napenda (na ndivyo ilivyo) mtu ajiite M.D na sio Dr.
Inaonekana ungependa MD waitwe Dr na sio wana-filosofia! Lakini ujue filosofia nayo ni gangwe kama ilivyo MD.
Ukimaliza kuwaondolea Dr wanasiasa ili ubaki na MD; utakuta kuna doctor of dentistry, doctor of Pharmacy, etc

tragedy of the commons
 
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Dr. Joyce Ndalichako, Dr. Hussein Mwinyi, Dr. Mohamed Shein, Dr. Michael Kadeghe, Dr. Philemon Sarungi(Prof), Dr. Mgona sipakune Tulimumu, Dr. Maji marefu("Prof"), Dr. Hamis Kigwangala nk.

nyingi za kuhongan
Hawa wote hapo juu wanaitwa na wengine kujiita madaktari. Hapo kuna madaktari walioteseka madarasani kusomea utabibu wa binadamu na wanyama, kuna waliobobea katika fani mbali mbali za kitaaluma lakini sio kutibu, kuna waliopewa udaktari wa heshima kutokana na utendaji wao au misimamo yao lakini hawajakanyaga darasani kuteseka na kitabu na kuna wanaojitwika udaktari.

Hoja yangu ni kuwa hivi hakuna namna ya kuwatofautisha madaktari hao wakati wa kuwataja ili mtu ajue anayetajwa ni daktari wa aina gani. Hivi mtu akiwataja Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Dr. Hamis Kigwangala na Dr. Joyce Ndalichako mtu wa kawaida asiyejua historia zao kikazi au kielimu atawatofautishaje? Kuna rafiki yangu mmoja ni Dr. anayefundisha chuo kikuu alipokuja kunitembelea, na jirani yangu nilipomtambulisha kwake kama Dr. akawa anataka msaada wa ugonjwa wake unaomsumbua muda mrefu. Je hakuna namna ya kuiandika au kuitamka hii Dr. ikiwa na kitu cha kuonesha kuwa huyu kapewa, kasomea au kajipachika?? Tusaidiane maana nchi hii ina madaktari wachache na wengi feki lakini wajibebea heshima wasizostahili. Kuna vyuo vikuu pia vinapoona havivumi au ni vya kiwango cha chini huwa vinakuwa sharp kutoa udaktari wa heshima hasa kwa viongozi wakubwa ili vitambulike.

Kuna vyeo kama Mwalimu, padri, mchungani, ustaadhi, dereva, urubani, mhandisi nk mara nyingi huwa vinaelekezwa kwa watu wenye taaluma husika. Mfano mtu hawezi akaitwa dereva au rubani kwa heshima wakati hana taaluma hizo. Hivyo watu hao wakitajwa huwa hakuna tatizo kwani wanajulikana ni wataalamu wa fani hiyo. Kwenye udaktari naona kuna nipa shida! Utawatambuaje?

nyingine za kununua na kuhongana au nyingi za huku za kupeana na wala sio za kusomea
 
Mimi nashauri hawa wengine kwa vile wanang'ang'ania kuitwa hivyo basi tuwaite 'dr' yenye kuanza na herufi ndogo na akina Sarungi tutumie 'Dr' yenye herufi kubwa. Ni mawazo tu
 
Back
Top Bottom