Jabulani ulichokisema ndiyo haswaaaaaaaah. Wanachojaribu kufanya kwa udi na uvumba ni kuonesha kuwa huyo mama hafai kwa sababu kiutendaji anafunika sana. Sasa hivi kuna mkakati mzito wa kuendelea kumng'ang'ania na wanashikisha viongozi wa the gambaz na wengine ni viongozi wakubwa sana serikalini. Hata hao MAWIO wamefanya makusudi kwa lengo la kuendelea kuwatia watu hasira kuhusu huyo mama ambaye mimi naona ni jembe chapa kazi lakini kwa sababu za kiimani wanatafuta kila njia ili aonekane hafai. Upo mkakati wa kutumia vyombo vya habari kumchafua na hasa hiki kipindi cha kuelekea mitihani ataandikwa sana ili Mkuu wa Kaya asalimu amri.
Jionee mwenyewe kinachoendelea kinaambatanishwa
Asante sana Mkuu kwa kutuletea hivyo vielelezo. Kweli Dr. Ndalichako anaonekana ni tishio sana na inaonekana wapo hata viongozi wa juu ambao hawapati usingizi kwa sababu yake. Nchi hii haitaki wachapakazi hata kidogo