Elections 2010 Dr slaa anaweza kuangushwa na ''wasomi''

Kwa kweli wasomi ni problem,wengi hata kwenye daftari hawajiandikishi.Wanajifanya hawana muda wa kupanga foleni...Tunahitaji kubadilika wasomi wa Tz.
 
Unazungumzia "wasomi" wa Mzumbe au Tanzania nzima? Mimi naona nguzo ya Slaa ipo kwa mwananchi wa kawaida zaidi!! Kwa uamuzi huo wa hao "wasomi" wa Mzumbe nadhani naanza kukubaliana na jamaa zangu waliokuwa wanajadili kiwango na uwezo wa upembuzi wa mambo kwa wasomi wa vyuo vyetu....wangeuka kuwa wanfunzi wa sekondari sasa.....
 
Hao sio wasomi ni walioenda shule bila kelimika. Leo nimesikia wanachuo wa UDOM walioko field wamebadilika kuwa ombaomba kwani Bodi ya mikopo imewasahau. Nilicheka sana kwani ni ujuzi walimchangia JK achukue fomu, wakidai kafanya vizuri. Hawana kitu wanakariri tu;
 

Point.............. 100%
 
Watu wanaojiita au kuitwa wasomi hapa Tanzania ndio kundi la wananchi hopeless nambari wani katika kuleta mabadiliko. Wengi wao, wakishabahatika kuwa na ka-gari, na nyumba na mkono unaenda kinywani, baasi hawataki kusikia mabadiliko.

Nimeongea na baadhi wa walimu wa vyuo vikuu. Wanamkubali Dr Slaa. Halafu wanasema he came a bit too early kugombea uraisi. Nimewauliza kura yako utampa nani? Hakuna jibu la kueleweka. Ni unafiki na ujuha uliowajaa wasomi wetu. Shame on you!
 
Invicible,

Wasomi waliogopa kukuambia kura watampa nani. Wanakuja hapa JF, na wote wanataka Dr. Slaa akomboe nchi. Wakipata nafasi ya kupiga kura ya siri, watamchagua Slaa.

Woga uliojengwa ndani ya mioyo ya Watanzania kwa miaka 50 ni mkubwa sana. Utachukua muda kutoka. Wasomi bado waoga!

Nisimulie kituko kimoja cha kuogopesha wananchi. Kampeni za uchaguzi za 1980, nilikwenda Nkrumah Hall kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Ulikuwa wakati wa kura za NDIO au HAPANA kwenye kura ya Rais. Upande wa HAPANA kulikuwa na picha ya ukuta. Mkuu wa Wilaya akatuonya vikali tusijigonge ukutani! Ilikuwa ndio nipige kura kwa mara ya kwanza. Nilisuza, na hadi leo sijawahi kupiga kura.

Inawezekana, timiza wajibu wako. Mbona imewezekana kuving'oa KANU na UNIP?
 
wasomi wetu wengi wao wamesomea chieti na si kuelimika ndo maana wako hivyo!!
Taib,kama tatizo ni 'wasomi' mboni hata huko CCM wamejaa?? akina Mwakyembe, sijui nani etc etc..To say the truth wasomi wa ukweli Tz ni kama hamna na kama wapo ni kama asilimia isiozidi 1,ndio maana mambo yataendelea kuwa vivihivi milele.
 
sio wasomi, wengi watakamuangusha ni watu wa chini

Wasomi wengi watachangia si kumwangusha Slaa tu,bali wasomi wanachangia kuchelewa kwa mageuzi na maendeleo ya nchi hii. Ilikuwaje jimbo la Ubungo lenye watu wengi wenye uelewa CCM wakashinda 2005 na wale ndugu zangu wakulima pale Mpanda Rukwa wakakataa sera mbovu za CCM au pale Tarime dhidi ya wasomi/wajanja wa dar?

Wasomi wanatakiwa kuwasaidia wasiosoma kuzieleza sera za vyama kwa kuchambua vizuri mbele ya wazee wetu,lakini wao ndio kwanza wanafanya kinyume. Wasomi wetu wakibadilika na kuwa na ujasiri hata wa kukosoa na kuelekeza hadharani nchi yetu itabadilika haraka.

Ni mchango tu.
 

Mkuu tupo pamoja taitizo watu wanaangalia upande mmoja wa shilingi, watu hawataki kujiuliza kwanini hivi, Mimi nipo pale pale je upinzani wamefanya nini kuwashawishi wasomi kuwa wao ni mbadala halisi wa CCM?
Au wapigie tu upinzani kwasababu ni upinzani?
 
wasomi wengi wa tanzania ni waoga wa mabadiliko wamekarili tu mfumo unawangozi ndiyo sahihi, utasikia utafuti wa REDET utakavyompamba kikwete,

Kabisa wasomi na niongeze wale waliopitia vyuo vikuu ni waoga wa kutupwa...maprofesa ni waoga tena mno. Kwa nini? Ni mfumo- nchi ya amani na utulivu (mhhhh!!!) lakini mishahara na marupurupu kiduchi kwa watu hawa, lakini akivuka mipaka akaingia kwenye mfumo, kama mshauri, mkurugunzi, memba wa bodi, mara matatizo yote ya fedha yanakuwa hadithi...maprofesa na wasomi wanabembeleza mfumo wa kisiasa ili wapate vibakishsishi vya cheo, na amini usiamini hata pale CCM walikuwa wanatuhumiwa kwa kushindwa kufanya mengi jijini Dar, ni Dar penye kusanyiko la wasomi wengi walipata kura nyingi katika chaguzi zote..Na ukichungulia takwimu vizuri utaona wapinzani wamekuwa wakipata kura nyingi hapa Dar sehemu za walala hoi kule Manzese au hivyo.

Pili, nahisi wasomi hawaguswi vya kutosha na hali ngumu ya maisha inayosababishwa na mfumo wa kibabaishaji wa siasa wa awamu zote zilizopita. Sababu ni pengine wana jinsi ya kutorokea matatizo haya labda kama hapo juu kukikmbilia siasa au kutafuta huduma za ushauri(consultancy). Kuwa na mabadiliko katika chama tawala kwao kunaleta hofu, hofu ya mabadiliko ya mfumo na kuzibwa kwa mirija ya kujinufaisha. Wanataka hali ibaki ile ile. Ni muhimu sana jitihada za kuleta mabadiliko zikaelekezwa pia kwa kundi hili, kwa kupitia wanaharakati wachache baina ya wasomi.

Tatu, ni vyema pia tusisahau mfumo wa chama kimoja na urithi wake ulijenga jeshi kubwa la maafisa kachero-(mashoga - sema spies au wana-usalama) ambao wamejaa kila taasisi. Hawa wanasimamia maslahi ya Chama Tawala na sio Serikali. Bahati mbaya wana ushawishi mkubwa na wengi ndio wanatawala taasisi za juu (sina uhakika sana na hili, lakini inasemwa hadharani tu kuwa huwezi kuwa na cheo kama hujawa vetted). Viongozi hawa wana desturi ya kuwamulika na kuwagandamiza wenye mawazo ya upinzani. Matokeo yake ni mara chache sana utasikia midahalo ile mikali mikali kama ya enzi za kina Shivji, Mushi, Walter Rodney na wenziwe miaka ile ya 1970 katika vyuo vyetu. Inawezekana sana sio 'elimu ya Nyerere' iliyowadumaza wasomi bali ni hili dude la maisha bora hewa (rushwa na mdogo wake ulaghai) na utawala wa mabavu kupitia wana usalama. Kama ningekuwa na madaraka ni kuangalia upya kabisa na kutengenua usalama wa taifa, kuona tunahitaji nini kwa usalama wa taifa na sio kwa nafasi ya nani awe nani katika uongozi wa taifa
 
Wasomi by nature wanaweka nadharia zaidi.Msomi unaweza kumwambia hilo hapo andazi kwenye kisahani yeye akakwambia hizo ni atoms za carbon zimejipanga.There is a danger of overanalyzing the crude political system in Tanzania.

Kama unajua kweli CCM ni wezi wa kura, na huwataki, huu wizi wao kwangu mimi ni sababu tosha ya kukuhamasisha uende kupiga kura, tena uhamasishe wenzako wengi waende kupiga kura, ili kuwe na tofauti kubwa kati ya kura za wapinzani na zile za CCM na hata wakiiba iwe wazi kwamba wameiba.

Kukataa kupiga kura kwa sababu CCM wanaiba si usomi, ni a self defeatist attitude.Msomi wa kweli hawezi kukubali kuchukua a self defeatist attitude. Tuseme ukweli tu kwamba Watanzania struggle hatujazoea, na tunavyozidi kusoma ndivyo wengi tunavyozidi kutaka wengine watufanyie kazi, tunataka CCM atupe ushindi kwenye kisahani cha dhahabu.

Mimi naona kuna watu wameenda shule tu, na wamepata vyeti, lakini wasomi ni wachache.Tungekuwa na wasomi tusingekuwa na matatizo ya umasikini kama tuliyonayo sasa.
 
Kimsingi wasomi wapo wengi tu, Kwa maana tusemapo wasomi nadhani si wale wa chuo kikuu to. na hata tukisema hao
bado ni wengi. lakini kujitokeza kwao katika mambo haya imekuwa ni vigumu sana ila ni kelele tu.
Yaani mchango wao ni mdogo sana na hao ndo wanaiangusha nchi hii.
 
" Wasomi by nature wanaweka nadharia zaidi.Msomi unaweza kumwambia hilo hapo andazi kwenye kisahani yeye akakwambia hizo ni atoms za carbon zimejipanga.There is a danger of overanalyzing the crude political system in Tanzania..." (Kiranga)

Hapana Kiranga, hatuna wasomi wa upeo mkubwa kama huo! Unatakiwa tu usome makala za wasomi wetu hazina uwezo wa kulinganishwa na za wenzao katika vyuo vikuu vingine...kwa urahisi ningesema hawana uwezo wa kujua hata hizo andazi ni atoms ...natamani ningeweza kutoa mifano hai hapa lakini yaweza kuzua utata (kuweka makala halisi za kitalaamu). Huwezi ukawa Profesa kwa kuwa tu umeitwa Profesa au umepewa cheo cha Profesa. Kwa nini jamii isikuone wewe kama Profesa. Kuna mtu anaweza akawa na utata wa uprofesa wa Shivji? Marehemu Chachage? Baregu? Lakini hao walio kifua mbele sijui ni wakuu wa mashule, vyuo na watetezi wa vitu kama Redet - wana mchango gani katika jamii ambao ungeweza kuwataja ni maprofesa? Magwiji wasomi kina Kimambo tunawajua sio kwa sababu UDSM wametuambia huyo ni Profesa la hasha, kwa kuwa tumeona kazi zake.

Kwa hiyo haja ya usomi hapa ni tabu kweli kweli, ni wasomi wasioiva, waliojipa mavyeo, wakaanga njaa zao, wanaojikomba kwa mfumo wa siasa, wasiopenda mabadiliko, na wasiojali matatizo ya jamii kutokana na ubinafsi wao. Nyerere alisema nini? jamii inakusanya kila walichonacho wanampa mtu mmoja akawatafutia neema na yeye anatokomea (akizungumzia ufadhili wa elimu kwa wachache)!
 
Kweli tupu umeongea yale yanayotokea , wasomi wangeunga mkono upinzani kwa wazi sasa hivi tungekuwa tunaongelea Tanzania yenye mchanganyiko wa mawazo ya kiitikadi na kisiasa,kwa maana hiyo uwakilishi ungekuwa sawia na raslimari za nchi na pato la taifa lingeongezeka na maisha ya kila mtanzania yangeboreka.
Inasikitisha kuona wasomi na watu wa mijini baado kabisa hawajachangamkia uamuzi wa busara wa kuchagua vyama vingine zaidi ya CCM wasomi,maprofesa wote wanajikita kutaka kuingia kwenye siasa kupitia CCM,lakini vijijini tunakosema hawajimudu wao ndio wameweza kwenye baadhi ya halmashauri kukamata halmashauri hizo ,kwa hiyo biidii ya elimu ya uraia na uzalendo ikita katika pande zote vijijini waliko wapiga kura wengi na mijini ambako watu upako na uamsho wa ukombozi haujaingia vizuri masikioni mwao,na uoga haujawatoka.
Mazingira ya wasomi na watanzania kukataa kuweka viongozi mchanganyiko toka vyama imara utakuja kutufikisha mahali pabaya sana ,mara nyingi watu wasipotumia haki yao ya kikatiba ya kupata viongozi bora huwa kuna chuki na hasira inayojengeka ndani ya mioyo yao,
Kupoka haki ya mtu kwa kugeuza matokeo ya aliyeshinda na kumpa aliyeshindwa,au kutokutoa fursa sawa za kugombea au kuiba kura zilizopidwa jibu lake litakuja kuwa kama bomu la atomiki,nchi hii ni kubwa sana itakuja kuwa shida mno kuzima fujo kama ilivyo kwa Congo, na nchi zingine zenye mavurugano,ningewaomba hawa CCM na vyombo vya habari kama television ya taaifa na ITV wakome kabisa kuwafitinisha wananchi kwa kuwatisha kwamba kuchagua upinzani vurugu zitattokea,ukweli tunaelekea kwenye vurugu kama mizania ya uchaguzi wenye haki,salama na ukweli hautakuwepo,olee wao wanaochezea hii amani tuliyonayo tutakuja kuitafuta na tusiiione tena
 

Mkuu hapo kwenye red please note:
maelezo yako ya mwanzo unaonekana kuwa na mantiki na kuwashangaa wasomi wenzako wa digrii ya Uzamili. Huku ukiwalaumu wenzako, na wewe mwnyewe umeungana nao kwa mlango wa nyuma kwa kupinga uliyoambiwa na huyo mwalimu. ALICHOKISEMA HUYO MWALIMU NI KWELI TUPU.
Ukweli ni kuwa mfumo wa Elimu wa tanzania unawaandaa watu kutokuwa JASIRI WA KUTHUBUTU, na ndiyo sababu wasomi wa nchi hii wako tayari kuongozwa na mambumbumbu ali mradi tu mambumbumbu hao wamethubutu kujiingiza kwenye siasa na wamewaahidi vyeo vya bure-ukurugenzi, ukamishna, etc. Hata waajiri binafsi wengi si wasomi wa kutisha, wanaoendesha biashara hapa nchini, kwa mfano, wengi wao si wasomi wa ngazi za vyuo vikuu. Usomi wao ni katika kujua na kudiriki kupambana, they are realists.

Si vibaya, chukulia mfano wa Shigongo ambaye amediriki kuanzisha biashara ya magazeti na sasa anawania ubunge, je ni msomi wa chuo kikuu? Je pale Global Publishers hajaajiri wasomi?

Na pengine sababu huyo mwalimu alikuambia hivyo kwa kuzingatia hesabu hii.
Kumbuka ulioanza nao darasa la kwanza, wangapi walibahatika kupata elimu ya sekondari..................kwa nini wengine walikosa, je hawakuwa na akili?
O-level, wengine waliishia wapi, kwa nini?
A-Leve je?
Chuo kikuu undergraduate, wote uliokuwa nao darasani kuna hata mmoja uliyetoka naye kijijini kwako na au ulikuwa naye darasa la saba, form four au form six? Kwa nini iko hivyo? na wewe mwenyewe ukiwa mmoja wa waliobahatika kuelimika hivyo, uko tayari kupambana kutetea maslahi ya wanyonge hata kama ni kupotesa ajira yako na marupurupu yako? kwa nini mangumbalo wasioweza kuanalyze issues wanajiingiza kwenye siasa na wanaweza? kwa nini wasomi wanaogopa wanabaki kulaumu tu pembeni?
-tatizo ni elimu tuliyoipata na hapo ndipo penye shida.

Ukiangalia hata wasomi wanaojitokeza katika masuala ya siasa, wengi wao utakuta kwa namna moja au nyingine wamebahatika kupata elimu ya nje ya nchi hii. wenye Bachelor na Digree za uzamili za hapa bongo ni waoga mno.
Usomi wa nchi hii ni kuajiriwa na kukopa pesa benki na kununua gari, huku umepanga kwenye nyumba ya msomi aliyefeli mtihani wa darasa la saba au form four, but ana ujasiri wa kupambana na mazingira.

tuache kumshambulia Malaria Sugu, maana wasomi mmewaachia watu kama yeye kuwa viongozi wetu. Nchi hii itabadilika pale tutakapoacha kuwa waoga.

NOTE; I have nothing personal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…