Huyu bwana Slaa. Disqualification zake:
1. kwanza alikuwa padre, akahasi. Hiyo ni dalili kubwa sana ya udhaifu. Anaweza uza nchi huyu kwa kuwa hana msimamo.
Hujui ni kwanini aliomba kuacha upadre. Unajua maana ya kuasi? Yeye aliomba kuacha daraja la upadre, mtu anayeasi huwa anaondoka bila kuaga au kutoa taarifa. Yeye alifuata taratibu zote zinazotakiwa.
CCM ndio waliouza nchi, nenda kwenye hifadhi za wanyapori vitalu vyote wameuziana wenyewe na vingine wamegawa kwa wazungu.
2. Alikuwa CCM, mpaka leo sisi tunajua tuko naye. Alipogigwa chini 1995 akahamia upinzani. Siyo mpinzani halisia. Mkewe anataka kufuata hiyo.
Kama mnajua mko nae kwanini anawaumiza vichwa na ilihali ni mtu wenu. Kosa la kumpiga chini mpaka leo hii linawatesa CCM na amebaki kuwa tishio kwao miaka yote.
3. Analalamika kuhusu mishahara midogo ya waalimu, yeye hatuwahi sikia amechangia chochote kwa lolote katika maendeleo ya popote
Nenda Jimboni kwake ukaone jinsi alivyochangia maendeleo ya Jimbo lake. Yeye alikuwa Mbunge wa Karatu so mchango wake wa maendeleo uko Jimboni kwake. Pamoja na hayo, hakuishia huko bali pia alikuja kuwatumikia wananchi wote kwa kufichua ufisadi ambao ulikuwa umefunikwa na serikali ya CCM. Kama siyo Dr. Slaa CCM wangekuwa wanajiandaa kuchota EPA nyingine BoT na wala wasingekuwa na wasiwasi na hela ya kampeni.
4. Sidhani kama mtu yoyote hapa JF akipata file chafu akaenda mwembeyanga kutangaza, tukamwona safi kuanzia siku hiyo. Usafi ni tabia.
Wenzako walipewa wafanye kazi ya Richmond, wakafanya nusu. Yeye akipata credible information anaifanyia kazi mpaka mwisho. Muulize Spika wako Mzee Sitta aliyedai kwamba viambatanisho vya tuhuma za ufisadi vilikuwa vya kughushi, akapeleka polisi ili wachunguze, mpaka leo hakuna feedback, sana sana ni swala la kuibuka kwa EPA na akina Mama Meghji kumwaga sembe.
Unajua kama mtu ni mchafu hawezi kuwa na jeuri ya kumnyooshea kidole mtu mwingine. Ndiyo maana waziri Sofia Simba alisema ndani ya CCM hakuna msafi hata mmoja, wote ni wachafu. Kwa hiyo wasinyoosheane vidole. Kama Dr. Slaa angekuwa na madudu angeishapelekwa mahakamani siku nyingi sana.
5. Huyu ana nyumba ndogo lukuki kila sehemu, disqualification kubwa sana. Dodoma ana wanawake watano.
Hayo ni maisha binafsi ya mtu, pamoja na hayo inaweza kuwa ni uzushi. Labda tukuulize wewe kwamba kulikoni Mkuu wa Kaya kila siku anajitetea kwamba hajaoa mke mwingine na ilihali kwenye magazeti kuna habari hizo? Kama ni habari za uzushi, kwanini haendi mahakamani kufungua kesi za madai ama kupeleka malalamiko ili magazeti hayo yafungiwe?
Ukianza kuongelea nyumba ndogo, hakuna kiongozi wa CCM kuanzia ngazi za juu na serikalini ambaye atasimama na kuonyesha usafi/uadilifu wake. Kwa hiyo kwenye hiyo angle itakula kwenu maana uchafu huo ni mkubwa sana ndani ya CCM na serikalini. Ndiyo maana ukipeleka hiyo hoja huwa inapigwa majibu ya kiswahili.
6. Security-wise, baadhi ya mambo hata senators wa US hawawezi sema. He is incompetence. Tutamnyung'unyiaa hapo
Mambo yepi? Hawasemi mambo yanayogusa usalama wa nchi yao, lakini kama kuna ufisadi kwenye deals za majeshi watasema. Kama kile anachosema Dr. Slaa kingekuwa kinahatarisha usalama wa taifa, sasa hivi angekuwa gerezani siku nyingi. Hakuna mahakama inaweza kumfunga kwa kusema kile ambacho kina maslahi kwa nchi na wapiga kura wake na ndiyo maana hata yale madudu ambayo serikali inaita ni SIRI yeye anayo na anatembea nayo na alimwambia Mh. Pinda aende kumshika maana ana manyaraka kibao yenye nendo ya serikali na mhusi wa SIRI.
7. Alikuwa hana mpango wa Urais. Amelazimishwa. Urais siyo wa kulazimshwa. Ni plans za miaka mingi. Anaweza tuyumbisha huyu
Ni kweli hakuwa na mpango wala wazo, ni wananchi wenye uchungu na nchi hii ambao wamemuona ana uchungu na nchi yake ndio waliomuomba, hawakumlazimisha. Mipango ya muda mrefu hiyo ndio ilituletea mafisadi ambao bado tunao mpaka leo. Mkapa alipochukua fomu hakuna aliyetegemea kwamba angepita na hakuwa amefanya maandalizi yoyote. Kwani unajiandaa ili uandae mafisadi ili ukichaguliwa waje waifisadi nchi?
8. Watu alionao ni wachafu sana,, hatutegemei mtu kama yeye akawa na watu wa namna hiyo.
Uchafu wao ni nini? Hivi kuna watu wachafu kama vigogo wa CCM? Ufisadi umewazunguka kila kona, hakuna ufisadi unafanyika bila kuona majina yao na hao ndio vipenzi wa JK na ndio waliomzunguka.
Tafuteni hoja nyingine za kum-disqualify Dr. Slaa na siyo hizi ambazo hazina mashiko.