OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Mnunuzi wa nyumba za Lugumi zilizopigwa mnada na Kampuni ya Yono Auction Mart kufidia deni la TRA, Dr.Luis Shika amekanusha vikali madai ya polisi kwamba alikusudia kufanya utapeli kwenye mnada wa uuzwaji wa nyumba hizo.
Dr.Shika ameshangaa polisi kumlisha maneno kwamba alitamka milioni 700, 800 na 900, wakati ukweli alitamka 900 lakini sio milioni. "Ni kweli nilipanga kununua nyumba zote tatu, na kwenye mnada nilitamka fedha 700, 800 na mwisho 900. Hakuna popote niliposema milioni 800 au milioni 900" Amesema Dr.Luis Shika aliyejipatia umaarufu siku za karibuni kutokana na sakati hilo.