Sabau kubwa ya kuuliza swali hilo, ilikuwa ni kutaka kujuwa kama ni mtu huyo huyo au la, baada ya kupata majibu kutoka kwa wachangiaji tofauti, nimeridhika na nimeona kuwa hawa ni ndugu, iwe wa tumbo moja, au wa ukoo, au wa kutoka kijiji kimoja, kwa kifupi, kwa njia moja au nyengine wanahusiana.
Kilicho nisababisha niulize hivyo ni kuwa, niliwahi kusikiya kuwa Dr. Mwakyembe (wa TBS) anahusika na ufisadi wa kumpa mfanya-biashara mmoja wa Dubai, UAE biashara ya kukaguwa magari yanayotarajiwa kuletwa Tanzania, kwa misingi ya utatanishi, nikimaanisha yana ka-harufu harufu cha ufisadi.
Kwa kuwa si yeye, sina haja ya kumlaumu kwa kosa la nduguye. Ni hilo tu. Nashukuru kwa wote waliochangia majibu.