Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
Tetesi toka vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa Dr Slaa anatafakari kugombea urais kutokana na shinikizo toka kwa wananchi ndani na nje ya chama chake.
Habari zinaeleza kuwa hata uamuzi wa viongozi wakuu wa chama hicho na wabunge kufanya kikao cha pamoja Dodoma ilikuwa ni sehemu ya hatua kuelekea maamuzi hayo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wakati CCM ikifanya kikao na wabunge wake Dodoma na Kamati ya Mwinyi, wakati huo huo kikao cha Mbowe na wabunge wa CHADEMA na wakurugenzi wa chama hicho kilikuwa kikiendelea.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kambi ya Lowassa na Rostam Aziz kupata taarifa hizo sambamba na kikao cha kawaida cha kuidhibiti kambi ya Sitta na Malecela palifanyika kikao cha kuidhibiti CHADEMA na kuzima azma ya Dr Slaa kugombea urais kupitia chama hicho.
Mtoa habari wetu anaeleza kuwa katika kikao hicho iliamuliwa kama mkakati wa muda wa awali uwepo mkakati wa kuvunja imani ya wananchi kwa Dr Slaa kupitia kuvunja imani ya CHADEMA na utendaji wa Dr Slaa kama katibu mkuu.
Chini ya mkakati huo iliamuliwa kwamba magazeti ya Mtanzania na Rai yaendeshe propaganda za kudumu yenye dhamira ya kuonyesha kwamba CHADEMA ni chama cha udini, ukabila na ubadhirifu wa matumizi ya ruzuku. Kama sehemu ya mpango huo habari za mara kwa mara ziandikwe kumhusisha Chacha Wangwe na Zitto Kabwe na masuala mbalimbali yanayojitokeza ndani ya CHADEMA.
Kwa upande mwingine, gazeti la Mwananchi ilikubaliwa kwamba liibue suala la Dr Slaa kugombea urais. Tayari gazeti hilo katika toleo lake mojawapo la wiki hii limeshamtaja Dr Slaa kama mgombea urais wa mwaka 2010. Mkakati huo pia utahusisha kuhoji jitihada zote za Dr Slaa za kupambana na ufisadi zikihusisha na nia yake ya kugombea urais na kuelezea vita hiyo kuwa ni ajenda ya kusaka madaraka. Habari hizo pia zitahoji utendaji wa Dr Slaa ndani ya CHADEMA na kutaka aondolewe kama ambavyo kuna shinikizo la kutaka Makamba aondolewe kwenye nafasi hiyo ndani ya CCM. Habari hizo zitahusisha kuhoji baadhi ya watu na hata pale watakapokosekana habari zinazoitwa za kiuchunguzi zitaandikwa.
Mtoa habari anaeleza kuwa uamuzi wa kambi kuishughulikia CHADEMA na Dr Slaa hautokani tu na ukweli kuwa Orodha ya Mafisadi iliyotolewa naye Sept 15 mwaka 2007 bali unatokana na hofu kubwa ya ushirikiano wa kiajenda kati ya viongozi wakuu wa chama hicho na wabunge wa ndani ya CCM wanaojiita makamanda dhidi ya ufisadi.
Inatarajiwa kwamba mkakati huo utaweza kuzalisha mgogoro na makundi ndani ya CHADEMA lakini pia utaleta mgawanyiko wa kiajenda ndani ya chama hicho kama ilivyo kwa CCM. Kama mkakati huo ukishindwa kuleta mgogoro ama mgawanyiko basi inatarajiwa walau mkakati huo utasababisha Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu wake Dr Slaa washindwe kukiongoza chama hicho kutokana na mivutano ya moja kwa moja na hivyo chama kupoteza nguvu yake kinapoelekea mwaka 2010.
Chaguzi za marudio za Tarime, Mbeya Vijijini, Busanda na Biharamulo ambazo kwa sehemu kubwa wagombea wake kwa upande wa CCM walitoka kambi inayoitwa ya mafisadi zimetoa ishara kwao kuhusiana na nguvu za CHADEMA kwenye ngazi za ubunge kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Hivyo, namna ya kuvunja nguvu hizo ni kuhakisha chama hicho kinavurugika ama wananchi wanapoteza imani nacho mapema.
Tayari viongozi wakuu wa chama hicho wamekuwa na misimamo tofauti katika hoja zinazohusu ufisadi hali inayoashiria kuanza kwa mpasuko wa kiajenda katika chama hicho. Kwenye masuala hayo mbalimbali Mwenyekiti Freeman Mbowe amekuwa na msimamo sawa na Katibu Mkuu wake Dr Slaa huku Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe akiwa na msimamo tofauti nao.
Baadhi ya masuala yanayotajwa ni pamoja na kuingia kwenye Kamati ya Madini(Bomani), hoja ya Mkapa kustakiwa, Mitambo ya Dowans, taarifa ya Kamati teule kuhusu Richmond na suala la Dr Mwakyembe kuhusu mradi wa kufua umeme Singida. Katika siku za karibuni viongozi hao wametofautiana kimsimamo kuhusu kutenguliwa kwa uteuzi kwa maafisa wa chama hicho David Kafulila na Danda Juju. Wakati Mwenyekiti Mbowe na Dr Slaa wametoa msimamo mmoja wa kupinga utovu wa nidhamu ya kiutendaji na maadili ya uongozi wa maafisa hao, Zitto amemtetea Kafulila pekee akieleza kwamba hatua hiyo imemwonea ikimlenga yeye na kwamba itaathiri nafasi ya Kafulila kugombea ubunge wa Kigoma Kusini ambapo yeye amemwandaa kwa muda mrefu kuwa mbunge.
Dr Slaa amekuwa akikanusha mara kwa mara kuwa hakusudii kugombea urais na kwamba yeye anapendelea zaidi kuwa mbunge wa Karatu. Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambaye aligombea urais mwaka 2005 tayari ameshatangaza kutogombea urais mwaka 2010 na ameelekeza nguvu zake kurejea bungeni kupitia jimbo la Hai ambalo ameliongoza mwaka 2000 mpaka 2005. Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe, yeye ametangaza kugombea urais siku za baadaye. Wadadisi wa mambo wanaeleza kuwa kwa umri wake, hatakuwa amefikisha umri wa kugombea urais mwaka 2010 hata hivyo anaweza kugombea urais mwaka 2015. Wachambuzi wengine wa mambo wanaeleza kuwa mvutano ndani ya CHADEMA kama ilivyo ndani ya CCM unaweza kutokana na nia za wanaotarajia kugombea urais mwaka 2015 ndani ya vyama hivyo.
PM