SI KWELI Dr. Slaa ana siku ya pili akiwa kwenye mgomo wa kula kushinikiza kupata rufaa yake

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Shalom wana Jamii Forum. Habari zilizonifikia hivi punde kwa njia ya simu kutoka kwa familia ya Dk. Wilbroad Peter Slaa ni kwamba Dk. Slaa ana siku ya pili ya mgomo wa kula huko gerezani na ameanza kudhoofu sana.

Anatumia njia hii kama hatua ya kushinikiza sheria dhidi yake ichukue mkondo sahihi na si kumtesa bila sababu.
 
Tunachokijua
Dr. Wilbrod Slaa ni mwanasiasa na mwanadiplomasia ambaye amewahi kushika nyadhfa mbalimbali ikiwemo nafasi ya katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), lakini pia amewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Sweden mwaka 2018 na baadae kuvuliwa hadhi ya ubalozi mwaka 2023.

Dkt. Slaa alikamatwa usiku wa January 10, 2025 nyumbani kwake na Jeshi la polisi ambapo baadae alifikishwa mahakama ya Kisutu kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa X ambapo inadaiwa ni kinyume na sheria ya mitandao.

Aidha Dkt Slaa hakuwepewa dhamana licha ya kosa aliloshitakiwa nalo kuwa na dhamana ambapo wakili Boniphace Mwabukusi alieleza kuwa baada ya walipofika mahakamani walikuta Jamhuri imewasilisha kiapo cha kupinga Dkt. Slaa asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake lakini mawakili wa upande wa utetezi hawakuwa wamepewa kiapo hicho hivyo kuhitaji muda wa kukifanyia kazi kiapo ili kuandaa kiapo kinzani.

Kumekuwapo na taarifa zinazodai kuwa Dk. Slaa ana siku ya pili ya mgomo wa kula huko gerezani na ameanza kudhoofu sana.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa ya Dkt. Slaa kutia mgomo wa kula akiwa gerezani si za kweli.

Aidha katika kuutafuta uhalisia JamiiCheck iliwasiliana na wakili Peter Madeleka ambaye ni miongoni mwa jopo la mawakili wanaomtetea Dkt. Slaa ambapo alikanusha uwepo wa taarifa hizo huku akisema anaendelea vizuri.

"Dkt. Slaa anaendelea vizuri, hajafanya mgomo wa kula kama inavyodaiwa, hizo ni stori za kutunga kutoka kwa baadhi ya watu wenye maslahi yao binafsi"

"Hata jana (Februari 12, 2025) nilienda kumtembelea gerezani, anaendelea vizuri, hawezi kumpigia magoti Mtu kuomba atolewe kinyume cha Sheria, yuko tayari akae gerezani hata miaka 20 kwa haki na sio kutoka kwa kumnyenyekea mtu"
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…