Dr.Riwa anastahili pongezi sana katika hili jukwaa

Dr.Riwa anastahili pongezi sana katika hili jukwaa

LOOOK

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
3,389
Reaction score
674
Hayo ni maon yangu tu lakini natumaini nitaungwa mkono huyu jamaa anajitahidi sana kutusaidia hapa jamvini kila la kheri na mungu azidi kumtia nguvu nakuombea mema Dr. Riwa nimekuwa nisomasana michango yako na ushauri wako ubarikwesana mkuu.
 
ni kweli!

huyu ndugu si mchoyo wa maarifa, wangekuwa madokta wengine ungewasikia kila case wakisema niPM ili wapate chochocte ila huyu mpendwa huweka kila anachojua hadharani. namuombea baraka tele na Mungu awe naye katika huduma yake na amjalie mafanikio tele katika kazi zake

kwako Dr Riwa:
Mungu akutie nguvu na usituchoke kwa maswali yetu magumu na yanayosumbua, huwezijua, pengine ni kwa sababu kama hizi ndo maana umekuja duniani na umejaaliwa maisha hadi nyakati hizi!

Mungu akuongoze katika njia zako na kukuvusha kutoka utukufu mmoja hadi utukufu mwingine! amina

Glory to God!
 
Hata mie namkubali sana. Mungu azidi kumtia Nguvu Dr Riwa aendelee kutusaidia hapa jamvini..
 
Nilikuwa sijasoma Michango yake, hii post imenisababisha kuzipitia, NAUNGANA NA WENGINE KATIKA KUMPONGEZA
 
Nilikuwa sijasoma Michango yake, hii post imenisababisha kuzipitia, NAUNGANA NA WENGINE KATIKA KUMPONGEZA
inaonekana haupo active; RIWA ndo jembe letu la hapa JF doctor. tunapata tips za kufa mtu. kwa maelezo yake anaonekana amehama muhimbili(subject to be corrected), kwa sasa riwa anapatikana hosp ipi?? tunataka tumuibikie kwa misaada ya kiafya
 
inaonekana haupo active; RIWA ndo jembe letu la hapa JF doctor. tunapata tips za kufa mtu. kwa maelezo yake anaonekana amehama muhimbili(subject to be corrected), kwa sasa riwa anapatikana hosp ipi?? tunataka tumuibikie kwa misaada ya kiafya

Ni kweli mkuu huyu jamaa ni mtu fresh sana angetujuza anapopatikana ingekuwa vema sana.
 
Wandugu,

Nashukuru sana...tena sana kwa kuona na kuthamini mchango wangu hapa JF sana katika jukwaa hili la JF Doctor. Ahsanteni pia kwa dua, Husninyo ahsante 'free style'! Najitahidi kila pale ninapoweza kuchangia na/au kushea nanyi elimu hii ya utabibu na afya nikiamini kuwa kuna matatizo mengi ambayo hata wengine hawawezi kuongea na daktari wake, lakini anayamwaga hapa na tunajadili. Najua jukwaa hili lina madaktari wengine, manesi na wadau wengine mbali mbali wa afya ambao wana michango mizuuri tu, nami mara kwa mara najifunza kwao na kwa wachangiaji wengine pia! kwa kifupi ni jukwaa nilipendalo...

Nilifanya kazi kama daktari kwa miaka kadhaa Muhimbili, nikapata matatizo na mwajiri wangu (Wizara ya Afya), nikawa frustrated sana na kupractice clinical medicine, nikahamia kwenye utafiti wa masuala mbali mbali ya afya. Nimejikita zaidi kwenye 'afya ya jamii' kwa sasa, sitibu tena...hivyo sina hospitali ninayofanya kazi kwa sasa.

Lakini mara zote unapohitajika ushauri/ufafanuzi ambao upo ndani ya uwezo wangu, au issue ambayo naweza soma zaidi ili kuweza kushea nanyi nijuacho, basi karibuni kwa kuanzisha thread hapa jukwaani...au hata kwa PM...ni furaha yangu pale ninapoweza kusaidia.
 
Thanx Dk.Riwa yani kiukweli nilikua na idea ya kuanzisha thread kama hii ila mdau kaniwahi...kwa kweli huwa unasaidia sana watu nakumbuka mdau mmoja alikuaja na tatizo la kuota nyama sehemu fulani ya mwili yaani ulimsadia sana na maelezo yako yalitusaidia kuongeza uelewa wetu saana,Mungu akubariki.....
 
Thank u dr. riwa. Kwa kweli lugha ya kidr. unayo, MUNGU akubariki akutane na mahitaji yako yote ya kimwili na kiroho pia.
 
Dr Riwa pamoja na pongezi toka kwa ndg yetu kauk najumuika naye kukupongeza kwa kutokuwa mchoyo wa tiba. Vile vile nina shida kubwa ya fungus kwenye vidole vya miguu, nimejitahidi kutumia dawa nyingi na lotion pia lakini sipati nafuu ya kudumu. Hivi sasa naumwa miguu siwezi hata kuvaa viatu vidole vimevimba na vinatoa maji kwenye joints, naomba msaada wako Dr!!!!!!!!!! Naishi Arusha.
 
Tupo wengi tunaothamini mchango wa DR. RIWA, yani nikikuta swali huku huwa nafuatilia kujua dr riwa amejibu nn! Mungu akutie nguvu uendelee kutusaidia katika matatizo ya kiafya, tunajifunza mengi kupitia michango yako.
 
Asante Dr Riwa tafadhali endelea na moyo huo huo.
 
Binafsi naungana na mleta mada ni kweli dk. liwa anastahili pongezi. ubarikiwe na uendelee kutusaidia pale unapoweza maana matatizo duniani yanazidi kuongezeka.
 
Back
Top Bottom