Dr Riwa pamoja na pongezi toka kwa ndg yetu kauk najumuika naye kukupongeza kwa kutokuwa mchoyo wa tiba. Vile vile nina shida kubwa ya fungus kwenye vidole vya miguu, nimejitahidi kutumia dawa nyingi na lotion pia lakini sipati nafuu ya kudumu. Hivi sasa naumwa miguu siwezi hata kuvaa viatu vidole vimevimba na vinatoa maji kwenye joints, naomba msaada wako Dr!!!!!!!!!! Naishi Arusha.
Japo thread hii haihusu Fungus lakini labda nikujibu tuu....
Fungus ni moja ya vimelea vigumu sana kutibu kwani upata usugu wa dawa haraka sana, hasa Fungus wa kati kati ya vidole vya miguuni (Athlete's foot). Fungus hawa hufaidika sana na hali ya maji maji/unyevu miguuni.
Vitu vinavyopelekea kuwa tabu kuwatibu:
1. Unyevu unyevu miguuni, hasa kama unavaa viatu vya kufunika...kijasho kitatoka kidogo miguuni na hivyo kufanya hali ya unyevu. Hata kama unatumia dawa hawatapona
- cha kufanya ni kuhakikisha miguu inakaushwa vizuri baada ya kunawa au kuoga, vaa viatu vya wazi..sandals au kandambili kwa muda mrefu, uvae viatu inapohitajika tuu. Ofcn ukifika basi toa viatu ushinde na ndala.
2. Dawa zenye steroid...dawa nyingi za Fungus huwa zinakuwa na steroids ndani yake, steroids husaidia kupunguza inflammation (kama reaction ya mwili kwa ile infection). Lakini ubaya wa steroid zikitumiwa kwa muda mrefu zinapunguza local immunity ya eneo hilo husika, na hiyo immunity inapopungua hapo Fungus ndio wanachanua zaidi
- cha kufanya ni kuacha kutumia Antifungal zenye steroids (zipo nyingi, ukienda pharmacy mwambie akupe antifungal lakini isiyo na steroids, wanaelewa). Na kama ukitumia yenye steroids basi tumia kwa muda mfupi tu
3. Hygienic measures...fungus huwa wanapenda mazingira machafu (miguu, soksi, viatu), lakini tricky part is, huwezi kuosha miguu yako mara kwa mara kwani hutaifanya iwe na unyevu.
- cha kufanya kuosha miguu kwa maji yenye antiseptic (dettol), usiloweke, osha tu...kisha ikaushe kwa taulo safi ikauke kabisa, kisha paka dawa. Fanya hivi mara mbili kwa siku. Hili taulo unalofutia miguu usilirudie bila kuliosha na maji yenye dettol na kuanika likakauka. Na vivyo hivyo kwa soksi, zifue kwa dettol, na usizirudie bila kufua. Usivae viatu vya kufunika bila soksi, na ukifanya hivyo usivirudie mpaka uvifue preferably kwa dettol na uvianike vikauke.
Pia unaweza tumia Antifungal za vidonge mara moja kwa wiki kwa wiki si chini ya sita kama bado watakuwa wanasumbua. Pole