Ntambaswala
JF-Expert Member
- Dec 7, 2008
- 255
- 78
Kikwazo kikubwa cha kuleta mabadiliko ya kweli nchi hii ni wasomi na wakaazi wa maeneo ya mjini. Nimesoma kwenye threads nyingi hapa, watu wengi wenye mashaka kuwa DR Slaa hatapita ni watu ambao wanatamani mabadiliko yatokee ila hawatambui kuwa wao ni sehemu ya kufanya hayo mabadiliko yatokee.
Jana tulikuwa na wenzangu hapa Mzumbe University (Dar Campus) tunajadili kuhusu uchaguzi. Wengi wakawa wanasema watafurahi sana siku CCM ikiondoka madarakani. Lakini papo hapo wakawa wanasema Dr Slaa hataweza kuishinda maana CCM ni ''wezi'' wa kura hivyo haina haja ya kwenda kupiga kura maana upige kura usipige watashinda tu.
Nilisikitika sana maana tuliokuwa tunajadili wengi walikuwa ni wanafunzi wa shahada za uzamili. Nikajiuliza hivi wasomi wa nchi hii wana matatizo gani, maana hii si mara ya kwanza kusikia maneno kama haya kutoka kwa wasomi wa nchi hii. Nilishaona mwaka 2000, 2005 na sasa 2010.
Lakini cha ajabu mwezi wa tatu mwaka huu nilitembelea wilaya ya Newala kijiji kimoja kinaitwa Nkunya, nilikutana na wananchi wengi ambao kielimu naweza kusema sio wasomi- yaani ni darasa la saba kushuka chini, wao walikuwa wanasema kulingana na tabu wanazozipata akijitokeza mgombea yoyote wa upinzani ambaye ''anaeleweka'' wao watampigia kura na atashinda bila shida maana wamechoka na CCM. Maelezo kama haya nimeshayasikia mara nyingi sana huko vijijini kutoka kwa watu wasio wasomi.
Sasa najiuliza kwanini wasiosoma wanaona upinzani unaweza kushinda lakini waliosoma wanaona tofauti?. Zamani kidogo kuna mwalimu mmoja mstaafu aliniambia tabia ya watanzania wasomi kuwa wapole, kuburuzwa, uoga wa kuthubutu na kutokuwa tayari kujitoa mhanga ni mpango kamili ulioratibitiwa katika aina ya elimu tunayopatiwa- yeye alisema Nyerere alitengeneza mfumo wa elimu ambao unatufanya tuwe hivyo. Sikukubaliana na mawazo yake kwa vile huyo mwalimu alikuwa hampendi kabisa Nyerere.
Lakini sasa naanza kuamini watanzania ambao hawajasoma (wengi walioko vijijini) hawajalishwa sumu (indoctrinated) na elimu ya ''Nyerere'' ndo maana wanaona mageuzi yanawezekana lakini wasomi wanaona tofauti.
Anyway, unahitajika utafiti kubaini kwanini wasomi wako pessmistic upinzani kushinda tofauti na watu wasio soma?