Uchaguzi 2020 Dr. Shein miaka 10 iliyopita, nitaifanya Zanzibar iwe kama Dubai. Mwaka huu Magufuli nae kaahidi kuifanya Tanzania kuwa kama Ulaya

10. Kuheshimu haki za binaadamu.???!
Haki zipi wakati mashehe wapo ndani miaka nenda rudi, na uchaguzi wa huru na haki hakuna?
 
Daah nikajua huko Zenji hii michezo ni ya kutosha tofauti na huku bara.
Ilikuwa inafanywa bushi sehemu inaitwa Pwani Mchangani, kipindi icho ilikuwa kibali kinatolewa vijana tunakwenda kuburudika. Ila naona hawatoi tena na saivi watu wanafanya kimagendo. Kuna Njia ya Fumba alojenga Bakhressa, watu wanafanya drag Race lakini ni usiku kuanzia saa nne au tano uko.
 
Daah asante kwa ufafanuzi mkuu,maana nilikua najua zenji ni full kujiachia tu.
 
Nitafanya Tanzania kuwa Kama Ulaya...
Kazi kweli kweli.
Htr sn mkuu.....

Nakumbuka magufuli kwenye Sakata la MO amewahi kusema Watz sio wajingaπŸ€”πŸ€”
 
Huo Ni wajibu wa Serikali kuwafanyia hayo walipa Kodi wa nchi husika
 
Sasa hivi TBC baada ya Aridhio kuna kituko wanarusha wanaita "bongo kama Ulaya " wanaonyesha treni za Ulaya ,magari ya mwendo kasi na flyovers eti wapo kama Ulaya.

Wanatia aibu wangeonyesha maisha ya Tandale pia tuone kama ipo kama Ulaya.
Kuna neno hili ARIDHIO, naliona Tbc, maana Yake Nini?
 
Hahaha huwezi amini kuna vichwa huko CCM vinaamini kila kitu wasemacho hao watawala.

Kuna mtu wa CCM tulikuwa tukiongea akasema daraja la mfugale ndiyo ulaya wanaziita highway.
Yani wanaccm hawana tofauti na misukule ya gwajima...
 
Ohooooo........ Aliahidi ametekeleza mwinyi atasongesha mbele sio?
 
sentensi yako ya mwisho imekinzana na hoja namba kumi !!!
 
Chato tu miaka 20 ya ubunge ameshindwa.

Urais miaka 5 ameshindwa.

Sasa hili li inji looooteee ataweza kweli.

Wanasiasa waache ulaghai.
Hahahaaa...... Meko bana ni shida sn
 
Hahaaa...... Kwa hiyo ni km Dubai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…