Dr LWAITAMA asisitiza muundo wa serikali 3...!

Mhe. AJAYE

Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
32
Reaction score
6
Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, ni katika maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika mkoa wa dodoma yamefanyika kwny ukumbi wa Mwl NYERERE(chuo cha mipango), Dr LWAITAMA amesisitiza muundo wa serikali 3 wakati akijibu swali kutoka kwa mwanafunzi wa UDOM aliyetaka kujua "ufafanuzi juu ya serikali 3 na madhara yatakayotokea endapo bunge litakubali au kukataa muundo huo uliopendekezwa na TUME ya jiji WARIOBA, amekunusha usemi wa wanaodai serikali tatu ni gharama na akatoa mfano: sasa tuko kwny serikali 2 lkn tuna mawaziri zaid ya 30 na ukjumlisha na naibu mawaziri ni takribani mawaziri 56 na wabunge 357, wakati tukiwa na serikali 3 mawaziri hawatazidi 15 na wabunge 75 tu, sasa ebu linganisha gharama ya kulipa wabunge 357 na mawaziri 56(serikali 2) vs gharama ya kulipa wabunge 75 na waziri 15(serikali 3), hayo ni maneno ya Dr lwaitama, amezungumza mengi kama, migogoro ya muungano, kufichwa kwa TANGANYIKA, lakini kwa ujumla amesema serikali 2 ng'o twende serikali 3..!
 
wangu 75 tu? ....hahahaha sugu, ngamia, maji marefu, lusinde kamwe hawata kubali serekali tu kama mi kweli wabunge watakuwa 75 tu.
 
miongoni mwa wasomi wa kweli tz na ni wachache sana tanzania inajivunia mtu huyu.
 
.

..Serikali tatu ndio mapendekezo ya waTanzania wengi na sio vinginevyo ...........
 
wangu 75 tu? ....hahahaha sugu, ngamia, maji marefu, lusinde kamwe hawata kubali serekali tu kama mi kweli wabunge watakuwa 75 tu.

Hao wataingia kwenye baraza la wawakikishi (bunge) la Tanganyika
 
Haikuwa mdahalo bali ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kauri mbio yake ni KATIBA MPYA "CHOCHEA MABADILIKO LETA USAWA WA KIJINSIA" kutokana na kauri mbiu ile watu walipewa nafasi kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa baadhi mambo muhimu yaliyomo kwny RASIMU ya PILI.
 
Ni sauti iliayo nyikani!
 
ni kweli serikali 3 ndio mpango mzima, hasa hasa hasa Tanganyika kwa nini CCM hawaipendi???? DR.Lwaitama ndio matunda ya Tanganyika, wale wote wanaoshabikia serikali mbili ni uzao wa Tanzania
 
Namuunga mkono bila serikali 3 tutakuwa na mgogoro mkubwa sana.
 
Dr.Lwaitama ni miongoni mwa wasomi wachache wanaotumia muda mwingi kuitetea nchi bila woga kwa maslahi ya vizazi vijavyo.
 
Dr.Lwaitama ni msomi makini sana na tukubaliane kwamba anauzalendo mkubwa sana hasa pale alipowalipua air precision ikidai kiswahili kitumike ndani ya ndege.naunga mkono serikali 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…