Dr. Nassoro Ally Matyuza, Katibu wa chama cha madaktari wa michezo Tanzania

Dr. Nassoro Ally Matyuza, Katibu wa chama cha madaktari wa michezo Tanzania

beal

Senior Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
114
Reaction score
60
Dr. Nassoro Ally Matuzya ni daktari wa binadamu mgombea wa nafasi ya Katibu Mkuu chama cha wataalamu wa tiba ya michezo Tanzania (TASMA) ana uzoefu mwingi mno ndani ya chama hiki na masuala ya tiba za michezo amewahi kuwa daktari mkuu wa team ya Young Africans kwa vipindi tofauti, team ya taifa ya vijana wa Tanzania Serengeti boys na team ya taifa ya wakubwa Taifa Stars.

Dr. Matuzya ana sifa kubwa sana nchini kupigania masuala ya michezo na tiba za wachezaji kwa vilabu vyote kwa kuwa ni msimamizi wa tiba kwa wataalamu wote wa tiba za michezo wa kwenye vilabu vyote kwa kutoa elimu na kuhamasisha umoja wa vilabu kwa watoa tiba wote.

Wakati anaingia tasma kuna mambo yalikuwa mengi hayapo sawa amejitahidi kukutanisha wataalamu kuwa kitu kimoja na kuifanya sasa TASMA kujulikana nje na ndani ya Tanzania kwa usimamizi wa tiba za michezo nzuri amejitoa haswa kwa kutafta wataalamu mbali kuja kutoa mafunzo kwa chama hiki ili uweredi uwe mwingi zaidi kwa maendeleo ya TASMA.

Chagua Dr. Matuzya nafasi ya Katibu Mkuu ili ainue TASMA na kuleta maendeleo zaidi sifa yake kubwa ni mcheshi na mpenda maendeleo ya michezo ukiacha ndani ya mpira ana mchango mkubwa kwa jamii kwa nafasi ambazo anazo hakika wana TASMA twende na Dr. Matuzya atuvushe tusonge mbele kwa maendeleo.
IMG-20170729-WA0001.jpg
 
Weka C.V yake tuone...hasa elimu yake,udaktari sio siasa ni taaluma.
 
Huyu jamaa nadhani ni mzawa wa Sikonge Tabora. Ameshawahi kugombea ubunge Sikonge bahati mbaya alidondoshwa kwenye kura za maoni kupitia chama alichogombea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom