Wakuu naomba mnifahamishe kama huyu dr anatibu kweli kisukari. Huwa namsikia mara nyingi kwenye vyomba vya habari akijinadi kuwa anadawa za kutibu kisukari.
Ni kweli anatibu??,,make dawa zipo za 50,000/=;150,000/=;300,000/= etc
Mimi nimekuwa na kisukari kwa miaka 13 natumia vidonge,nakula vyakula vya kawaida,situmii sukari,nafanya mazoezi na sijawahi kupata matatizo yoyote.Kuhusu hizi dawa mbadala sishauri mtu kutumia kwakuwa kuna watu wawili niliowafahamu walitumia na kuacha vidonge na wote ni marehemu sasa.