Kwa mara ya kwanza nimebubujika machozi -- hasa pale alipochambua sera yake ya elimu bure na afya bure kwa kugusia kuwa Nyerere aliweza hivyo bila ya kuwa na migodi ya dhahabu na madini mengine mengi -- na pia kubanwa na wafadhili!!
Kwa mara ya kwanza naamua kumpa kura yangu Dr Slaa na ninaahidi kila siku nitajaribu kuwashawishi watu wengine kumi wafanye hivyo. Na ninawaomba watu wenye nia njema na nchi hii wafanye hivyo. Machozi yalizidi pale alipojibu swali la uamuzi wa kugombea kwake -- kwamba alitetemeka wakati anaombwa hivyo.
Kwa mara ya kwanza pia nimeelewa kwa nini JK hataki mdahalo: Hana ufasaha wa kuongelea mambo. Na huo ndiyo ukweli jamani, baada ya kumsikiliza mheshimiwa Dr Slaa.