Dr. Mwigulu kushukuru na kupongezwa Jimboni kwake Iramba juma lijalo

Lyambalyetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2021
Posts
278
Reaction score
255
Mamba aliyepo kwenye kina kirefu kuanzia Jumamosi ijayo atakuwa Jimboni Iramba akitembelea kata na tarafa zake kwa ajili ya kupongezwa na wanaCCM kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na pia kuwashukuru wapiga kura wake wa Chamani kwa kumwezesha kuingia bungeni na hatimaye kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Mojawapo ya maandalizi tunayoendelea kuyafanya ni pamoja na kumwandalia zawadi zenye kubeba mila zetu za KiNyiramba ikiwepo togwa, matogo, "mandi", "mbilu" n.k pamoja na kumpa mavazi ya Kichifu kuashiria nguvu aliyonayo jimboni kwa sasa

Karibu Iramba Dr Mwigulu mbunge wetu na hongera sana kwa wema wako hadi kutukumbuka wanachama wenzio!
 
Wanyiramba mtaendelea kuwa masikini kwa muda mrefu sn, Mwigulu siyo kiongozi but anajua weakness zenu mnapenda nyama na pombe akishawanunulia anatimua vumbi mpaka mwakani tena mnabaki na shida zenu. Mtakaa sn kwenye nyumba za tembe bila maji, barabara, umeme na bei nzuri ya mazao.
 
Mpinzani wake jimboni wakt wa uchaguzi ni nani? Alishinda kihalali ili afae kupongezwa au alipitishwa na tume bila kupingwa?

au ndiyo kuanza kwa kampeni za chinichini za kugombea urais kipindi kijacho?

embu mwambie ajikite kumsaidia mama yetu kwanza kwa namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato ya serikali badala ya mumminya tu mwananchi kwa kodi inayo chezewa kwenda kununulia maviieeitee, misafara ya magari ya kifahar kwa wakuu wa mikoa nk...

badala ya kwenda huko, atembee nchi nzima akutane na wafanyabiashar nakusikiza kero na ishauri wao kwa serikali ya nini kifanyike.

mama apende asipende tutamwongezea muda wa kutawala, kwa sauti ya ndugai
 
Tutamshauri!
 
Wanyiramba mtaendelea kuwa masikini kwa muda mrefu sn, Mwigulu siyo kiongozi but anajua weakness zenu mnapenda nyama na pombe akishawanunulia anatimua vumbi mpaka mwakani tena mnabaki na shida zenu. Mtakaa sn kwenye nyumba za tembe bila maji, barabara, umeme na bei nzuri ya mazao.
Maneno yako yanachoma sana! Tunajifunza
 
Badilikeni broo
Tupe strategy ya kubadilika blaza! Tutaachaje sasa mataputapu yetu tuliyoyazoea? Tena kwa ziara yake Dr. Mwigulu pipa zisizopungua 150 zitanyweka Iramba juma lijalo!
 
Back
Top Bottom