Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekutana na kufanya mazungumzo na Dr.Shein Mjini Zanzibar.
Mkutano huo uliofanyika ikulu mjini Unguja, tarehe 25 Septemba, 2018 ulilenga kumkutanisha msajili Mutungi ili kupatiwa baraka kumuwezesha kuendelea na hujuma zake za kuisambaratisha CUF.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana , Dr. Shein ameonekana kuunga mkono mpango wa hujuma uliopangwa na Balozi Seif Ali Idd ambapo amekusudia kutumia fedha za serikali kugharamia na kuitisha Mkutano Mkuu kwa lengo la kumvua uanachama na kumfukuza katika nafasi yake Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwatumia baadhi ya maofisa wa vikosi vya SMZ, maafisa wa idara ya usalama wa Taifa (TISS) na wanachama wa CCM.
Chanzo chetu kinabainisha kwamba katika siku za hivi karibuni Dr. Ali Mohamed Shein ameonekana kushiriki kikamilifu na wakati mwengine ameonekana kuhimiza kwa ukali mkubwa kila anapobaini ucheleweshaji wa hatua na mipango iliyopangwa.
Ukali wa Dr. Shein unaelezwa kutokana na kukerwa na uwepo wa Maalim Seif Sharif Hamad katika nafasi yake kama Katibu Mkuu wa Chama hicho.
Chuki hizo za Dr. Shein dhidi ya Maalim Seif Sharif Hamad zinachagizwa na kuongezeka kwa mbinyo wa kudai kuheshimiwa kwa matokeo ya Uchaguzi na kuheshimiwa kwa demokrasia na haki za binadamu kuongezeka kila uchao kutoka ndani na nje ya nchi hasa madola makubwa na washirika wa maendeleo.