Dr. Ott ni mmarekani aliyekuwa anafanya kazi ya udaktari huko Kenya. Muda wote alipokuwa anafanya kazi hiyo aliwanajisi watoto wengi kwa kuwadanganya na zawadi pamoja na wengine kuwalipia karo za shule. Wamarekani wenzie walisikia tetesi juu ya vitendo vyake na kuamua kuvifanyia upelelezi na hapo ndipo kesi ilipofunguliwa na huyu daktari baada ya upelelezi kukamatwa akiwa amekimbilia Tanzania na kupelekwa U.S.A. ambako alihukumiwa kifungo hicho baada ya ushahidi kutolewa na yeye kukutwa na hatia.
Serikali yetu inapaswa kuiga mfano wa serikali ya mareakani ambako sheria ni msumeno kwani haijali cheo cha mtu wala utajili wake. Je kuna wakina Dr. Ott wangapi nchini Tanzania ambao wanawanajisi watoto wadogo na sheria inawalinda? Lazima watakuwa wengi sana kwani kama Alhaj Kapuya mpaka sasa bado analindwa ingawa kuna kesi ya kubaka imefunguliwa dhidi yake itakuwa hao wengine wanaowanajisi watoto wa nchi hii kwasababu ya umaskini wao? Tutafakari na tuchukue hatua.