Elections 2010 Dr Slaa kukosa kura za baadhi ya vijana

Elections 2010 Dr Slaa kukosa kura za baadhi ya vijana

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
9,710
Reaction score
2,240
Leo nilikuwa mtaani nkawahoji vijana wachache kuhusu uchaguzi.
Wachache wao walikuwa wachuuzi wa vitu vidogo vidogo ambao hunyemela bar kupata wateja wengi wao walionekana kuwa wamejiandikisha ila ukimuuliza utaenda kupiga kura.Wengi wao wakasema hawataenda kupiga kura kwa sababu mgombea wanaemchagua miaka nenda rudi hashindi so hawaoni sababu ya kwenda ungua na jua wakati mshindi anajulikana.
Nkawauliza iwapo Slaa atashinda je utashangilia wengi wakajibu ndio,then nkawatwanga maswali kuwa kwa nini usiwe sehemu ya HUO USHINDI wengi wao waliishia kucheka tuu.
Kuna mzee pembeni akadakia Slaa ana support ya vijana wengi ambao wengi hawaendi kupiga kura madhara yake wazee wakienda CCM itaendelea kubaki madarakani daima.
My plea to you all ni kuwaelimisha hawa vijana wetu mbaya zaidi wapo niliokuwa nachart nao ni garaduate bado wana mtazamo kuwa nipige nisipige matokeo yanajulikana.
 
Niliwahi kugusia hili tatizo nikajibiwa hovyo hovyo. Bado watu wengi hawaamini wakipigia upinzani kura zao zitahesabika. Kwa sababu hii wengine wanadai bora kupigia ccm au kutokupiga kura. Kwa bahatibaya hakuna mkakati wa kutumia vyombo vya habari kurekebisha hili tatizo. Kwa kuwa watu wanakereketwa hapa jamvini wanadhani wapiga kura wote wanatembelea hapa
 
Campaign Team ya Chadema CuF na CCM wako wapi wawashauri waende kupiga kura ikiwezekana beba wakapige kura
 
haina ukweli mimi vijana ninaowajua wako gado

Nathani inabidi tuwe makini na watu ambao kila mara wanaponda taadhari zote zinazotolewa hapa. Wana-generalize ushsbiki wao kuwa ni wa kila mtanzania. Kwani ukifanyia kazi tahadhari ndo tunapoteza Uchaguzi? Nadhani ni kinyume chake
 

Attachments

  • DOGOLALA.jpg
    DOGOLALA.jpg
    41.7 KB · Views: 42
Duh inastua sana. ila naamini kwamba jinsi vuguvugu la mabadiliko linavyosogea mbele ndivyo nao watapitiwa na upepo na kufanya maamuzi sahihi hapo oktoba.
Hilo nalo NENO
 
leo nilikuwa mtaani nkawahoji vijana wachache kuhusu uchaguzi.
wachache wao walikuwa wachuuzi wa vitu vidogo vidogo ambao hunyemela bar kupata wateja wengi wao walionekana kuwa wamejiandikisha ila ukimuuliza utaenda kupiga kura.wengi wao wakasema hawataenda kupiga kura kwa sababu mgombea wanaemchagua miaka nenda rudi hashindi so hawaoni sababu ya kwenda ungua na jua wakati mshindi anajulikana.
nkawauliza iwapo slaa atashinda je utashangilia wengi wakajibu ndio,then nkawatwanga maswali kuwa kwa nini usiwe sehemu ya huo ushindi wengi wao waliishia kucheka tuu.
kuna mzee pembeni akadakia slaa ana support ya vijana wengi ambao wengi hawaendi kupiga kura madhara yake wazee wakienda ccm itaendelea kubaki madarakani daima.
my plea to you all ni kuwaelimisha hawa vijana wetu mbaya zaidi wapo niliokuwa nachart nao ni garaduate bado wana mtazamo kuwa nipige nisipige matokeo yanajulikana.

hapo ndio haja ya mwanakijiji inapokuja kuwa inawezekana kuwa sisi wenyewe wapenda mabadiliko tukawakatisha tamaa wapiga kura kkutokana na kulipa kipaumbele suala la wizi wa kura.

So kutokea sasa everybody should be positive about this election. Hii itasadia pia kuwa na stable nation post election period
.
 
Duh inastua sana. ila naamini kwamba jinsi vuguvugu la mabadiliko linavyosogea mbele ndivyo nao watapitiwa na upepo na kufanya maamuzi sahihi hapo oktoba.
Hilo nalo NENO
Kama hawajajiandikisha kupiga kura Oktoba watakuwa wameishachelewa. Ambaye hajaamua mpaka sasa si mpiga kura. Kwa kweli swala la vijana, hasa wa vijiweni, kukosa misimamo linatia shaka. Wao wanaenda kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza Bongo Flava (JK) au kuona helikopta. Lakini hili si tatizo la vijana bali ni tatizo la vyama, hasa pinzani.Havikulifanyia kazi ingawa vilijua kuwa kwa sasa ndiyo block kubwa ya wapiga kura. CCM ina uhakika na vijana wake. Sina uhakika na Chadema, CUF, etc.
 
Maskini weee, huyo mzee nadhani si mmoja wa wale wa africa mashariki ndo maana kasema hivyo maana wale wa africa mashariki ( jumuiya) sidhani kama hata wamejiandikisha watampigia mshkaji, handsome wa bagamoyo
 
Tamasha la Kuhamasisha Vijana Kupiga Kura, Oktoba 23 2010 Viwanja vya Sayansi
 
VIJANA wamehamasika ile mbaya hata wale waliouza kura sasa wanaanza kuzifuatilia kwa waliowauzia.

Hao wanaosema vijana hawatapiga kura aibu iwajae..
 
Hili tatizo lipo pande zote wapo wazee ambao safari hii haweendi kupigakura kwa sababu wanaona CCM itaanguka tu. Kwa hiyo msiangalie upande moja tu hili ni panga linakata sehemu zote mbili.
 
Back
Top Bottom