Elections 2010 Dr. Slaa: Beware of Swift Boat trap!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,540
Dr. Slaa,

Majuzi ulilazimika kusimama kwenye kampeni ukatufungulia maisha yako na mahusiano yao na mchumba wako Bi. Josephina.

Hii ilikuwa ni nia wako kuweka sawa kile ambacho CCM wameanza kukifanya cha kukupata tope la kutokuwa muadilifu kwa kuangalia mahusiano yako na Bi. Rose na Bi. Josephina.

Umeshatoa jibu moja na linatosha. Hauna haja ya kuendelea kutoa hadithi hii au ufafanuzi wa ziada kwa mtu yeyote yule tena.

Lakini, katika majibu yako na kufafanua kwako mahusiano yako ya kiunyumba/ndoa, uliingia kwenye mtego uliotegwa makusudi.

Ulijibu hoja kwa kuwahoji Yusuphu Makamba na Kingunge Ngombare Mwiru na kuwahoji maisha yao na mambo walioyafanya kama vile kuonyesha kuwa wao nao si Waadilifu au hawana mamlaka ya kuongea kuhusu uadilifu.

Mheshimiwa Dr. Slaa, Makamba na Kingunge au yeyote yule wa CCM ambaye si Kikwete si wagombea Urais na hawana lolote lile la maana na wapuuzie bila kupoteza muda wako kujibishana nao.

Wewe unayeshindania naye urais ni Kikwete, he should be your Target and not the attacj dogs.

Sasa hawa wanakuchezea mchezo ule ule waliomgfanyia Salim, nawe tafuta attack bulldogs wako washambulie haya mengine na wewe ubakie kufanya Kampeni za kujinadi wewe na Chama chako na ni nini mtafanya kwa Tanzania.

Aidha kampeni zako ziwekeze kuchambua miaka mitano ya Kikwete na miaka 50 ya CCM hususan miaka 20 ya mwisho na si maisha binafsi ya mtu.

Angalia sana unaweza potea muda jibishana na Makamba mambo ya Udaku ambayo si presidential material nawe ukapoteza nguvu na nafasi ya kuwaambia Watanzania kwa nini KIkwete na CCM hawafai.

You are presidential candidate, with presidential image and credibility, stivk to presidential status and do not allow any one to Swift boat ypu the way Kerry was Swift boated in US elections of 2004 ending up spending a whole heck of time and campaign time fighting Swiftboaters and not addressing the incompetencies of George Bush.

Attack Kikwete on his leadership and his failure to bring progressive development to Tanzania.
 
Unfortunately bulldogs wake wote nao ni wagombea majimboni....:mad2:
 
Rev Kishoka
Uko sahihi kabisa. Dr. Slaa asipoteze muda kubishana na taahira Makamba. Dr. Slaa tuanchie sisi tutakula sahani moja na makamba pale atakapoendelea kuleta upuuzi wake.
 
Ngoja Taso na Companero waione hii uone utakavyolaania kwa kulinganisha (au hata kutolea mfano tu) siasa za Marekani na Tanzania
 
Ni ukweli mtupu, apuuzie udaku wa CCM, afafanue madhaifu ya utawala wa JK na CCM,

Kwanini ahadi za mwaka 2005 hazikutekelezeka, atawezaje kutekeleza ahadi mpya?
 
Mchungaji,
Labda wewe watakuelewa mimi niliposemea hii niliambiwa niache kuishabikia CCM (double standard)...kumbe kuna watu wanaona mbali kama wewe, wasaidie kuwazindua...the hit backs should not be by mud smearing campaigns but on what CCM claims to have done in the past 5 yrs or so...mfano hapo chini.


 
Hivi Chadema wana nani anayefanya kazi ya kupiga domo wakati huu wa kampeni kama CCM walivyokuwa na Makamba?

Makamba alitakiwa ajibiwe na mtu mwingine Chadema mwenye kazi hiyo (level ya Makamba) na sio Dr Slaa ambaye anagombea uraisi.

Mpaka wakati huu namsikia Dr Slaa peke yake....where is the team?
 
Kishoka nakubaliana nawewe juu ya Slaa ila niongeze angalizo- najaribu kutafakari majibu ya Slaa kwa upana wake, na hapa nitasema si kwa kudhihaki bali kwa kujaribu kutumia piccha halisi ambayo nadhani hata yeye kama mwanafalsafa atakua ameifikiria- ishu hapa ni kupata kura- ameangalia wapiga kura wengi ni akina nani? ni vijana- Je vijana wengi wakitanzania wana haiba gani kwenye masuala ya siasa-, wana jali hoja ama nani yuko safi maisha binafsi? kwenye hili napenda kutumia uwigo wa magazeti yetu ya udaku na namna ambavyo vijana wanalishwa "news". Mtu ambaye kijamii ni "mchafu" anaonekana hafai- potelea mbali sera zake ni nzuri- nimeenda kasi lakini nitaanzia hapo- hivyo basi, ninavyoona kujibu kwa kuchafua ni sawa na kusema - toa kwanza kibanzi kwako- na kwa kuwa vijana wengi wanapenda kusikia hayo (ninaishi tanga- natumia expernece hiyo) nafikir naye anlipojibu alikua anawaambia- "na nyie chambueni ya hao wanaojidai ni wasafi"- kwa mantiki hii, kama Silaa atatumia muda mchache kujibu hilo ambalo wengi wanatumia kigezo cha kupigia kura- sio vibaya- na ujue kwamba watu wengi hawajali sana kujua "social contract" - hzi ilani ndani muna nini- hata humu JF nahakika ni watu wachache sana- Slaa anatumia kile ambacho Franz fanon alishauri - violence -kwa violence- kwa kuwa lugha ambayo vijana wanaielewa zaidi ni nani msafi na yupi mchafu- ndio anafaa- akaamua kuwajibu nao kihivyo.
 
Msimdanganye dr.mwacheni mara mojamoja ajibu mapigo.vinginevyo watammaliza
 

Inakuaje iwapo wao wanakuja na attacks ambazo ni personal. Asijibu in kind? Hawa CCM wana mbinu chafu sana na katika siasa hakuna hicho unachotaka kiwe -- yaani wao warushe madongo yake binafsi naye DR Slaa ajibu kistaarabu! Nchi hizi za Kiafrika ukifanya hivyo katika siasa umekwisha! Tit for tat should be the game -- and that's what CCM knows best.

Isitoshe hawa akina Makamba na Kinana ndiyo wasemaji wakubwa wa JK -- why not attack them? I think it has worked and it will work effectively. Yakipatikana na ya JK binafsi naye ayamwage! Hakuna ustaarabu tena hapa -- kwani wao hawataki ustaarabu!
 
Nilisema,ninasema na nitarudia kusema kuwa Dr.Slaa anaelekea kufilisika kisiasa...anajichimbia karibu lake mwenyewe.just imagine ma week mangapi yamepita toka campaign zianze...actualy ni muda mrefu bt cha kushangaza huyu jamaa mwenye Ph.D ya Divinity hanadi sera wala ilani(manifesto) ya chama chake...yeye ni kupiga zogo na mipasho majukwaani...alianza na makamba,akaja Kinana,then Pinda na mzee wetu Mkapa...jamani wana CHADEMA kama mpo(coz mm sina chama jamani) mwambieni SLAA anadi sera coz we are not interested na mipasho yake and his marriage saga la sivyo heshima yake itazidi kushuka....
 
Rev.

Siku ya kwanza alianza Marando. Ndiye aliyemwaga kuwa Mkapa, Kikwete, Lowassa na Rostam ndiyo waliochukua pesa BoT na hapo matangazo ya TV LIVE yakakatwa.

Nakubaliana na wewe kuwa yeye abaki KUMSHAMBULIA Kikwete na CCM na hawa akina Kinana, Makamba, sijui mume wa mtu wabaki wakishambuliwa na akina Marando peke yao.

Junius, tunachokikataa kwako ni pale unaposema ASISHAMBULIE KABISA yeye au kundi lake.

Alichokisema Rev ni kuwa Slaa amshambulie Kikwete na CCM na hawa wa chini awaachie wa chini wenzake.

Sijui kama unaona tofauti. Kuna swali? Hakuna swali, Kawawa funika Kikombe (JKN akiwa Kizota).
 
Sikonge,
Unanilisha maneno, nilisisitiza sana kuwa CCM wanampotezea mda Dr. Slaa kwa kuwa wanajuwa uwezo wake wa kueleza na kufafanuwa hoja mpaka mwananchi wa kawaida akafahamu ni mkubwa...kumuingiza kwenye kampeni za matusi na uchokozi ni dhahiri wanam-divert kutoka kwenye malengo na hilo kiasi wamefanikiwa.

Nilisema hivyo, nikijuwa kuwa tayari Prof Mwesiga Baregu anawarudi kidogo kidogo na mimi wala sikumgusa. Halafu ukumbuke kuwa ni vyombo vya habari vinavyo highlight issues za kampeni kwa hiyo hata kundi lake likijibu linatakiwa liwe makini nini linajibu vitu vingine ukivipuuza na kuviacha vife vyenyewe watu wala hawaulizi. JK alipoambiwa ana mke mdogo mlisikia likavuma kama ngoma ya usiku? alijibu mara moja tu mpaka leo kimya!
 

Kijana Mkweli,

Sio kwamba Slaa anapiga domo tuu, bali media zinaandika habari kwa angle hiyo tuu kwani ndizo habari zinazouza gazeti. Na kumbuka ownership ya vyombo vingi vya habari ni mali ya CCM, sasa unategemea vitampa airtime ya kueleza sera zake?
 
=======

Kwanza nikiri for the first time, Rev. Kishoka amenipata hata mimi.
Pili, Dr. Slaa ananendelea vema na kampeini na mambo haya ya udaku hayamsumbui hata kidogo. Sisi wapiga kura tunaelewa hii ni njia ya kumchelewesha. Chadema hawajalala pia, baada ya muda mbwa wakali wa Dr. Slaa watatoka na manyigu na ninawahakikishia, mwenye roho ndogo itabidi afunge screen yake, maana akuanzae mmalize.

Hata aliyemlala binti yake, atawekwa hadharani! Dr. Slaa anaendelea na kazi yake. Hatajibu, kama CCM walivyoamua kutojibu hoja zake za ufisadi. Mkuu wa nchi na mgombea katajwa ni fisadi, yuko kimya. Tunamtaka akanushe tuone.
 
Rev
This is crap, tell it to the babies; so far Dr Slaa is doing very perfect!! Haanzishi attacks, bali anajibu mapigo that is what he is supposed to be doing! What the hell do you think he has to be doing? One issue[rumour] spoken hundred times will be taken as truth. Who has to answer on behalf of Dr? He is doing it very well and perfect! For your information, if you are following, he has completely silenced Mr. Makamba aka Kasuku.

Bravo doctor, tell it to the birds!! Do it briefly as you are doing, and we will finish it!! God bless you!!
 

unasema 'we will finish it' wewe na nani? Wapi? Na wakati gani? Dont tell me utakuja kumaliza hasira zako hapa Jf...ninaomba ufafanuzi wako kaka mkubwa...
 
Makamba hastahili kujibiwa hata na mbwa... hadi aconfess issue ya kubaka
 

wewe humjui Makamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…